Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Nimecheka sanaaa baada ya kusikia stori hiiii
=============
ALIYEKUWA Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Matiko Chacha, amesimulia kisa cha mwananchi aliyemtaja kwa jina la Sophia, aliyekuwa akimtumia ujumbe mfupi wa maneno kupitia simu - akimtongoza, licha ya kuonywa mara kadhaa lakini hakuacha.
Chacha amesema mwanadada huyo aliendelea kumtumia ujumbe huo, hali iliyomlazimu kuchukua hatua kwa kulifikisha suala hilo kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora (RPC), hatua ambayo amesema ilimfanya Sophia kuacha kabisa kumtumia ujumbe.
Amesema kabla ya kufikia hatua ya kutoa taarifa kwa RPC, alitumia njia mbalimbali za kumfikia mwanadada huyo kupitia wajumbe waliokwenda kumuonya na kumtaka kuacha kumtumia ujumbe wa aina hiyo, lakini juhudi hizo hazikuzaa matunda.