Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
Nimekuwa nikishangaa mnoo mara kwa mara kusikia mijadala ya kujadili namna ya kuwarejesha au kuwakataa wabunge wa Covid 19, Mchungaji Msigwa na Dr. Slaa. Hizi hoja zilishika kasi kipindi cha uchaguzi wa mwenyekiti ndani Chadema na zinaendelezwa hadi sasa huku upande wa wapambe wa Mbowe ukipiga chapeo zaidi kwa Covid 19 warejeshwe na upande wa wapambe wa Lissu ukitaka Mchungaji Msigwa na Dr. Slaa warejeshwe. Kimantiki ni ujinga mkubwa kwa Chadema kuwajadili hao watu sasa, ni kupoteza muda. Sababu chache za kimsingi ni hizi.
1. Hao wote ni kundi lililoamua kuunga mkono CCM wakati wa mapambano, na huko wakalipwa na kupewa fursa kede kede huku likipambana kuididimiza Chadema. Hawa ni wasaliti.
2. Hakuna hata mmoja ya hao aliyekiri kuwa alikosea kuunga mkono CCM katikati ya mapambano ili sasa Chadema imeone ni mtu huru. Bado ni wasaliti.
3. Wote hao wamepoteza umaarufu wa kisiasa na sio mtaji wa kutumainiwa na watanzania tena. Wanaitaka Chadema ili iwabebe, wanasaka fursa.
4. Chadema kwa sasa ina watu wengi na bora zaidi wa kufanya siasa kuliko hao wote. Kutaka kuwakumbatia tena hao ni kuirudisha nyuma mnoo chadema na hapo hapo ni kuwakatisha tamaa wapambanaji wa dhati wa Chadema wa muda wote.
5. Utaratibu wa kujiunga na Chadema uko wazi kikatiba kwa watu wote na wala hauhitaji mjadala wa kubebana au kuchukiana. Kama hao wote wanadhani wana haki ya kurudi Chadema wafate taratibu na taratibu zitajibu zenyewe. Huu mchezo wa kutaka kurudi nyuma kupitia nyuma ya mlango umejaa uovu, ujanja ujanja na hila.