CDM mkija na sera ya kufunga mipaka ili bei ya chakula ishuke mtapotea vibaya sana

CDM mkija na sera ya kufunga mipaka ili bei ya chakula ishuke mtapotea vibaya sana

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Pengine mmesahau, hii sera ya kufunga mipaka ambayo Bashe anaitekeleza ni sera ya CDM. Wakati wa uchaguzi wa 2020 Salumu Mwalimu kila alikokwenda alisema kuwa CDM ikishika madaraka wananchi watauza mazao yao kokote kule, ilimradi tu wamelipa kodi ya serikali. Ilikuwa sera moja bora sana.

Sasa Bashe na serikali ya CCM waliona sera hiyo ni mtaji mkubwa sana kwa wakulima wa Tanzania ambao ni zaidi ya 60 percent. wameichukua na wanaitelekeza. Sera hiyo lazima ilete ongezeko la bei ya chakula na ongezeko la bei ya chakula na mfumuko wa bei wa wastani si kitu kibaya.

Ni kitu muhimu sana katika kuchochea uchumi. Kwa hiyo hii sera ya kuacha mipaka wazi si tu ya kujipatia umaarufu kwa wakulima, ni sera sahihi kwa uchumi.

Sasa ni vyema CDM mkawa na sera ya kupunguza bei ya chakula bila ya kupinga hii sera, mkipinga hii sera ya kuuza mazao nje mtapoteana sana.
 
Huu ujinga wa kupunguza bei ya vyakula kwa kuwabania wakulima masoko ya nje ni sera mbovu na ya ubinafsi, kama kuna mtu anaona chakula ni ghali mapori yamejaa aende akalime.
 
Sio kwa bei kubwa sasa inabidi iwe bei ambayo ni rafiki, sasa kenya si watanunua Chakula sana kutoka Tanzania,
Na kitu kingine wakulima hao hao ndio huuza mazao yao yote wakitegemea mvua kisha mvua inasumbua sasa wao ndio wanabaki wanaumia na njaa.
Wakulima wengi huwa hawafaidi kabisa bali wafanya biashara, sasa wajinga wengi wanahisi labda ndio muda wa mkulima kupiga hela kumbe hakuna sababu wafanya biashara wakubwa huwa wanaenda wanakusanya mazao msimu wa mavumo ambapo mazao huuzwa kwa bei ndogo kisha wanaweka kwenye maghara wanasubiri wayauze baadae.
Sasa hapa ukiwa na akili kama huyu mjinga mtoa mada una mkulima anafaidika kumbe hata sivyo.

Na jambo lingine lililosababisha mazao kupanda ni kwa sababu msimu wa mwaka jana hakuwawa na mvua za kutosha.
 
Huu ujinga wa kupunguza bei ya vyakula kwa kuwabania wakulima masoko ya nje ni sera mbovu na ya ubinafsi, kama kuna mtu anaona chakula ni ghali mapori yamejaa aende akalime.
Mkulima gani wa tanzania anauza mazao nje ya nchi zaidi ya matajiri na madalali wa mazao? Hii bei wanayouza hao madalali mkulima angeipata hata nusu yake wangekuwa mbali sana.
 
Back
Top Bottom