Kuna standards zikiwa set kuna namna post kama hizi hatutaona.
Kwa Tz timu zenye msuli wa kifedha ni 3. Hizi timu 3 zikaset standard kwamba malengo ni international achievement kuna vitu vingi vitabadilika.
Kwanza mikataba haitakua ya sasa ya mwaka mmoja au miwili.
Kocha atachagua nani asainiwe.
Kocha atahukumiwa kwa project nzima na siyo kufungwa kwenye derby.
Timu zitalazimika kuendana na standards za nje, wasemaji wa timu automatically watakua makocha. Wapiga domo watatafuta maisha mengine.
Rekodi kubwa na ndogo zitaanza kutunzwa.
Eventually mashabiki watajua kua mafanikio ya timu siyo kushinda derby.
Ila kwa sasa shabiki anatarajia ceo alie kisa mechi moja. Siyo project kufeli, no, ni mechi moja.