Tetesi: CHADEMA chini ya Uongozi wa Lissu washindwa kuchangisha 180 million kwaajili ya uzinduzi wa mikutano nchi nzima

Ngongo

Platinum Member
Joined
Sep 20, 2008
Posts
20,654
Reaction score
35,887
Heshima wanajamvi.

Baada Lissu kuchaguliwa Mwenyekiti Taifa na kuunda kamati kuu yake,waliweka maazimio ya kuchangisha 180,000,000 kwaajili ya kufanya mikutano Mikoa yote ya Tanganyika.

Taarifa za uhakika mpaka leo wamekusanya kiasi cha Tshs. 1,920,000 ambazo zitaweza kufanya mkutano wa Buguruni pekee yake.

Ni wazi Lissu na team yake wameanza vibaya hawajui nini cha kufanya na kibaya zaidi bila upatanisho wa uhakika Lissu kufikia mwezi July atakuwa kachoka vibaya.

Kikao cha Kamati Wajumbe walijikuta wanakula mandazi huku wakitakiwa kujilipia.

Ngongo kwasasa Ababati.
 
kama chadema ikikosa jimbo hata moja 2025
manake wawotopata ruzuku hapa ndipo mwanzo wa kifo cha chadema
 
bilashaka yoyote,
mtaalamu wa kuomba omba kuchangiwa atakua anajipanga kuja hadharani kimkakati kuomba kuchangiwa chochote kitu kama kawaida yake 🐒
 
Weka ushahidi wa picha au sauti
 
Sio ajabu kukwama kwa Lissu kupata pesa. Mbowe alifanya chama mali yake na alipewa ufadhili wa moja kwa moja kutoka serikalini ili kuigiza upinzani, mbali ya ruzuku.

Kutoka kwa Mbowe chamani kunamaanisha kuondoka kwa support ya serikali kifedha CHADEMA.
 
Uzi bila ushahidi ni chai.
 


Uongo uongo mbona hawaja omba michango! Kwani kulikuwa na shida gani kuomba michango kama ni ulweli
 
Alichangisha za matibabu, hata kusema Asante alishindwa, akaishia kupost picha akila nyama choma.

Juzi kachangiwa za gari, hata appreciation Hana.

Nani akachange 180M za kwenda kwenye mipasho.
 
Hata kama ni kweli, huo ndio uhalisia boss. Una lingine kwa msaada zaidi? Mwambie Mbowe ahamie chama kingine akapeleke hela zake huko. Kwa sasa chama kiko kwenye mikono salama, asali haina nafasi ndani ya cdm ya kweli.
 
Baada ya Mbowe kushindwa uchaguzi kazi yako mpya ni kuupiga vita uongozi mpya wa Chadema na kufurahia kuona ukishindwa/ukikwama.

Tindo
 
Alichangisha za matibabu, hata kusema Asante alishindwa, akaishia kupost picha akila nyama choma.

Juzi kachangiwa za gari, hata appreciation Hana.

Nani akachange 180M za kwenda kwenye mipasho.
Hakuna anayetaka hela yako ww unayetaka kupewa asante huko nyumbani kwako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…