Kwasababu ni zaidi ya wiki sasa chadema inawachangisha wanachadema na wananchi Tanzania nzima na makusanyo hayajazidi million 65, wakati Dr Emanuel Nchimbi, kwa siku moja tu, tena chini ya masaa ma3, halafu ni kwa watu wachache tu, amefanikisha kuchangwa kwa milioni zaidi ya 950, kwajili ya kusaidia matibabu ya wagonjwa wa mguu kifundo.
Ikumbukwe pia mwezi February tu mwaka huu2025, Dr.Emmanuel Nchimbi aliongoza harambee ya kwaajili ya ujenzi wa ofisi ya CCM Singida na chini ya masaa ma3, zilichangwa zaidi ya 1.7 billion.
Kwa hali hiyo,
chadema ina kila sababu kumtumia kiongozi huyu wa kitaifa kufanikisha jambo lao tone tone na kua matone kwa urahisi zaidi.
Nayasema haya sio kwa ubaya, bali ustawi wa demokrasia nchini.
Ndugu mdau wa jukwaa hili muhimu sana, sote ni mashuhuda zoezi ni zito na halisingi mbele, kwa mtazamo wako,
unadhani nini kinasababisha michango ya tone tone ya chadema kusuasua?
Ni kwasababu ya kutoaminika kwa chadema kama Chama cha siasa nchini kulingana na mienendo yake ya kususia michakato ya kidemokrasi?
Au ni kwasababu ya kutoaminika kwa viongozi wake wahamasishaji waliowekwa mstari wa mbele kwenye masuala haya ya fedha huku wakiwa na historia mbovu ya udokozi na ujambazi?
Au ni kwasababu wasimamizi wa mfumo wa uchangiaji michango hiyo wanajulikana kwa utapeli?
Kama mdau wa siasa Tz,
nini kinafanya michango hiyo ya tone tone ya chadema, isivuke million 65 kwa zaidi ya wiki? Au ndio lengo lilikua kiasi hicho?🐒
Mungu Ibariki Tanzania