Celebrities wa Bongo kuweni na wanasheria wa kushughulikia mambo yenu nyeti

Down To Earth

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2011
Posts
21,940
Reaction score
16,643
wakuu, nimekuja na neno hili baada ya kushuhudia wema Sepetu alivyofanya fujo na kujidhalilisha ndani ya Ofisi za GPL..

kwa kweli kwa jambo kama lile, sidhani kama wema sepetu alistahili kwenda yeye kama yeye kama kweli aliona ameonewa na uongozi wa Global Publishers Limited..

huu ni wakati sasa wa wasanii wetu kuiga mifano kwa wasanii wakubwa wa nje kama Chriss Brown, J-z ama msanii yeyote yule, wasanii wetu wanatakiwa kuwa na wanasheria wa kushughulikia mambo yao nyeti kama dai la Wema sepetu kama kweli aliona ameonewa..

hebu tujiulizeni wakuu,

--hivi ilikuwa ni sahihi kwa wema sepetu kwenda ofisi za GPL na kufanya fujo na kujiita kichaa?
--kwa picha alioinesha wema mpaka kuvua viatu na kupigana na uongozi ndani mle, je ile imemjenga ama imembomoa?

nimebaki najiuliza sana kwanini wema sepetu hakuchukua hatua za kufungua mashtaka mahakamani badala yake akaenda mwenyewe kufanya fujo???

nadhani sasa wasanii wetu wafikie kipindi cha kumiliki wanasheria wao binafsi, wema angeweza kulipwa kwa madai yake endapo angepata mtu wa kumsimami kisheria....



kwa incident ile, kampuni nzima na uongozi wa GPL una haki ya kumshtaki wema sepetu kwa kuwafanyia fujo na kuwazalilisha kwa mameno machafu...

celebrities wetu jamani jipangeni kwenye mambo yenu, tafuteni wanasheria wa kusimamia mambo yenu kiujumla..
 
Na jana tu katapeliwa pesaa na petiti man wakuacheee hana hata wazo la mwanasheriaaa
 
uhuru wa habari unawapa fursa wahandishi kufanya wanavyotaka,,so inabidi uwe fiti kichwani kupambana nao,kama hawana uthibitisho wa habari wanazotoa unaweza kuwadai fidia.....sasa Wema ni kichaa kweli na waliiomzunguka as washauri sio vichaa wao ni matahaira kabisa,,,unategemea nini hapo?
 
Na jana tu katapeliwa pesaa na petiti man wakuacheee hana hata wazo la mwanasheriaaa

katapeliwa na nani tena mkuu??

ile video nimeiona vizuri sana alipofanya fujo GPL, na huyo anaejiita mlinzi wake yuko nyuma na rasta zake tu hafanyi chochote.. sijui kazi yake hasa ni nini??
 

mkuu unadhani kwa habari kama ile kama ingepata mtu wa kuisimamia haswa, GPL wangeshinda??

mkuu nimeamini kweli wema ni kichaa, hata siku moja hatopata nafasi ya kuigiza na omotola J.
 
Ila ukiangalia kwa undani wao wenyewe wanataka warushwe,usije kushangaa Wema kuvamia GPL nayo ikawa ni mbinu tu ya kuandikwa gazetini
 
Hiyo ni fursa walionyimwa wanasheria. Hapa wangempata msanii asuyeendekeza hayo mambo ingekua mtaji.

Hata mwanasheria wa bongo movies basi awepo ila wapi.

Ila kuna jambo moja hapa mi ninalojua. Ni kwamba wasanii wanatumia vyombo kuwika na kupata sifa. Sasa ikizidi au ikaenda kinyume wanageuka mbogo.

Huyo mwanamke asiye na stara anaenda karibu na kamera na amevaa nguo nusu makalio anategemea nini kama sio kujionyesha? Hawa wanatumia vyombo vizuri tu. Leo ukishika gazeti la udaku utasikia 'ooh nimeacha kuliwa kinyume na maumbile' seriously? Vyombo na wasanii vinatumiana. Muelewe hilo. Nawasilisha
 
Ni ngumu sana Shigongo kumshitaki Wema kwani anawaingizia hela nyingi kwenye magazeti yao
 
Ni ngumu sana Shigongo kumshitaki Wema kwani anawaingizia hela nyingi kwenye magazeti yao

hili nalo neno mkuu, kweli wataanguka kwa kiasi fulan kibiashara!
 
Mkuu Excel umetoa ushauri mzuri sana lakini unatakiwa kujua hawa unao wapa ushauri hizi skendo wanazipenda na kuzitafuta.

Ukiangalia swala la Wema uhitaji kutumia akili nyingi kukubaliana nae kuwa yeye ni kichaa na ni mgonjwa wa akili ndio maana alifanya yale badala ya kuwa sue GPL.

Pengine GPL wangeweza kumsue wema kwa kitendo na vurugu alizo fanya kwenye ofisi zao.
Wema aliitumia hiyo nafasi kutafuta umaarufu kama alivyo zoea ni kujidanganya kufikiri Wema aliumizwa na yaliyo andikwa na GPL.

Wema ni mgonjwa tena sana na hawezi kuajiri Lawyer maana hatoweza kumsikiliza kama hasivyo weza kumsikiliza Kadinda.

Wema haitaji Mwanasheria bali ana hitaji msaada wa kisaikolojia.
 
Last edited by a moderator:

Mkuu Wema hana muda wa kudai fidia maana ana nufaika na hizo habari na zinamfanya maisha yaende.
Wema haihitaji Mwanasheria bali daktari wa Magonjwa ya akili.
 
mkuu mimi nimejiuliza swali moja mpaka sasa nashindwa kupata majibu!

hivi ile ishu kweli ilimuumiza wema kiundani kabisa mpaka moyoni ama ni tricky tu za kusaka umaarufu??

wema inasemekana kwamba ana elimu! sasa kweli elimu yake ndio ile aliyotumia viatu vyake na kujiita kichaa? matusi aliyotoa ofisini pale hakika niilisikitikia nafsi yake..!

wema alifanya lile akiwa na akili yake nzima kabisa mkuu! hakika kama ingekuwa ni skendo yake ya kwanza, tungesema apewe ushauri nasaha, lakini jiulize, kafanya maovu mangapi mpaka akomalie lile moja?
 
Ni ngumu sana Shigongo kumshitaki Wema kwani anawaingizia hela nyingi kwenye magazeti yao

mkuu unajua mi huwa naiona journalism kama kitu cha ajabu sana!

kwanza, kwao kila kitu ni habari!-- wema kafanya fujo kwenye ofisi zao, tayari habari imejileta!

halafu kwa GPL kweli kwenda mahakamani haiwezekani, otherwise wema ndie angefaya hizo procedures! kitu ambacho kama kweli angeshinda, basi umaarufu wake ungetangaziwa wapi? angekufa kisoko..
 
Magazeti ya udaku yataendelea kupata soko kwa wajinga na wavivu wa kufikiri, hivi hamjui hayo ni mambo wamepanga na Wenma kashalipwa pesa yake ili wauze magazeti yao?
 
hivi mkuu, nimejiuliza swali, huyu Wema S ana watu wake ambao anawaamini sana.. kwanini hakuwatumia hao wakafikishe taarifa kwa njia ya barua? hivi kulikuwa na haja ya yeye kwenda kuvua viatu mbele ya HDV camera kweli?..msomi kama wema, elimu yake imemsaidia nini haswa?
 
Magazeti ya udaku yataendelea kupata soko kwa wajinga na wavivu wa kufikiri, hivi hamjui hayo ni mambo wamepanga na Wenma kashalipwa pesa yake ili wauze magazeti yao?
surely, nimefikiri mara mbili hapo!

mkuu, hivi wema S amefikia level ya degree kweli kielimu?
 
Ile ilikuwa ni kutafuta kiki ya kuwashia bajaji tu.
 
mkuu unadhani kwa habari kama ile kama ingepata mtu wa kuisimamia haswa, GPL wangeshinda??

mkuu nimeamini kweli wema ni kichaa, hata siku moja hatopata nafasi ya kuigiza na omotola J.

tatizo la wasanii wengi wenyewe huwa wanapenda kuandkwa na magazeti ya shingongo kwa kupeleka habari Wema mwenyewe alikuwa anapenda kuandkwa sa iv nashangaa kpind wana mwandka kwa kununua nyumba million 400 mbona alikuwa haongei kpind kile mamake kawatukana na kuwatishia mbona alienda kuwaomba mwenyewe msamaha wawe wana mwandka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…