Cecil Mwambe: Sihitaji mtu anichukulie fomu, nitaenda kuchukua mwenyewe ila tuwe pamoja kwenye kampeni kama mnanikubali

Cecil Mwambe: Sihitaji mtu anichukulie fomu, nitaenda kuchukua mwenyewe ila tuwe pamoja kwenye kampeni kama mnanikubali

Hii ya mbowe kuigiza kuchangiwa pesana kuchukuliwa form nidariri za uoga nakutaka kuwafanya wengine wasigombee , mimk mwanachadema sisi huku kimara mbowe na myika hatutaki haya kuwasikia
Kajifunze kuandika then rudi hapa.....TUKUCHAPE MBOKO
 
Mbowe tangu awe m/k amejitahidi kukijenga chama anapaswa kupongezwa lkn huyo mwembe angetuli maana hawezi kupita
 
Ni hatari sana kumpa mtu mwenye njaa madaraka lazima atawasaliti tu. Kwasasa Mbowe ni mtu sahihi sana hao wengine watasaliti tu
 
Chadema waonyeshe demokrasia wanayoihubiri ndani ya chama.yeyote anayetaka kugombea achukue fomu, wanachama wataamua.
 
Hongera zake mh mbunge Cecil mwambe kwa kujitokeza hadharan na kutangaza kuwa mwaka huu atawania uenyekiti wa chama chake cha CHADEMA na kwa mujibu wa maelezo yake ameshachukua fomu ya uongozi huo mkubwa ndani ya chama chake.

Bila shaka bwana mwambe amesha soma na kujua wenzake huko nyuma nini kiliwatokea pale walipotangaza mabadiliko ya uongozi kwa ngazi ya Taifa kwa kutaka kungombea nafasi hiyo nyeti ndani ya chama kwani harakati za mabadiliko ya uenyekiti yalianzia zaman sana kabla ya bwana freeman mbowe kuwa mwenyekiti kulikuwa shwari, baada ya hapo wote mnakumbuka wakina hayati Chacha Wangwe na wenzake kilicho wapta baada ya tu ya kutaka nafasi hiyo uenyekiti, wakaja wakina Zitto Kabwe, Dr. Kitila Mkumbo, Samson Mwigamba Kwa uchache walipatwa na nini baada ya kutaka mabadiliko ambayo leo ndugu mbunge Mwambe ametangaza hadharani.

wote walionesha nia ya kutaka mabadiliko waliitwa kila majina mabaya na machafu mala wasariti, wame nunuliwa na CCM hawajui kuongoza zaidi ya Mbowe mwisho wa siku wakafukuzwa uanachama na kunyangwanya kadi ya chama hofu yangu sidhan kama haya yote bwana Mwambe amesahau najua ankumbuka vizur kilichowakuta wenzake hawa na atakuwa amejipanga kukabiliana na rafu na hujuma kama hizo ajakurupuka tu.

Picha linaanza ndani ya chama baadhi ya wanachama na viongozi wake wameshaanza kumpiga zengwe kuwa hatoshi anauwezo, acha lile la vijana buku kuchangishana zaidi ya milion 5 kwenda kumchukulia mh. Freeman Mbowe fomu ya kugombea uenyekiti hii yote ni mbinu tu ya kuwakatisha tamaa watu kama wakina Mwambe wasijitokeze kwenda kuchukua fomu na kuogopa kuona kama vile Mbowe bado anakubalika ndani ya chama ni mbinu mfu ya kizaman ambayo Mbowe ameitumia.

ila Konde Boy huyu kama yupo serious atakaza mwanzo mwisho na kuruka viunzi vya hujuma hizi anaweza toboa na CHADEMA kupata mwenyekiti mpya maana kuna zile za chini ya kapeti kuna baadhi ya wabunge hawamtaki Mbowe apishe watu wengine nao waoneshe uwezo wao hawa wanachagizwa na sera ya mbowe ya kuwakata wabunge 10m za kuendesha chma na wasijue matumiz yake, ila kwa sasa wabunge hawa wamekaa kimya kuogopa kushugulikiwa na wakubwa wao.

Je Mwambe atauweza mfupa ulioshinda fisi? yetu macho
 
Ana kifua cha kutouza chama kwa makapi ya ccm(lowasa) kama mbowe alivyofanya
 
Kiuhalisia Mbowe anatakiwa aachie madaraka chama kisonge mbele kumekuwa na manung'ununiko ya chini kwa chini na hii sio nzuri.
Kinadharia Cecilia hawez pambana na Siasa za upinzani against CCM. Mbowe atafia madarakani pale.
 
Ana kifua cha kutouza chama kwa makapi ya ccm(lowasa) kama mbowe alivyofanya
Chukueni hilo pandikizi lenu.
1572191509422.jpeg
 
Kiuhalisia Mbowe anatakiwa aachie madaraka chama kisonge mbele kumekuwa na manung'ununiko ya chini kwa chini na hii sio nzuri.
Kinadharia Cecilia hawez pambana na Siasa za upinzani against CCM. Mbowe atafia madarakani pale.
Sumaye je?!
 
Hili LA Cecil Mwambe, na Ugombea Uwenyekiti.

Linanikumbusha LA Mama Anna Mgwira na Uwenyekiti wa ACT
 
Back
Top Bottom