CHADEMA flip flopping at its best! Jisomee mwenyewe uone

CHADEMA flip flopping at its best! Jisomee mwenyewe uone

TAARIFA KWA UMMA

Maoni yangu Binafsi kuhusu Kamati ya Madini
iliyoteuliwa na Rais Kikwete

• Napinga Muundo, Mfumo na Mamlaka ya Kamati; nahoji
dhamira ya Rais Kikwete
• Sijawahi kupinga, sipingi na sitapinga Zitto Kabwe
kuteuliwa kwenye Kamati
• Zitto aingie kwenye Kamati kuendelea kuhoji na
kutuwakilisha
• Kupinga Kamati si maslahi binafsi, ni maslahi ya
Taifa- kupinga kwa nia ya kitaifa ni uzalendo.
• Gazeti la Mtanzania na Rai nipeni haki ya
kunisikiliza; chukueni maoni yangu toka kwangu
mwenyewe kuondoa kupotosha na kunichafulia jina.


Toka Rais Kikwete aunde Kamati ya Madini Novemba 13 na
kumteua Zitto Kabwe kama mmoja wa wajumbe, sijawahi
kujitokeza hadharani kutoa maoni yangu kuhusu suala
hilo hata nilipotakiwa kufanya hivyo na vyombo kadhaa
vya habari. Nilikwepa kutoa maoni yangu kutokana na
sababu mbili: Mosi, tayari nilishatoa maoni yangu
kuhusu kamati hii ya Rais toka Novemba 4 mara baada ya
Kauli ya Rais katika mkutano mkuu wa CCM. Pili; Mara
baada ya Novemba 14 Viongozi mbalimbali wa CHADEMA
walikuwa wametoa maoni yao kuhusu suala hili na kwa
kiasi wengine maoni yalitofautiana na baadhi ya vyombo
vya habari vikatafsiri kuwa ni mgogoro- hivyo sikutaka
kuongeza jina langu katika orodha ya watoa maoni
kuepusha kuendeleza hisia za kwamba
tunamgogoro-nilinyamaza kimya na kuyawasilisha maoni
yangu katika vikao vya chama chetu. Hata Novemba 17
ambapo Kurugenzi ya Vijana tuliandaa Kongamano la
Wasomi ambapo suala la Kamati hii pia lilijadiliwa,
sikutoa maoni yangu yoyote kuhusu hii kamati kwa
sababu ambazo nimezieleza.

Hata hivyo, nalazimika kwa shingo upande kuyatoa maoni
yangu kwa umma. Sababu mbili zimenisukuma nitoe kauli
yangu leo. Mosi, habari za gazeti la Mtanzania ambalo
katika matoleo kadhaa ya wiki hii limekuwa likinitaja
na mara moja ukurasa wa mbele kwamba napinga Zitto
Kabwe kuwepo kwenye Kamati(gazeti limewasilisha kwa
niaba yangu kitu ambacho sijakisema) na Gazeti la Rai
toleo la Jana(22/11/2007) ambalo si tu limerudia maoni
ya gazeti lake dada kwa niaba yangu- bali pia
limenihukumu natunguliza mbele maslahi yangu binafsi
badala ya maslahi ya Taifa. Katika hali hii ya
kutolewa maoni kwa wiki nzima, nikinyamaza wasomaji na
watanzania wenzangu wanaweza kudhani kwamba hayo ndiyo
maoni yangu. Nimeamua nitoe taarifa hii kutoa wazi
maoni yangu. Pili; kikao cha Kamati kuu ya CHADEMA
kinakaa kesho Jumamosi 24/11/2007- kwa vyovyote vile,
katika kikao hicho chama kitatoka na msimamo mmoja wa
chama baada ya kupokea maoni mbalimbali, hivyo baada
ya kikao hicho mimi kama kiongozi zitaweza tena kuwa
na fursa ya kuwasilisha maoni yangu binafsi kuhusu
suala hili. Nitawasilisha msimamo wa chama kama sehemu
ya uwajibikaji wa pamoja hivyo sitapata wasaa tena wa
kukanusha na kutoa maoni yangu binafsi tofauti na yale
yaliyoandikwa na magazeti ya Mtanzania na Rai. Napaswa
kusema sasa, ama ninyamaze milele.


Novemba 4, 2007 nilitoa msimamo wangu pale tu Rais
alipotangaza kuunda kamati hii- kwa ujumla katika
msimamo huo nilihoji dhamira ya Rais kuunda kamati
mpya wakati ya Masha aliyoiunda pindi alipoingia
madarakani na ikatangazwa kuwa imempatia ripoti yake
Septemba 2006 hatujaelezwa ilibaini nini na imeshindwa
kubaini nini ili iwe sababu ya kuundwa kwa kamati
nyingine. Pia nilisema wazi kwamba wapinzani hawapaswi
kunyamaza kwa kuwa tu watahusishwa kwenye kamati,
wapinzani wanapaswa kuendelea kutetea maslahi ya taifa
popote walipo na umma wa watanzania unapaswa kuendelea
na mjadala kuhusu madini na rasilimali zingine za
taifa. Na kwa ujumla nilieleza kwamba katika mazingira
hayo suala sio kuundwa kwa kamati, suala ni kutekeleza
matokeo ya kamati, na suala hili linahitaji kitu
kimoja tu- Dhamira ya kisiasa ya kuchukua hatua. Huu
ni msimamo wangu ambao sikuhitaji tena kuutolea maoni
baada ya Rais kuunda kamati mpya Novemba 13, 2007.

Mara baada ya Rais kuunda Kamati ya Madini na kumteua
Zitto Kabwe Novemba 13, (narudia tena)- sijawahi kutoa
msimamo wangu kwa chombo chochote cha habari.Kwa
waraka huu; nawasilisha rasmi maoni yangu kwa umma
kuhusu Rais kuunda Kamati ya madini:

Napinga Muundo, Mfumo na Mamlaka ya Kamati na nahoji
dhamira ya Rais Kikwete katika kuunda kamati yenye
muundo, mfumo na mamlaka kama kamati hii chini ya
Mwenyekiti Jaji Msaafu Mark Bomani. Baadhi ya masuala
ya kujiuliza yaliyopelekea niwe na maoni haya
nimeyadokeza kwenye ujumbe wangu niliowapatia baadhi
ya wahariri Novemba 19 mwaka 2007. Sijawahi kupinga,
sipingi na sitapinga Zitto Kabwe kuteuliwa kwenye
Kamati. Zitto aingie kwenye Kamati kuendelea kuhoji na
kutuwakilisha. Kupinga Kamati si maslahi binafsi, ni
maslahi ya Taifa- kupinga kwa nia ya kitaifa ni
uzalendo. Gazeti la Mtanzania na Rai nipeni haki ya
kunisikiliza; chukueni maoni yangu toka kwangu kuondoa
kupotosha na kunichafulia jina.

Kwa maoni yangu: Muundo wa Kamati unazua mjadala- Rais
aliahidi kwenye mkutano Mkuu wa CCM kwamba angeunda
kamati itakayoshirikisha jamii kwa upana zaidi ikiwemo
asasi za kiraia-lakini kamati iliyoundwa imejaa
watendaji wa serikali na makada wa chama tawala huku
asasi za kiraia zikiwa hazina mwakilishi hata mmoja
tofauti na ahadi ya Rais. Katika hotuba yake Rais
alizungumzia uwakilishi-lakini katika uteuzi wake Rais
amefanya uteuzi wa watu binafsi ingawa wanatoka katika
taasisi mbalimbali ikiwemo vyama vya upinzani. Katika
Lakini hili ni suala dogo. Kubwa zaidi katika muundo
wenyewe ni Rais kuwahusisha baadhi ya wajumbe wenye
tuhuma za ufisadi ambazo Rais alikuwa anazifahamu
kabisa toka wakati akiwa Waziri katika serikali na
wengine wanamgongano wa kimaslahi ambao uko bayana.
Kama aliwahujua watu hawa, nini dhamira ya kuwateua?
Je, hakuna watanzania wengine ikiwemo toka katika
chama chao ambao uadilifu wao hautiliwi mashaka ya
kiasi hicho?

Mfumo wa Kamati unazua mjadala-Hadidu rejea za kamati
zimetogezwa lakini katika hadidu rejea zilizotajwa
masuala ya haki za binadamu katika maeneo ya migodi na
ya uchafuzi wa mazingira hayajaguswa. Nini cha pekee
ambacho kamati hii itafanya ambacho Kamati ya Masha
iliyokamilisha kazi yake mwaka jana haijafanya? Imani
yangu ni kuwa suala hili litatazwa vyema- ripoti ya
Kamati ya Masha itawekwa wazi kwa umma, Kamati ya
Bomani itafanya kazi yake kwa uwazi na kuwa na vikao
vya masikilizano na umma(public hearings) na ripoti
yote itawekwa wazi kwa umma.

Mamlaka ya Kamati yanaibua mjadala- Uamuzi wa Rais
Kikwete kuunda Kamati badala ya Tume unanifanya nihoji
dhamira yake. Rais Kikwete anafahamu kabisa kuwa
Kamati haina mamlaka ya kutosha ya kuita mashahidi na
kuwataka kutoa ushahidi wa kiapo kama ambavyo Tume ya
Rais inavyo. Uamuzi wa kuunda Kamati unafanya dhamira
ihojiwe, je masuala ya madini ikiwemo sheria na
mikataba hayana masuala nyeti yanayohitaji mamlaka ya
Tume kuweza kuyafuatilia? Kwa vyovyote vile- kamati ya
Jaji Bomani pamoja na kuundwa na Rais kwa mujibu wa
sheria za nchi yetu haiwezi kuwa na mamlaka
makubwa(executive authority). Kama Rais Kikwete
aliweza kuunda tume kadhaa haraka katika kipindi
kifupi cha utawala wake, ni vipi suala hili ameacha
kuliundia tume na badala yake ameunda kamati? Suala la
Mamlaka ni nyeti kwa kuwa ikumbukwe kuwa suala
alilolitaka Zitto Kabwe bungeni ni kuundwa kwa Kamati
Teule ya Bunge ambayo ni wazi ingekuwa na mamlaka
yanayoshabihiana na yale ya Tume ya Rais.

Ukitafakari masuala hayo kiundani utaoana suala la
kujadiliwa si kuwepo au kutokuwepo kwa Zitto Kabwe
kwenye kamati- Hoja ni Kamati yenyewe na dhamira ya
Rais Kikwete katika kuiunda Kamati hiyo. Katika
muktadha huo basi; maoni yangu ni kuwa kama serikali
haitarekebisha kasoro hizo zilizopo kuhusiana na hiyo
kamati, Zitto Kabwe kama mmoja wa wajumbe bado
anapaswa kuendelea kushiriki ili kuwasilisha na
kuwakilisha fikra mbadala katika kamati hiyo. Zitto
akawe hamira ya kuumusha na kuchachusha hoja na
mchakato wa kamati ya Bomani. Na kuendelea kumjadili
Zitto Kabwe badala ya kuendelea kujadili masuala hayo
ni kukwepesha mjadala wa msingi.

Kwa maoni yangu, CHADEMA kama chama cha demokrasia na
maendeleo kimefanya uamuzi wa busara mpaka sasa
kuruhusu mjadala huu. Maoni tofauti baina ya baadhi ya
wanaCHADEMA yamewasaidi kuimulika kamati na kufahamu
undani wake- utamaduni huu wa kuhoji na kutoa fikra
mbadala ni muhimu kwa mustakabali wa taifa letu na
unapaswa kuendeleza. Imenisikitisha kwamba Gazeti la
Mtanzania na Rai wamemua wazi kusambaza ujumbe kwamba
kwa kuwa na maoni hayo mimi(na wamenitaja kwa jina)
kwamba natanguliza maslahi binafsi badala ya maslahi
ya Taifa. Na wamehusisha maoni yangu na kuchunguzana
nani atagombea urais 2010 kupitia CHADEMA mintaarafu
umaarufu wa Mbowe na Zitto. Kwa maoni yangu, huu ni
mkakati mwingine wa wakagawe uwatawale (divide and
rule); haya mambo ya Urais yanatoka wapi tena wakati
Zitto hata miaka 40 ya kugombea Urais atakuwa
hajafikisha wakati huo? Bahati njema, naamini viongozi
wa CHADEMA hawawezi kuchonganishwa na habari za
magazetini.

Kwa maoni yangu mimi, hoja zote zinatetea maslahi ya
taifa na ni za kizalendo. Wanaotaka kamati iwe na
muundo, mfumo mzuri na mamlaka zaidi wanatetea maslahi
ya taifa na ni wazelendo kama ambavyo wenye mtizamo
tofauti nao ni wazalendo. Ni kupitia fikra hizi
mbadala ndipo tunapata kilichobora zaidi na kukiendea
kama taifa. Hivyo, kama ambavyo itikadi ya CHADEMA
inaamini katika siasa zilizojuu ya vyama zinazosimamia
ziadi maslahi ya taifa. Hivyo hivyo, wanaopinga
muundo, mfumo na mamlaka ya kamati, hawafanyi hivyo
kwa manufaa ya kisiasa ya CHADEMA, wanataka CHADEMA
itumike kama chombo tu cha kutumika kusimamia fikra
hizi mbadala na matokeo yoyote mazuri ya fikra hizi
yatasimamia rasilimali za taifa na matokeo yale
yatanufaisha watanzania wote bila kujali itikadi.
Wazalendo hawakai kimya wanapoona jambo lolote katika
taifa lao linakwenda tofauti na hoja zao ama za
makundi ya kijamii ambayo wanayawakilisha. Maoni ya
pande zote ni mazuri kufanya watchdog function kwa
kamati; kwa mfano mijadala kama hii inaweza kupelekea
kamati kuacha kufanya kazi kwa kificho; kamati kufanya
kazi kwa undani zaidi na pengine hata kufanya matokeo
ya Kamati hii kutekelezwa kwa sababu ya ufuatuliaji wa
karibu wa wa vyombo vya habari na umma. Mambo haya ni
muhimu yakajadiliwa wakati kamati inaendelea kufanya
kazi kwa sababu kazi ya kamati miezi mitatu
inagharamiwa na walipa kodi watanzania; fedha hizi
zingeweza kutumika kujenga madarasa- hivyo kama kamati
haitafanya kazi kwa kadiri ya matakwa ya umma matokeo
yake ni hasara kwa taifa kwa ujumla bila kujali
itikadi. Ifahamike mjadala kuhusu ufisadi na hatma ya
rasilimali za Tanzania ni suala pana kuliko Kamati ya
Bomani. Nikumbushe kauli niliyoitoa mwaka 2005 wakati
wa uchaguzi- “Tanzania ni yetu sote; SIASA SIO UADUI”.

Naamini Kamati kuu ya kesho baada ya kupokea maoni
mbalimbali italipokea na kulitolea msimamo wa chama
suala hili na PAMOJA TUTAFIKA.

Nautoa waraka huu leo Ijumaa 23 Novemba mwaka 2007:


John Mnyika
Mkurugenzi wa Vijana Taifa(CHADEMA)
0754694553
mnyika@yahoo.com

PS: Natarajia Gazeti la Mtanzania la 24/11/2007 na
Gazeti la Rai la Wiki ijayo mtachapa maoni yangu kama
sehemu ya maadili ya vyombo vya habari ya kutoa fursa
kwa mhusika kutoa maoni yake kabla ya kuandika habari
inayomhusu. Naamini mtachapa ufafanuzi wangu kuhusu
suala hili.


Kwa maelezo zaidi na rejea(tazama viambatanisho):

Sehemu ndogo ya maoni yangu ya 4 Novemba 2007 Kama
yalivyonukuliwa Na Tanzania Daima 5 Novemba,
2007(maoni baada ya Mkutano Mkuu wa CCM)

Ujumbe kwa baadhi ya Wahariri nilioutoa 19 Novemba,
2007

Muoneni sasa kada alipo, yaani waaaay back before the firm, nilikuwa nao hawa jamaa, i was among the first online kada's uniting with the so called wapinzani, we used to get together discuss issues na wazee yaani way back, NIKAONA KUNA KILA HAJA YA KUWA MPINZANI, kama unabisha you do the history*reference jina:KadaMpinzani, baada ya kukosa utendaji wa haki, kuzidisha siasa kupita kiasi angalau nilijua ni POLITICAL LUGGAGE, now am watching wapinzani kuongea vyovyote wanavyoweza to get their day by,thats the reason why i like to celebrate being a CCM Kada so i can visualize the collages and images of my life nilipokuwa na wapinzani JF with no regrets of hate, NOW ITS HARD FOR THEM TO BREATHE kama wapo kwenye high altitude, no wonder everything i touch turns into CCM haooo yaani hate kupita kiasi wakati nilishasema sana tuweni pamoja, tuwafichue jamaa bila ya kujali vyama,WAKAKATAA NA KUSEMA SI UENDE MWENYEWE* now i rather walk on the sideways talking than kuwa na hawa jamaa.

Anyway weekend njema !
 
Kada: nakuhurumia sana. Kazi unayoifanya ni ngumu mno japokuwa unajitahidi. Wapo wengi walipita hapa kwa nia ya kuitetea CCM walikimbia wenyewe. Hamna kitu kigumu kama kutete uovu au chochote kisichoteteeka. Haya endelea bwana, yetu macho. Lakini CHADEMA itakutoa kamasi, unajaribu kupanda mlima kilimanjaro wakati una asthma, utafia katikati!
 
sawa si tupo hapa ! mie sisemi sana ! hayo ya kutetea ccm umesema wewe mwenyewe !
 
" NIKAONA KUNA KILA HAJA YA KUWA MPINZANI, kama unabisha you do the history*reference jina:KadaMpinzani, baada ya kukosa utendaji wa haki, kuzidisha siasa kupita kiasi angalau nilijua ni POLITICAL LUGGAGE, now am watching wapinzani kuongea vyovyote wanavyoweza to get their day by,thats the reason why i like to celebrate being a CCM Kada so i can visualize the collages and images of my life nilipokuwa na wapinzani JF with no regrets of hate, NOW ITS HARD FOR THEM TO BREATHE kama wapo kwenye high altitude"

Kada!
Hii ni dalili ya kuweweseka, who is on the defensive sisiem or wapinzani? Sisiem sasa hivi inaweweseka? It is just a matter of time watakuwa History. Pamoja na dola wanaweweseka siku wakikosa dola tutawasahau. Pamoja na kashfa zote za IPTL, NBC, NMB, NET Group solusheni nama it bado unawasapoti. Una roho ngumu sana.
 
Mugo"The Great";103549 said:
" NIKAONA KUNA KILA HAJA YA KUWA MPINZANI, kama unabisha you do the history*reference jina:KadaMpinzani, baada ya kukosa utendaji wa haki, kuzidisha siasa kupita kiasi angalau nilijua ni POLITICAL LUGGAGE, now am watching wapinzani kuongea vyovyote wanavyoweza to get their day by,thats the reason why i like to celebrate being a CCM Kada so i can visualize the collages and images of my life nilipokuwa na wapinzani JF with no regrets of hate, NOW ITS HARD FOR THEM TO BREATHE kama wapo kwenye high altitude"

Kada!
Hii ni dalili ya kuweweseka, who is on the defensive sisiem or wapinzani? Sisiem sasa hivi inaweweseka? It is just a matter of time watakuwa History. Pamoja na dola wanaweweseka siku wakikosa dola tutawasahau. Pamoja na kashfa zote za IPTL, NBC, NMB, NET Group solusheni nama it bado unawasapoti. Una roho ngumu sana.

sasa kama mimi naweweseka iweje tena useme ccm ?? nikikosea mimi mnasema ccm ! inakuwaje wakuu !
 
Kada: nakuhurumia sana. Kazi unayoifanya ni ngumu mno japokuwa unajitahidi. Wapo wengi walipita hapa kwa nia ya kuitetea CCM walikimbia wenyewe. Hamna kitu kigumu kama kutete uovu au chochote kisichoteteeka. Haya endelea bwana, yetu macho. Lakini CHADEMA itakutoa kamasi, unajaribu kupanda mlima kilimanjaro wakati una asthma, utafia katikati!

Huyu mbona wanampa kazi ambayo haiwezi? Wakuu wake wakijua kazi waliyomtuma haifanyi ipasavyo ila anaishia kupiga ukasuku hapa sijui mlo wa wiki ijayo utakwepo?
 
Back
Top Bottom