Naomba kwamba wale wanaopenda kuharibu nyuzi kwa kuleta mapishano ya TZ vs KE watulie kidogo.
Kuna jambo moja ambalo nimegundua kuhusu baadhi ya wachangiaji wa TZ kwenye JF (Haswa kwa majukwaa mengine kama vile la siasa) Utapata kwamba mara nyingi, hawa ndugu zetu huwa na uwezo wa kuandika na kusoma mambo mengi kutushinda sisi. Sisemi eti anayeandika mambo mengi ana hoja kali, lakini nimekuja kuona kuwa nyuzi zetu nyingi iwe hapa, au Wazua, Nipate, au hata JamiiForums.com huwa ni fupifupi na hazina depth. Ni kana kwamba tumekuwa na attention span ndogo sana na tumezoea jumbe za WhatsApp na chochote kile kirefu sie husema "too long hebu summarize".
Sijui kama ni uvivu wa kusoma au nini. Au ni tatizo la elimu inayotokana na kutumia lugha ya kimombo kama medium of instruction. Ndio, kuna Wakenya ambao huleta mada kama haya, lakini mara nyingi utapata ni zile fupi-fupi tu; au, itakuwa ni article ya gazeti ambayo ameleta kuripoti. Ni nadra sana upate Mkenya ameleta mada ya zaidi ya maneno 500 ambayo ni analysis. Lakini kule jukwa la siasa, utapata mtu amechukua muda wake kuleta mada ndefu ambayo ni analysis tupu, na hata hana haya kuweka jina lake hapo. Naamini hili ni jambo la kujifunza kweli.