Hongera zake mh mbunge Cecil mwambe kwa kujitokeza hadharan na kutangaza kuwa mwaka huu atawania uenyekiti wa chama chake cha CHADEMA na kwa mujibu wa maelezo yake ameshachukua fomu ya uongozi huo mkubwa ndani ya chama chake.
Bila shaka bwana mwambe amesha soma na kujua wenzake huko nyuma nini kiliwatokea pale walipotangaza mabadiliko ya uongozi kwa ngazi ya Taifa kwa kutaka kungombea nafasi hiyo nyeti ndani ya chama kwani harakati za mabadiliko ya uenyekiti yalianzia zaman sana kabla ya bwana freeman mbowe kuwa mwenyekiti kulikuwa shwari, baada ya hapo wote mnakumbuka wakina hayati Chacha Wangwe na wenzake kilicho wapta baada ya tu ya kutaka nafasi hiyo uenyekiti, wakaja wakina Zitto Kabwe, Dr. Kitila Mkumbo, Samson Mwigamba Kwa uchache walipatwa na nini baada ya kutaka mabadiliko ambayo leo ndugu mbunge Mwambe ametangaza hadharani.
wote walionesha nia ya kutaka mabadiliko waliitwa kila majina mabaya na machafu mala wasariti, wame nunuliwa na CCM hawajui kuongoza zaidi ya Mbowe mwisho wa siku wakafukuzwa uanachama na kunyangwanya kadi ya chama hofu yangu sidhan kama haya yote bwana Mwambe amesahau najua ankumbuka vizur kilichowakuta wenzake hawa na atakuwa amejipanga kukabiliana na rafu na hujuma kama hizo ajakurupuka tu.
Picha linaanza ndani ya chama baadhi ya wanachama na viongozi wake wameshaanza kumpiga zengwe kuwa hatoshi anauwezo, acha lile la vijana buku kuchangishana zaidi ya milion 5 kwenda kumchukulia mh. Freeman Mbowe fomu ya kugombea uenyekiti hii yote ni mbinu tu ya kuwakatisha tamaa watu kama wakina Mwambe wasijitokeze kwenda kuchukua fomu na kuogopa kuona kama vile Mbowe bado anakubalika ndani ya chama ni mbinu mfu ya kizaman ambayo Mbowe ameitumia.
ila Konde Boy huyu kama yupo serious atakaza mwanzo mwisho na kuruka viunzi vya hujuma hizi anaweza toboa na CHADEMA kupata mwenyekiti mpya maana kuna zile za chini ya kapeti kuna baadhi ya wabunge hawamtaki Mbowe apishe watu wengine nao waoneshe uwezo wao hawa wanachagizwa na sera ya mbowe ya kuwakata wabunge 10m za kuendesha chma na wasijue matumiz yake, ila kwa sasa wabunge hawa wamekaa kimya kuogopa kushugulikiwa na wakubwa wao.
Je Mwambe atauweza mfupa ulioshinda fisi? yetu macho