CDF Mstaafu Mabeyo ametaka kufikisha ujumbe. Je, wananchi tumeuelewa ujumbe?

CDF Mstaafu Mabeyo ametaka kufikisha ujumbe. Je, wananchi tumeuelewa ujumbe?

View attachment 2937945
Gen Venance Mabeyo akiwa na viongozi waandamizi wa Ulinzi na Usalama

Nimesikiliza clip ya mahojiano ya Mstaafu CDF Gen Venance Mabeyo na mwandishi wa habari wa gazeti la serikali, Daily News.

Udhubutu wa kuyaweka mambo wazi ni kipaji na ujasiri ambapo nampongeza kwa dhati Gen Mabeyo kwa hilo.

Mambo mengi imekuwa utamaduni kuyafutika futika na hivyo ukweli kutojulikana.

Kwa dhamira njema kabisa, Gen Mabeyo amethibitisha kuliweka mbele Taifa kama kiapo chake kinavyomtaka, kulinda Katiba.
Huu ni ujasiri usio kawaida, maana kwa watu walafi wangeweka maslahi yao mbele kuliko matakwa ya Taifa na Katiba.

Tunaona umuhimu wa viongozi waadilifu, ambao siku hizi ni wachache.

Mungu akulinde Gen Mabeyo.
Mwambie pia..ule unafiki alioshiriki kuwafanyia watanzania bado hajatubu, bado anao muda kuutubu wananchi wamsamehe! asipofanya angali hai mwambie pale safari yake itaishia..
 
Kuna kitu nimejifunza, mfano unaposajili anwani katika internet hutaka uweke password, unapo weka password mara nyingine inakataa kwa vile password uliweka ni nyepesi, hivyo hutaka strong password.

Hivyo kwenye katiba yetu kuna vitu vya umuhimu vimewekwa ila vinachukuliwa kwa wepesi sana.

Inapotokea nafasi ya kuchagua au kuteua unateua kwa kuangalia vionjo fulani fulani hivi!
Anateuliwa mtu kwa vile ni mwanamke!
Anateuliwa mtu kwa vile ni Mzanzibari!
Anateuliwa mtu kwa vile mmesoma nae au baba yake ni rafiki yako.
Anateuliwa mtu kwa vionjo na si kwa weledi!

Kuna wakati inaweza kugharimu.
 
Mara ngapi unataka? taifa ni masikini sababu ya vitu kama hivi
 
Back
Top Bottom