busha
JF-Expert Member
- Jan 21, 2019
- 1,712
- 2,577
Wakuu huyu dada C.E.O wa Simba sports club ni fullbright ni mwanamke wa shoka mwenye kujiamini na uelewa mkubwa sana wa mambo.
Ukifatilia huu mzozo uliopo sasa wa Simba kuvaa nembo za GSM utaona jinsi anavyosimama kwenye hoja na vipengeke vya kisheria kwa utulivu mkubwa bila mihemko, lakini pia yeye Barbara pekee anaonekana kumudu vema kuwajibu lundo la viongozi wa GSM, Yanga na TFF kwenye mgogoro huu pasi na kiongozi mwingine wa Simba kutia neno.
Hakika wanawake wanaweza kusimama kidete hata kama wanashindana na lundo la wanaume.
Hongera nyingi kwake madam C.E.O Barbara Gonzalenz.