CHADEMA haijafa, na bila muujiza haitakufa kabla ya Oktoba

Mimi ushauri wangu wabunge wa CHADEMA hata zikiisha siku 14 wasiende bungeni. Nahisi kuna mtego. Haya mapenzi ya Ndugai ya kuwataka warudi upesi bungeni yametoka wapi? Mbona alikuwa anawafukuza bungeni Siku za nyuma?
 
CHADEMA hata kama hawafanyi mikutano ya hadhara, bado CCM hawawezi kuwamaliza.

Yaani CHADEMA wanaweza kukaa kimya mwaka mzima, bado wananchi waka "respond positively" siku kiongozi yeyote wa CHADEMA akipatwa na tatizo, refer michango ya kuwatoa gerezani, hii ni stage ya juu sana ya ukomavu.

Inshort, by now; CHADEMA inatembea kwenye akili na mioyo ya watanzania wote wenye akili timamu, CHADEMA imekuwa kama kiungo kwenye miili yao, hawawezi tena kukiacha.

Wanaweza kujidanganya kuwapora ushindi wabunge/madiwani wa CHADEMA kwa lazima kwenye uchaguzi, but believe me; next time uchaguzi ukiitishwa, CHADEMA watashinda mara mbili mpk mara tatu zaidi sababu ya hasira watakazo kuwa nazo wananchi kwa uonevu wanaofanyiwa CHADEMA.

Kwa hapa kilipofikia, yeyote anayewaza kuiua CHADEMA ajue ni sawa na kuwanyima raha wote wenye kujielewa, atawanyon'gonyeza kwa muda, ila baadae awe tayari kwa kisasi chao.

Ukitaka kuiua CHADEMA, peleka watz wote hospital; "format" bongo zao, jaribu "install" pumba utazotaka, kinyume na hapo unajidanganya.

HAKUNA WAKUIONDOA CHADEMA KWENYE SIASA ZA TANZANIA, WATAMALIZA RESOURCES ZOTE, BUT THEY WON'T PREVAIL.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jiwe alifikiri kwa ukatili wake dhidi ya wapinzani wake ndiyo ingekuwa fimbo ya kuwamaliza. Matokeo yake kaimaliza chama chake mwenyewe. Hawa wanaounga mkono siyo kwa mapenzi yao wenyewe bali kwa nguvu ya dola na pia kulinda matumbo yao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hiyo hata ile kauli ya Bulembo kusema auawe katoka nayo Chadema??

Sent using Jamii Forums mobile app
Na anaye mdanganya Mkuu Siasa inapiganwa kwa risasi mabomu na kuweka watu wasiwasi anamdanganya sana aulize hata iliyo kuwa TANU (CCM) iliwezaje kumshinda Mkoloni Mweupe ulevi gani umewapata unasahau hata mlio kuwa mnatafuta uhuru kwa pamoja nao wanastahili japo heshima kwa vizazi vyo ambavo hata history bado mbichi kizazi cha pili
 
Ni kweli Mkuu kwani hata wale walionunuliwa kwa vyeo kama kina Waitara, Mollel na wengineo kila wakipata nafasi basi lazima waitamke Chadema ingawa kwa mabaya. Yote haya ni kuwaonyesha wale waliowanunua kuwa bado tunakumbuka tuliko toka.

Wako ccm kimwili lkn kiakili/kimawazo bado wako Chadema. Wanaumia sana mioyoni mwao kwa usaliti wao ndiyo maana hawafikirii kujijenga kisiasa huko waliko bali kujihangaisha na Chadema wakati walishaondoka.

Sijawahi kuwasikia Viongozi/Wabunge wa Chadema wakiwashambulia Wasaliti wale mara wapatapo nafasi. Hili liko wazi kuwa ukiondoka Chadema wao wanakusahau haraka na kujipanga upya ili kusonga mbele na siyo kupoteza muda kuwakejeli.

Hii ndiyo sifa kubwa ya Chadema inayowapa umaarufu ktk kujijenga kisiasa. Chadema hawana muda wa kumjadili mtu bali hoja. Tofauti na ccm wanaohangaika na watu individual. Ref kina Mh Lowassa na Sumaye walisakamwa kwa kejeli hadi walipokubali yaishe ndiyo kelele zikasha.

Chadema wao walishawasahau hakuna kuwakejeli wala kuwafuatafuata kwa maneno yasiyo na tija. Hii nndiyo Heshima ya Chadema. Ina Viongozi wastaarabu na wenye kujitambua.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba niongezee hapo nafkrir chairman mbowe ndo mtu makini anae waelkeza kuwapuuza kuna mtu alshawai kumskia mbowe anamtaja"slaa" tangu aondoke chadema na kuna kauli moja mbowe alsema "unweza kuongea ukaharbu lkn pia unweza kukaa kmya ukajenga".

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa CCM wangepewa nafasi ya Uungu siku moja tu tungepata shida Sana,hii corona ungekuwa ugonjwa wa Wapinzani tu na wanaowaunga mkono,na sio corona tu hata ukimwi kansa magonjwa ya moyo bp kisukari nk,wanaenda misikitini na makasani lakini hawana hofu ya Mungu hata chembe,huwa najiuliza wanaenda kwenye nyumba za ibada kufanya nini?
Najiuliza hivi hawa wanajua huko waendako hakuna CCM? Wafute vyama vya upinzani wabaki wao na vibaraka wao halafu tuone kitakachoendelea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuwatetea kwa kukwapua pesa za walalahoi na kuja kuzitumbua Dar badala ya kukaa bungeni ili mpitishe bajeti kwa ajili ya manufaa ya taifa!
Budget ipi, ile ya maigizo? Kinachokwenda wizarani ni chini ya 50%
 
Budget ipi, ya maigizo? Kinachokwenda wizarani ni ya 50%
Kama kinakwenda wizarani ni 50% inawezekana vipi kujenga vituo vya afya, hospitali ,mababarbara ,madaraja ,kununua ndege. na kusomesha watoto bure huku watumishi wanalipwa mishahara?
 
Kama kinakwenda wizarani ni 50% inawezekana vipi kujenga vituo vya afya, hospitali ,mababarbara ,madaraja ,kununua ndege. na kusomesha watoto bure huku watumishi wanalipwa mishahara?
Imba sana mapambio, LAKINI; hayo majengo,barabara, madaraja chini ya viwango.
TULIA Fuatilia kasi ya kubomoka nchi nzima. Pesa za elimu bure zaenda kiduchu shule zashindwa kuajiri hata mlinzi.
Mishahara bado ileile mwaka wa tano huu, pamoja kuwafuta vyeti feki na wafanyakazi hewa.
Tunajiita nchi tajiri wakati hatuna hata fungu/pesa ya kupambana na corona.Tulichojaaliwa kwa kuokoteza visingizio na kulazimisha hoja mfu. Mara kuugonjwa kadogo, sijui tunahujumiwa, mara hakuna ugonjwa.
Kufumba macho hakutasaidia kuepusha baa.
 
Kwa hiyo lile daraja la wami mnalopita kwenda kwenu wachina wamejenga chini ya kiwango?
 
Upo sahihi shida ni katiba mbovu tulionayo, hatakuwa na uchaguzi isipokuwa itakuwa ni vita.
 
Chadema ni nguvu ya wananchi ( umma ) kuiuwa unapaswa kuwauwa wananchi wote , je hili litawezekana ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…