Mwanzi1
JF-Expert Member
- Sep 19, 2016
- 6,000
- 4,589
Watanzania hata kwenye kuongea huwa na maneno mengi nafikiri ni hulka yao. Kuna polisi Mkenya alikua anasema akimkamata Mtanzania Itabidi asimpe fursa ya kuongea maana ataongea kama mashini.
Japo pia kuna wale huwa napenda analysis zao kule kwa hayo majukwa mengine, tatizo Watanzania wengi wana uzembe wa kusoma, utakuta mtu ameandika taarifa ndefu yenye analysis muhimu lakini jamaa wanachangia kwa maneno machache yaliyojaa kejeli.
Waandishi wengi walitamaushwa na ni wachache waliosalia wanaoandika vizuri hivyo. Ipo wakat JF ilikua ya great thinkers, siku hizi imevamiwa na madogo wavaa milegezo wasiokua na heshima.
Binadamu wote hawako sawa, mtandao ni tasnia huru ambayo haibaguwi uwezo wa mtu yoyote. Ukisema watu hawasomi na wanachagia maneno yenye kejeli, lakini huo ndio Uhuru wa kimtandao. Hata zamani mtandao kama Facebook au YouTube ilikuwa na watu wanaweka mambo yenye mantiki na weledi wa juu. Lakini kwasababu siku hizi mawasilino yamekuwa rahisi kila mtu anaweza kujiachia anavyotaka mtandaoni. Unaweza kwenda YouTube na ukakuta live stream mtu kaweka paka mbele ya kamera masaa 24.