Mkuu heshima mbele. Tatizo lililopo siyo la nani kumjua na nani bali baadhi ya wanakamati ndio waliohusika na madudu yaliyofanywa kuhusiana na mikataba ya madini. Pia miaka ya nyuma wameshawahi kuwemo kwenye kamati za madini ambazo ripoti zake hazijatangazwa kwa Watanzania. Hivi kweli hakuna Watanzania wengine wenye sifa za kuwemo katika kamati hiyo!? Hao waliohusika na kuandika mikataba feki kwa nini tena wawemo kwenye kamati hiyo!? Sidhani kama Lissu anaweza kutoa data kama hizi bila kuwa na ushahidi wa uhakika wa kile anachozungumza. soma hapa chini.
Mwanasheria Tundu Lissu, ambaye aliposimama kuzungumza alishangiliwa na mamia ya washiriki wa kongamano hilo, alisema haungi mkono kuwepo kwa kamati hiyo na haikupaswa kuwepo, huku akiwachambua wajumbe wake, mmoja baada ya mwingine.
Tuna historia ya ku-miss use hizi kamati, inapaswa tujiulize hii kamati ya Zitto ni ya nini wakati kuna kamati nyingine tano zinazohusu masuala ya madini zilishaundwa na zimewasilisha ripoti zao, lakini hazijawekwa wazi mpaka leo na hatujui nini ripoti hizo zimependekeza? alisema.
Lissu aliitaja kamati ya kwanza kuwa iliundwa mwaka 2001 chini ya uenyekiti wa Jenerali Mboma, ambayo ilikamilisha kazi yake, lakini mpaka leo ripoti yake haijawekwa hadharani.
Alisema mwaka 2002 kamati nyingine iliundwa na mwenyekiti wake alikuwa Brigedia Mangenya, ambayo ilitoa ripoti yake kimya kimya mwaka 2003 na haijulikani nayo ilipendekeza kitu gani.
Kamati ya tatu iliyoundwa ni ile iliyoongozwa na aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini mwaka 1994-1995, Dk. Jonas Kipokola. Mmoja wa wajumbe wake kwa sasa anaonekana tena kwenye Kamati ya Zitto
Maria Kejo alikuwepo kwenye kamati hii
ripoti haijatolewa, alisema Lisu huku akionekana kusikitika.
Lissu, katika madai yake alimuelezea Kejo kuwa ndiye aliyehusika kusaini mkataba mbovu wa IPTL, hivyo kuteuliwa kwake katika kamati hiyo, kunaonyesha jinsi Rais Kikwete alivyofanya uteuzi wenye shaka.
Maria Kejo, miaka ya 1994/95 alijibadilisha jina akijiita Maria Ndosi, miaka ya hivi karibuni ameanza tena kujiita Maria Kejo, huyu ndiye aliyehusika kusaini mkataba wa IPTL, hii ipo kwenye ripoti ya Transparence International ya IPTL, na kwamba zipo kumbukumbu zinazoonyesha kuwa alihusika kuwashawishi baadhi ya viongozi kuchukua rushwa ili mkataba huo usainiwe.
Mjumbe mwingine aliyetajwa na Lissu kuwa hafai kuwa kamati hiyo, ni Mwenyekiti wa Chama cha United Democratic (UDP), John Momose Cheyo, kwa vile alikuwa mpiga debe mkubwa wa kusainiwa kwa IPTL.
Akizungumza kuhusu ushiriki wa Zitto katika kamati hiyo, alisema bila kuingia kiundani kuwa, uteuzi wake hauna maana kwa sababu hana cha kufanya katika kamati hiyo iliyojaa tuhuma nzito za rushwa.
Lissu pia alimgusa Machunde akidai kuwa ni hatari kuwa katika kamati hiyo kwa vile kuna ushahidi wa kualikwa kwake bungeni na Karamagi kwa ajili ya kushawishi baadhi wa wabunge wasilivalie njuga suala la Richmond.
Mwingine aliyetajwa katika orodha hiyo ya kutofaa kuwa katika kamati hiyo ni Salome Makange, Mwanasheria wa Wizara ya Nishati na Madini anayedaiwa na Lissu kuwa si muadilifu na kwamba ni mmoja wa watu waliohusika kusaini mkataba wa Buzwagi.
Mkataba wa Buzwagi au wowote ule ni lazima usainiwe na mwanasheria wa wizara, leo wapo kwenye kamati
Mark Bomani (Jaji) ambaye ni Mweyekiti wa Kamati hiyo, historia inaonyesha kuwa ni mwana CCM na Harrison Mwakyembe hajawahi kusema chochote kuhusu madini. Tume inakwenda kufanya nini, haina term of reference? alihoji Lissu.
Alisema mbali na wajumbe wa kamati hiyo kutokuwa na sifa, hata muundo wa kamati yenyewe hauna nguvu za kutosha za kufanya kazi kwa uhuru na uwazi.
Alisema kama Rais Kikwete ana nia ya dhati ya kuunda kamati ya kupitia mikataba ya madini, anapaswa kuunda kamati teule ya Bunge ambayo ina mamlaka na nguvu kisheria za kumuita mtu yeyote na kumhoji.
Kamati ya Bunge ina nguvu, kwenye kamati hii unaweza kumuita Karamagi na ukamwambia lete mikataba, akikataa unamfunga, Kamati ya Rais haina judicial power, mimi naona rais anajitakasa tu kwa wananchi, alisema Lissu.