Keynez
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 3,809
- 6,948
Inawezekana wengi wanaona kiza kinene mbele ila wengine tunaona dalili za mwanga mbeleni.
Ningeshauri kwa sasa CHADEMA wafanye mambo makuu matatu.
1. Kutengeneza timu ndogo ya wanadiplomasia watakayezunguka dunia nzima kujenga mazingira ya uungwaji mkono kuanzia sasa kabla na baada ya kutwaa madaraka. Inawezekana ikawa ngumu kukutana na maafisa wa serikali wa nchi husika, ila kujenga mahusiano ya karibu na vyama vya siasa, taasisi zisizo za kiraia, nk. ni jambo litakalokuwa na faida kubwa huko mbeleni. Katika mikutano ya SADC, AU, UN, DAVOS, etc. inabidi CHADEMA wawe na uwakilishi hata kwenye "sidelines" kujenga network na kubadilishana mawazo na kutafuta uungwaji mkono.
2. Kuanza kuwatambua Watanzania waliopo ndani na nje ya nchi walio ndani na nje ya mfumo wa Serikali ambao wanaweza kuwa msaada mkubwa pale CHADEMA itakaposhika madaraka. Tukumbuke kuna kazi kubwa iliyo mbele ya kufumua mifumo mingi ya Tanzania. Itahitajika kuanza kazi kwa kasi huku njia na malengo yakijulikana. Bila kufanya hivyo, mtajikuta mnategemea na mnaokoteza wahuni wa CCM walioharibiwa na mifumo ya rushwa, ubadhilifu na ukiritimba na ambao watawapotezea muda na nyie muonekane hamfai na msipokuwa makini wananchi watawakataa nyie pia.
3. Kutengeneza roadmap ya jinsi misingi na ngome zote za utawala wa CCM zilizojipenyeza katika taasisi mbalimbali zitakavyovunjwa haraka iwezekanavyo ili zisije zikatumika kuvuruga na kukwamisha kwa makusudi harakati za maendeleo za serikali ya CHADEMA.