Salama wakuu?Kwanza kabisa nitoe shukrani kwa wakuu zangu wote PrN-Kazi,Saitama_Kein,Mkwasa,Katavi,Gazeti,Kakalende na wengine wote kwa kuendeleza libeneke hiyo jana......Niliondoka ghafla hewani baada ya kupata tatizo(la msiba wa rafiki yangu) hali iliyonilazimu nianze kujiandaa kwa safari kwa ajili ya kuwahi mazishi hivyo kushindwa kufuatilia kilichokuwa kikiendelea uwanjani.....Thank God hakuna kitu kilichoharibika hiyo jana.....Napenda tu kuwapongeza Yanga na watanzania kwa kuweza kutupa matumaini ya kulibakiza kombe hapa nyumbani Tanzania...Hongereni sana wana Yanga wenzangu...Kuhusu kubebwa.....Pamoja na kuwa mnazi mkubwa sana wa Yanga nachelea kusema kwamba Yanga katu hawajabebwa kwenye mechi ya jana wala kwenye mechi ya robo fainali.......Nadhani kama lengo lilikuwa ni kubebwa basi marefa wangehakikisha Yanga wanapata ushindi ndani ya dakika 90 ama 120 na si kusubiri mpaka wakati wa penati......Kuna tofauti kubwa sana kati ya penati ya Nadir Haroub na ile ya Antony Bongole....Penati ya Nadir iligonga mwamba ikaingia ndani(ikavuka msitari wa goli) lakini penati ya Bongole iligonga mwamba ikarudi ndani(ikawa njea kidogo ya msitari wa goli) na Super Sport walijaribu kuirudia kwa angle zote ikaonekana si goli,na hata wakati wa kipindi cha Jambo Tanzania cha TBC leo asubuhi Pendael Omary amerudia penati zote mbili na kuonesha tofauti kubwa kati ya penati zile...Hata kocha wa St. George Dossena alipohojiwa na Thomas Mlambo wa Super Sport alikiri kwamba lile si goli na alipata uhakika wa kwamba si goli baada ya kuangalia Replay ya penati ile.....Pia hata mtangazaji Thomas Mlambo akihojiwa na mtangazaji Charles Mwabeya wa TBC Taifa leo asubuhi alisema kwamba yale yalikuwa ni mamuzi sahihi kabisa,ni kweli penati haikuingia ndani ya goli na hata yeye(Mlambo) ameongea na kocha Dossena wa St. George kamwambia ni kweli ile penati haikuingia,so maamuzi ya refa yalikuwa halali kabisa.....Cha msingi ni timu zetu Simba na Yanga zijipange vizuri ili watupe burudani hiyo kesho maana iwe isiwe ni lazima kieleweke na mmoja wao achukue kombe hiyo kesho.....Btw.....Kuna taarifa kwamba watani zangu Simba kesho watawakosa Jerry Santo,Juma Kaseja na Amir Maftah,ni kweli?........Hizi zitakuwa habari mbaya sana kwa Simba.....Tukutane basi hiyo kesho hapa hapa JF....Bala.