Uchaguzi 2020 CHADEMA, ACT Wazalendo vyapigwa marufuku kunadi wagombea wasio wa vyama vyao. Waambiwa kufanya hivyo ni kuwachanganya Wananchi

dikteta2020

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2018
Posts
595
Reaction score
3,991
Wakuu mkistaajabu ya tume ya uchaguzi basi jiandae kuona ya msajili.

Jana kumbe Sisty kuwahi kote huko na boda boda pale makao makuu ya Chadema ni kupeleka barua ya katazo kuwa kuwanadi wagombea wa nje ya vyama vyao ni kukiuka maadili ya uchaguzi hivyo wamepigwa marufuku.

Yani hii ofisi ya msajili imekuja na kituko cha aina yake!




===
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Sisty Nyahoza ahudhuria kipindi cha Clouds360 kinachoendeshwa na Clouds Media na kuongea masuala mbalimbali wakati huu nchi ikiwa inaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu.

Aidha, katika mahojiano hayo, Sisty aliulizwa kuhusu masuala mbalimbali ikiwamo suala zima la Vyama vya Siasa kuungana na kushirikiana katika uchaguzi.

Akitoa ufafanuzi wa kina kuhusu suala hili Mh. Sisty Nyahoza alisema “Vyama pekee vimewahi kuungana ni ASP na TANU viliungana ikawa CCM. Kilichofanyika 2015 kwa jina la UKAWA ule ni ushirikiano kwamba wote mnabakia mna status ya kisheria kama chama cha siasa halafu mnashirikiana kwenye shughuli za kisiasa”

Ameongeza kuwa "Kisiasa kuna ushirikiano wa aina mbili, wa kwanza ni Coalition mnashirikiana kwa malengo ya kushinda uchaguzi. Halafu kuna Alliance mnashirikiana katika mambo yanayojitokeza tu katika siasa halafu kila mmoja anaendelea na shughuli zake, Coalition imewekewa masharti”

“Ni vyema haya mambo ya ushirikiano vile vyama vinataka kushirikiana viingie mkataba wakubaliane sera zetu zitakuwa zipi, tutawekaje wagombea, tutaundaje Serikali, tutagawanaje vipi ruzuku. Baada ya hayo makubaliano wayalete kwa msajili wa vyama vya siasa”

“Waliokuwa wameshasema wanaunga mkono wa chama kingine wanachopaswa wanatakiwa wabakie kama walivyobakia baada ya uteuzi wa Wagombea, baada ya uteuzi wa wagombea Urais Agosti 25 hawawezi kuteua tena mgombea Urais”

Aidha akiweka bayana kuhusu ushirikiano unaofanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo na ACT Wazalendo Sisty Nyahoza amesema “Wao (CHADEMA, ACT) hawapaswi kwenda hadharani na kumsapoti mgombea yule kwa sababu ukiwa unamnadi mgombea wa chama kingine na wewe una chama na sera zako, wananchi hawajui baada ya uchaguzi mtaunda Serikali moja au utatekeleza ya kwako. Mnawachanganya wananchi”-
 
Sasa huoni mantiki ya katazo hilo kweli?
 

Hiyo ni hofu ya ccm kushindwa.
Kama kweli wanataka kushinda, basi wawaache hao wagombea wawachanganye watu.
Huwwezi kumfundisha mpinzania/adui wako mbinu za kukushinda.
 
Mbona Mrema na Magufuli wako serikali moja?
Hao walishafuata sheria inavyosema! Unajua Chadema wanafeli sehemu nyingi sana. Kwa mfano mwaka jana wakati wa kuboresha daftari la wapigakura CCM ilikuwq inahamasisha wanachama wao kwenda kuboresha na kujiandikisha wakati Chadema walikuwa wanawakataza wanachama wao wasishiriki wakitegemea kuwa kutakuwa na Katiba mpya na kwamba hawatashiriki uchaguzi bila Katiba mpya.

Sasa uchaguzi umekuja tena hawakumbuki Katiba mpya. Wakishindwa watalalamika kuwa wameibiwa wakati hawakuwaandaa wanachama na washabiki wao!! Chadema ni shidaaa!!
 
Omindiii....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…