KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,181
- 17,187
Nimeona niandike juu ya CHADEMA na si kwa Upinzani kwa jumla kwa sababu ndio waliolengwa wafe.
Sijui kama ACT-Wazalendo nao wanatakiwa wafe, au wao watavumiliwa wawepo pamoja na usumbufu wanaowapa watawala.
CHADEMA sio kwamba wapo tu na wana - 'savaivu' bali wanatambuliwa kuwa ni tishio kubwa ndio maana walitakiwa wafe. Kungali mapema ili wakati kama huu tukielekea kwenye uchaguzi mkuu pasiwepo tena na kuulizana itakuwaje!
CCM sasa itabidi wakubali. Wameshindwa kuwaua CHADEMA, na dalili zote zipo wazi kwamba hakuna njia ya kuwaua na kuwamaliza kabisa kabla ya uchaguzi mkuu Oktoba.
Kama sio COVID-19 iliyotuondoa mjini na kutupeleka kijijini, inawezekana kuwa ni aina ya 'sabbatical' ya kutafuta mikakati mipya ya kukabiliana na hawa CHADEMA?
Maana huu sio wakati wa kukaa lelemama kijijini huku ukijua kuna mambo makubwa yatakayokukabili miezi michache tu inayokuja.
Sitapenda kuijaza hii mada na mambo ninayofikiri CHADEMA wanapaswa kuwa wmeyafanya au wanayafanya, kwa maana hilo ndilo linaloweza kuwa michango kutoka kwa wasomaji wa mada hii. Kwa hiyo hili naliacha wazi, kasoro sehemu hii tu ndogo inayonikereketa akilini.
Viongozi (wabunge) wa CHADEMA wameeleza kutokwenda Bungeni kwa siku kadhaa kwa sababu ya coronavirus. Wanasema watajifungia Dodoma (?)
Je, huu muda utapotea bure? Kwa nini wasifanye Dodoma ndio iwe Chato yao kwa wakati huu!
Kama hawafanyi hivyo.(ngoja nisiwakosee heshima waheshimiwa).