Leonel Ateba Mbinda
JF-Expert Member
- Feb 20, 2023
- 644
- 2,695
Bendera ya Chadema ina rangi nyekundu, kila mtu anajua maana ya nyekundu ni nini, lakini pia ukisoma Katiba ya Chadema unaona kabisa kuwa kwa namna ilivyoandikwa inaashiria kuwa wao ni watu wa vita tu, nchi hii imepata uhuru wake kwa amani kabisa bila kumwaga damu, nyie mna bendera yenye rangi nyekundu, kwa maoni yangu itakuwa ngumu sana kupewa uongozi wa nchi kwa kutumia rangi nyekundu.
La pili kazi kubwa imefanywa katika kuijenga nchi hii, watu wamekufa katika kuitetea nchi hii, nyie mnasema mnatafuta uhuru hapa nchini, mbona naona kama sera na mipango yenu ni ya mashaka sana, badilisheni mipango yenu, hamuwezi kutaka uongozi wa nchi huku mnatukana viongozi, mnatishia kumwaga damu, mnashirikiana na mabeberu kutaka kuisaliti nchi, akina Lissu wameacha familia zao kwao huko Sweden huku wanazuga tu.
Mwisho, waonyeni vijana wenu akina Mdude, Boni Yai, Mwaipaya, Sativa, Martin na akina MAria Sarungi kuwa kwa harakati zenu mnazoendelea nazo huku mkitegemea jumuiya za kimataifa ziwasaidie hamtofanikiwa, mtaumiza vijana wengi nchi hii, kwa sababu hamtafanikiwa kwa lolote, kama uchaguzi wa mitaa umekuwa hivi itakuwaje huo uchaguzi wa mwakani, kesho mnasema mnakaa wakati leo mko na kikao cha Baraza Kuu Dodoma, wenzenu wanajua kila mnachopanga, kesho mnakutana hata mkipanga kupeleka vijana wa kujibu mashambulizi mtapoteza maisha ya vijana hawa, kaeni pamoja na serikali mjadiliane namna ya kufanya siasa za kistaarabu, siasa za akina Lema kumtishia kifo Rais aliye madarakani ni mambo ya kijinga sana haya.