CECAFA KAGAME CUP 2011 Finals in Tanzania

CECAFA KAGAME CUP 2011 Finals in Tanzania

SImba yanga.JPG
Mkijaaaliwa kuvuka kesho tutawauliza
 
Tunaimba ccm ccm KWA YANGA sio kwa sababu ya rangi,ni kwa sababu wanabebwa japo mara nyingine hawabebeki. ingekuwa rangi ya jezi tungeanza zamani siyo leo. WANABEBWA KAMA MIZIGO NA KAMA CCM
 
nimeanza kuamini sisi watanzania tuna matatizo makuubwa sana

yaani hata hili la historia za simba na yanga linapindishwa?

timu zote yaani simba na yanga zilishiriki saaana kwenye kupigania uhuru

na mpaka kuundwa kwa ccm

ndo maana uwanja wa yanga ni uwanja wa karume,
na karume huyo huyo ndie aliezindua jengo la simba,msimbazi
kwa ufupi timu ya yanga ilikuwa ni sehemu ya wana tanu na baadae wana ccm kukutana

simba baadae ilichukua mkondo wa wasfanyabiashara,but na wao wameanzia huko....

sasa asili ya kushangilia ccm ni hiii
kutokana na yanga kuwa na jezi zinazofanana na ccm
ni yanga wenyewe ndio walioanza kushangilia kwa kuimba ccm ccm ccm......

baadae simba waliuchukua huo wimbo ili kuwakejeli yanga.....
yaani badala ya yanga kuimba ccm wakishinda,
simba waliimba ccm,yanga ikifungwa
 
...hata barca wanabebwa! Yanga Bomba, Yanga Imara!
 
Jana katika tukio ambalo sikulitarajia ni Juma Kaseja kusema yupo peke yake hapa Tz..
Nimebaki na maswali mengi kichwani
1. Je alikuwa anawalenga wale ambao wallimbeza kwamba amekwisha kimchezo?
2.Au alikuwa akimwambia Babu Poulsen kuwa yeye ni mvinyo wa siku nyingi hata kama asipomwita bado nabaki kuwa TZ one?
3.Kwanini aliandika maneno hayo katika lugha ya kiingereza au kwa vile supersport wapo Tanzania au alitaka kufikisha ujumbe kwa Poulsen bila chenga?
4.Kaseja bado anakiwango kinachofanana na maneno yake?

Mwisho wa siku Tunampongeza sana Juma Kaseja kwa kufanya kazi 3 jana za ukweli mfano uwanjani jana alikuwa kama kocha msaidizi, kepteni wa timu na kuipeleka timu fainali...saaaaaaaaaaaafi sana JUma k Juma
 
Juma K Juma............Is the Only and Only One!
Namkubali!~
 
Mechi ya jana vijana wa msimbazi walitotoa watanzania kimasomaso ingawa dakika 30 walikuwa wamepoteza mwelekeo. Nawatakia kheri vijana wa Jangwani leo waweze kututoa kimasomaso watz!
 
wanashangilia ivyo kwasababu Yanga inafadhiliwa na Mafisadi toka CCM wakiongozwa na Mtoto wa JK nyuma yupo Manji na pia kwasababu yanga mara nyingi uwa inapendelewa na uwanjani kwasababu ya serikali inayoongoza TFF so kuimba vile ni kuwatania mnapendelewa koz mpira hamjui...

kwa hiyo haya Magamba yatakapoacha kujiingiza Yanga hawataitwa tena CCM? Lkn sioni kama yataacha kujichomeka kwenye mipira manake mpira una nguvu sana. kupitia mpira unaweza hamasisha watu wakafanya vitu vikubwa sana. ndo maana enzi za TAA walipitia mpirani kufikishiana ujumbe wa ukombozi. mmh kazi wanayo Yanga. manake CCM watakapotoka madarakani wataendelea kuchekwa...
 
Tunaimba ccm ccm KWA YANGA sio kwa sababu ya rangi,ni kwa sababu wanabebwa japo mara nyingine hawabebeki. ingekuwa rangi ya jezi tungeanza zamani siyo leo. WANABEBWA KAMA MIZIGO NA KAMA CCM

kwa hiyo kama Yanga wanabebwa kama CCM wabebwavyo, japo wote hawabebeki, so hata Rage nae alibebwa kule Tabora? na yeye akiwa uwanjani atawashangilia Yanga kama CCM! CCM!?
 
Acha zako ww ni Simba damu, huo U taifa staz unaoongelea unataka kutuibia tu, na kama ni kweli ww sio mshabiki wa simba ama yanga basi ww sio Mtanzania (najua zipo timu nyingi na kwa hapa unaweza kuchangia unavyoweza)

pole sana Obe. sio Watanzania wote wanamwelekeo wa Simba/Yanga, hata kama ni wapenzi wa soka. mimi ni mmoja wao.
 
Naona upendeleo wa wazi kwa timu zetu.
Nadhani ni mpango mahsusi wa waandaaji na TFF ili kombe libaki nchini.
Kwa namna hii ya uongozi wa soka, tutakuwa tukiporomoka kwenye jedwali la FIFA kila kukicha.
TUBADILIKE
 
Nijuavyo mimi Historia ya Timu hizi ndo inapelekea yote haya. Yanga iliyoanzishwa miaka ya 1930 kama sikosei 35 to be specific ilitumika sana kuwakutanisha wapigania uhuru akiwemo mwalimu nyerere na kwakuwa mikutano ya kisiasa haikuruhusiwa/ilikuwa discouraged na wakoloni timu hii ilitumika kama kichaka cha kujifichia na watu wakakutana hapo wanacheza mpira huku mipangilio mingine ikiendelea. Hivyo kuna uhusiano mkubwa wa kihistoria kati ya vyama TAA, TANU baadaye CCM aka Magamba. Simba kwa upande wao walikuwa timu ya waarabu..... Pengine hii ndio asili ya Yanga kushangiliwa CCM,CCM na pia Mwalimu nyerere kuwa mpenzi mkubwa wa Yanga. Ushahidi mwingine ni Jezi ya Yanga. Kwa uchache nayakumbuka hayo.
Mkirua uko kkaribu na ukweli. Yanga ilanzishwa na wanaharakati wa kudai uhuru wa Tanganyika Hayati Mzee Karume akishirikiki kamilifu uanzishwaji wa klabu hiyo ambayo iltumika kama chombo chinichini cha harakati za mapambano dhidi ya ukoloni.
Kuona hivyo baadhi ya waafrika waliokuwa wakiupenda utawala wa waingereza nao walianzisha klabu yao iliyounga mkono utawala wa mwingereza waliyoipa jina la "Sunderland Sports Club." Nyerere na Karume walikuwa wapenzi wa Yanga kutokana na historia hiyo ila Karume alikuwa muwazi zaidi kwaupenzi wake kwa klabu aliyosaidia kuiasisi hadi kutoa fedha za ununuzi wa kiwanja na ujenzi wa klabu miaka ya mwisho wa sitini ambapo inasadikika kwamba kwa ushauri wa wazee wenye busara Mzee yule alitoa pia fedha kwa klabu ya Sunderland ili nao kama Yanga ziwasaidie kujenga makao makuu. Katika mgao ule Yanga ndiyo walipewa kiasi kikubwa. Ufisadi uliojitokeza baadae ulitaka kukwamisha ujenzi wa Jengo la Yanga ingawa ulikwamuliwa baadae na watu walioitakia mema klabu hiyo.
Chanzo cha Simba kushangilia CCM ni tambo za Yanga kwamba kwa vile wao ni sawa na Umoja wa Mataifa, kwani wao na chama pekee tawala cha enzi zile cha CCM walikuwa damu damu. Simba wao nao waliamua kujiita Taifa Kubwa kwa mantiki kwamba hata bila ya Support ya CCM wao wapo na wana nguvu tosha za kuikabili Yanga. Si viongozi wote waliokuwa kwenye chama na serikalini walikuwa Yanga, kwa mfano hayati Mzee Kawawa katika uhai wake alijitanabaisha kwamba yeye alikuwa mpenzi wa dhati wa Simba na hakukuwepo mgogoro wala uhasama wowote baina yake na wenzake.
Kwa miango kadhaa sasa Simba wanawatania watani zao Yanga wanapoifunga timu wanayocheza nayo au Yanga wanapofungwa au kukosea kwa kelele za CCM, CCM, CCM.... na yanga nao inapofungwa Simba husikika wakishangilia " Simba, Simba......." kiasi kama unasilikiliza kwenye redio unaweza kudhani Simba imefunga bao kumbe imefungwa na ni kelele za watani zao Yanga kuwakejeli.

 
Mkuu,
Usihisi bali ndio UHALISIA.
Elewa kuwa TFF & CECAFA hawaangalii kombe linaenda wapi, bali je gharama za kuendesha mashindano zinarudi vipi na kupata salio la kuendesha CECAFA kwa mwaka mzima. Maana zikikutana timu hizo gharama zooote za uendeshaji zitajilipa huku salio zuri tu likibaki.
 
Nijuavyo mimi Historia ya Timu hizi ndo inapelekea yote haya. Yanga iliyoanzishwa miaka ya 1930 kama sikosei 35 to be specific ilitumika sana kuwakutanisha wapigania uhuru akiwemo mwalimu nyerere na kwakuwa mikutano ya kisiasa haikuruhusiwa/ilikuwa discouraged na wakoloni timu hii ilitumika kama kichaka cha kujifichia na watu wakakutana hapo wanacheza mpira huku mipangilio mingine ikiendelea. Hivyo kuna uhusiano mkubwa wa kihistoria kati ya vyama TAA, TANU baadaye CCM aka Magamba. Simba kwa upande wao walikuwa timu ya waarabu..... Pengine hii ndio asili ya Yanga kushangiliwa CCM,CCM na pia Mwalimu nyerere kuwa mpenzi mkubwa wa Yanga. Ushahidi mwingine ni Jezi ya Yanga. Kwa uchache nayakumbuka hayo.

Hapo zamani huu ushangiliaji ulianzia kwa CDA ya Dodoma, kulikuwa na mashindano ya vilabu yalifanyika, sikumbuki vizuri, CDA walishiriki na yalifanyikia Dodoma, kwa mapenzi na timu yao, mashabiki hao, kila CDA walipokuwa wanafunga goli, walikuwa wanaimba, CDA...CCM...,hivyo kufanya aina hiyo ya ushangiliaji kuwa ndo style yao. Sasa kama mjuavyo hawa watani zetu huwa hakiwapiti kitu, wakajiona wao ni kama timu ya chama na serikali, wakauteka ushangiliaji huu na kuufanya mali yao, wakawa wakifunga goli na wao wanaimba ccm.


Sisi Simba kama kawaida yetu tukaja na ushangiliaji huu lakini katika namna ya kejeli, kwamba kila wanapofungwa goli na sisi tunaimba ccm. Hii ni katika namna tu ya kuboresha utani wa jadi, si unajua kuwa Simba huwa tunabuni sana vinogesho vya ushangiliaji, na tukafika umbali hadi wa kuhesabu pasi za timu pinzani inapoihenyesha yanga.
 
Swali ni kwanini simba wanashangilia ccm? Na sijengine watu wanaenda nje ya mada kwanza naingia ndani ya mada .... Simba wanashangilia ccm ni moja ya ushabiki wa utani yanga inaonekana kama ni ccm rangi zake na watu wake... Kama ilivyokuwa simba kipindi kile wachezaji wazee, yanga ilikuwa ikiimba shikamoo na simba wanaitika marahaba. Natoka nje ya mada sasa ukitaka kujuwa chimbuko la yanga sio nyerere jamani... Yanga ilikuwa yakina mzee mangara kabla huyo nyerere dar-es-salaam hajakanyaga na ukitakak ujuwa historia ya mzee mangara ndio aliyekuwa tajiri mjini dar-es-salaam mzee wa kizaramo na unaweza kusema ndio alikuwa katika mafisadi wa mwanzo waliomsaidia bakharesa mjini hapo na nyerere alivyokuja alisaidia vingi tu ndio sasa libeneke ccm wanaliendeleza kwa yanga na kina rostam na manji na yule wa chama cha mpira kina tenga na sasa hivi yanga hutoiona kwenye mgogoro sababu ya rais, mgogoro wao utakuja kwenye wivu wa madaraka ya kuitafuta pesa za magendo kutumia timu kuleta bizaa zao. Na kama tunavyojuwa yanga timu ya wabishi wabishi ipo kisiasa turudi kwenye simba... Simba ni timu sio watu wasiasa ila matapeli wa mjini wenye pesa zao ok unawezak usema wote mafisadi... Ila ufisadi wa yanga upo kisiasa zaidi chunguza utaona. Tunarudi kwa mzee mangara ndio aliyeivunja yanga ikawa pan african kwa ufisadi wa kisiasa ulipoanza kwenye timu. Timu zetu zinaharibika sababu ya mambo ya kisiasa.
 
Mechi inakaribia kuanza (Yanga na St.George): leo Jerry Tegete ndani ya nyumba: Gumbo, Kiiza, Mrope na Asomoah wako Benchi
 
kila timu imekoswakoswa kwa wakati wake dk za mwanzo kabisa.
 
Back
Top Bottom