CHADEMA anzeni na kauli hizi za viongozi kuhusu ajira kwa vijana, tunataka Serikali iwajibike

CHADEMA anzeni na kauli hizi za viongozi kuhusu ajira kwa vijana, tunataka Serikali iwajibike

The Sunk Cost Fallacy 2

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2022
Posts
9,434
Reaction score
10,970
Hello Tanzania!

Hapa Tanzania kumekuwa na Kauli mbalimbali za ahadi na kuudhi wanazotoa viongozi kuhusu Ajira Kwa Vijana.

Kwa bahati mbaya hatuna Mechanism ya evaluation ya Kauli zao Ili kujua uwajibikaji na matokeo ya kile wanachahidi.

Watu wanakimbilia vitu cheap hasa vya kujenga Jenga ambavyo havihitaji akili kubwa then wanakuja walisema ndio maendelea.

Kwa nyie Wapinzani ni muda muafaka Sasa kuwataka Viongozi wa Serikali waje na takwimu rasmi zinazoonesha structure nzima ya Ajira Kwa watu na ukosefu wa Ajira Kwa Vijana.

Namba zikijulikana itakuwa rahisi Sasa kufanya evaluation ya Kauli za viongozi Ili walete majibu ya jinsi wamepunguza tatizo la Ajira Kwa Vijana.

Nchi za wenzetu watu wasio na Ajira wanasajiliwa na hata wakipata Ajira takwimu zinajulikana ila hapa Tanzania ni upuuzi upuuzi usioeleweka,hakuna anayefahamu Kwa hakika watu wangapi wakiwemo Vijana hawana Ajira.

Matokeo yake Kila mtu akisimama jukwaani anatoa ahadi yake ila hiyo ahadi haijulikani from which base.Tunaambiwa Vijana mil.1 wanaoingia kwenye soko la Ajira Kila mwaka ila haijulikani wanafanya nini,wangapi wameajiriwa nk kiasi kwamba hata sera zinatungwa Kwa kubahatisha na pia hata kukadiria Kodi inashindikana Kwa sababu za mambo ya kiholela.

Nyie Chadema hapa ndio pa kuanzia Sasa Ili kuiwajibisha serikali,haiwezekani tuna ofisi ya Labor karibu Kila Wilaya lakini Hawa watu hawana takwimu zozote kwenye maeneo Yao licha ya kulipwa mshahara..

Mwisho natambua Kuna juhudi zinafanyika za kukabiliana na tatizo la Ajira ila ni za Zima moto,haziko consistent na hazina uhakika Kwa sababu hawana takwimu halisi za wasio na Ajira,so ni sawa na kutupa jiwe gizani ukitegemea kumkabili mwizi.

Tunataka uwajibikaji kwenye Kauli zifuatazo za viongozi.
👇

Ajira.jpg

Milioni 24.jpg
 
Sioni sababu kwanini usianzishe wewe hayo mapambano kisha Chadema wafuate..

Usipende kuwa chawa wa mama maisha yako yote, wacha akili yako ifanye kazi, mama yako akifanya vizuri mpongeze, akikosea mkosoe..

Hujui kwa kuwapa Chadema hiyo kazi, unaendelea kuwa goigoi wa kusifia tu, amka ndugu, kuambizana ukweli sio dhambi.
 
Hari ni mbaya sana, ata wanaoenda kwenye usairi Utumishi vijana wamekata tamaa. Hakuna ajira, hakuna kazi, hakuna vibarua, hakuna ata kujitolea, pia hakuna ata mbinu za wapi tunatoa mtaji wa kujiajiri. Basi naomba Serikali watulipe ata allowance ya kukosa kazi ili tusichanganyikiwe. Maana!.
 
Acha upumbavu Mimi sio mwanasiasa na sio chawa,na Wala Sina sababu ya kufanya hivyo maana nina Ajira na nimeajiri so nawasaidia Watoto wenu.
Upumbavu ni kuliona tatizo na kuwaambia wengine waanze kulifanyia kazi, ikiwa nawe una uwezo wa kufanya hivyo... , na wala hakuna aliyekwambia hana ajira, wewe ni chawa wa mama acha makasiriko, au huna hela ya chai na hiyo ajira yako?
 
Upumbavu ni kuliona tatizo na kuwaambia wengine waanze kulifanyia kazi, ikiwa nawe una uwezo wa kufanya hivyo... , na wala hakuna aliyekwambia hana ajira, wewe ni chawa wa mama acha makasiriko, au hujanywa chai na hiyo ajira yako?
Wewe ndio moumbavu ndio maana Mimi nimeanza Kwa kuwasaidia japo hoja,Sasa nyie kama chama kazi yenu ni ipi kama vitu vya msingi hamuwezi kujadili?

Ndio maana Huwa nawaelewa ACT Wazalendo,Huwa wanakuja na data,wanakosoa na kutoa way forward sio majinga kama nyie machadomo mnadakia dakia vitu kiumbea umbea tuu.
 
Back
Top Bottom