SI KWELI CEO wa Simba kufungiwa miaka mitano 5 au maisha kujihusisha na mpira

SI KWELI CEO wa Simba kufungiwa miaka mitano 5 au maisha kujihusisha na mpira

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
CEO wa Simba sports club Barbara Gonzalez kuna tetesi akafungiwa miaka mitano 5 au maisha kujihusisha na michezo haswa football

Hii imetokea baada ya yanga kupeleka malalamiko TFF kuhusu tuhuma alizozitoa kwa team hiyo inapokea wageni ambao Simba ilikua ikicheza nao champion league na shirikisho

Imeelezwa kua TFF wakiongozwa na karia bado wana hasira na huyo CEO kwakua aliwabania deal la GSM la billion 2 ambapo wanao huyo mwana dada ni kikwazo kikubwa kwao kwenye mipango yao ya kupiga pesa

1657977308243.png
 
Tunachokijua
Barbara Gonzalez ni Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba (CEO), mnamo Mei 20, 2022 ziliibuka tetesi zikidai kwamba kiongozi huyo yupo mbioni kufungiwa kujihusisha na soka kwa miaka mitano na Bodi ya Ligi ya Taifa (TPLB) kufuatia kitendo chake cha kusema kuwa timu ya Yanga inawapokea na kuwapa mbinu wapinzani wanaokuja Tanzania kucheza na Simba. Sehemu ya madai hayo inaeleza:

CEO wa Simba sports club Barbara Gonzalez kuna tetesi akafungiwa miaka mitano 5 au maisha kujihusisha na michezo haswa football
Hii imetokea baada ya yanga kupeleka malalamiko TFF kuhusu tuhuma alizozitoa kwa team hiyo inapokea wageni ambao Simba ilikua ikicheza nao champion league na shirikisho

Je, upi ukweli kuhusu madai hayo?
JamiiForums imepitia ripoti rasmi iliyotolewa na Bodi ya Ligi ya Taifa (TPLB) kuhusu sakata la kiongozi huyo wa Klabu ya Simba. Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi Kuu Tanzania Bara TBLP katika kikao chake cha Desemba 30, 2021 ilipitia mwenendo wa matukio mbalimbali na kufanya maamuzi yafuatayo.

Afisa Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba, Barbara Gonzalez na Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu kila mmoja wametozwa faini ya Tsh. 500,000 kwa makosa tofauti tofauti.

Barbara alifunguliwa kesi ya udhalilishaji na ofisa huyo wa TFF kwa madai ya kumdhalilisha wakati akijaribu kumzuia asiingie kwenye eneo VVIP katika mechi ya Ligi Kuu Bara kati ya Simba na Yanga Desemba 11, 2021.

CEO huyo hakufungikiwa miaka mitano kujihusisha na soka kama wadau na mashabiki wa soka kuwa na sintofahamu ya kiongozi wa Simba kufungiwa miaka mitano kujihusisha na soka bali alitozwa faini ya laki tano kutokana na tukio aliofanya.
Back
Top Bottom