Wenye chuki na taifa hili ni wale wanaonunua magari ya kifahari mil. 200 kwa kodi za wananchi halafu wanajiuzia mil. 5.
Wenye chuki na taifa letu ni wale wanaojaza magari mabovu kila ofisi za umma kisha wanajiandikia pesa za mafuta,tairi,spea na kuzitafuna kupitia magari juu ya mawe.
Wenye chuki na taifa letu ni wale wanaoajiri watu kwenye wizara ya ardhi lakini hawapimi viwanja kwa watanzania kwenye ardhi aliyoiumba Mungu matokeo yake wanasubiri watu wajenge juu ya mawe na mabondeni kisha wanadai kodi ya majengo wakati hawakufanya jambo lolote kuwawezesha hata kupima viwanja kwa kamba .
Wenye chuki na nchi yetu ni wale waliozoea kudhulumu kura za wananchi kwa kutumia bunduki na sasa wanadhulumu madini ya watu badala ya kuyapeleka panapohusika ili yalipiwe kodi.
Wenye chuki na nchi yetu ni wale wanaoshindwa kuwalipa maaskari mishahara inayokidhi mahitaji ya mwezi matokeo yake wanawaacha wakitafutie kijambazi ili nao waishi kama binadam.
Wenye chuki na nchi yetu ni wale Makada wa CCM kama akina Hamza wanaowaua askari wetu bila huruma na kuchukua silaha ili zimilikiwe na wajumbe. Kweli wajumbe sio watu wazuri.
Wenye chuki na nchi yetu ni wale wanaoshindwa kujenga masoko maeneo rasmi kwa sababu wameshindwa kupima miji na kuacha maeneo ya biashara na masoko . Uzembe wao umeligharimu taifa kila sehemu ni wachuuzi.
Wenye chuki na nchi yetu ni wale wanatunga sheri mbovu ya kuwawekea kinga ya kutoshitakiwa binadamu na makada wa CCM ili wavunje sheria kulinda maslahi yao kuipitia bunge ,mahakama, msajili wa vyama,serikali ili tu wakandamize wapinzania wao badala ya kusimamia haki. Kinga kwa ajili ya dhuluma ni chuki kwa Taifa.
Wenye chuki na Taifa letu ni wale wanaobambika watu kesi na kujenga chuki na visasi bila sababu.
Wenye chuki na nchi yetu ni wale wanaotoa madaraka kwa upendeleo na kwa watu wasio na uwezo na ubunifu.
Wenye chuki na nchi yetu ni wale walioficha ugonjwa wa Rais wetu wa awamu ya tano mpaka akafariki bila kutuambia ili tumuombee kwa Mungu. Wakaacha mpaka kifo chake wakaendelea kudanganya.
Wenye chuki na nchi yetu ni wale waliotumia mabilioni ya pesa kuleta katiba ya wananchi lakini wakaona kuwa katiba ya wananchi itawafanya wawe watumishi wa umma sio mabwana wakubwa na waheshimuwa na watapaswa kuwa waadilifu na kuweka wazi mali zao matokeo yake wakaamua kumuua Dr. Mvungi na kuwatisha wengine na kuwapiga huku wengine wakitolewa majalalani ili waikane katiba ya wananchi.
Wenye chuki na Taifa hili ni wale wanaotumia 75% ya pato la nchi kwenye utawala na mambo ya starehe badala ya kuinua maisha ya wananchi na mifumo ya Elimu na afya.
Wenye chuki na nchi yetu ni wale wanaoshindana kufanya vikao na semina ili wajilipe baada ya JPM kutangulia mbele za haki, wanaponda fedha za umma huku wakimponda mwananchi kwa tozo za simu.
Mwenye chuki kubwa kabisa na taifa hili ni mleta mada hii .