Benoit
JF-Expert Member
- Jun 1, 2026
- 754
- 1,696
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Matiko Chacha, amesimulia kisa cha mwananchi aliyemtaja kwa jina la Sophia, ambaye alifikishwa Polisi baada ya kumtumia ujumbe wa simu wenye maneno ya kumtongoza.
Kwa mujibu wa Chacha, mwanamke huyo aliendelea kutumia ujumbe huo licha ya kuonywa mara kadhaa, hali iliyomfanya suala hilo kufikishwa kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora (RPC).
Chacha amesema hata baada ya kufikishwa kwa RPC, mwanamke huyo hakukata tamaa, na alijaribu tena kufikisha ujumbe kwa njia mbalimbali kupitia watu waliokuwa wakimuona na kumtaka aache kutumia ujumbe wa aina hiyo.
Lakini swali linabaki, Kumtongoza kiongozi kwa ujumbe wa simu ni kosa la jinai, au ni suala ambalo linapaswa kuishia kwenye kukataliwa tu? 🤔
Chanzo : chanzania yetu