CHADEMA haina heshima kwa viongozi wake, inataka kumwondoa Mbowe kihuni bila kujali mchango wake, Mbowe alitakiwa kustaafishwa kwa heshima kubwa

Chama cha Chadema hakina heshima kwa viongozi wake, kinataka kumwondoa Mh Mbowe kihuni bila kujali mchango wake mkubwa ndani ya Chama hiki, Mbowe alitakiwa kustaafishwa kwa heshima kubwa

Mh Mbowe amejenga Chama kwa gharama kubwa ya fedha na Wanachama kwa zaidi ya miaka 30 historia hii ni kubwa sana
Mbowe wakati akianza uenyekiti Chama kilikua na hali mbaya sana hasa idadi ndogo ya wanachama pamoja na fedha za kujikimu

Hivyo basi Mh Mbowe alitakiwa kustaafishwa kwa heshima kubwa sana katika mchango wake huu mkubwa na sio kihuni kama vile kinavyofanya kwa sasa

Tatizo hili limeanzishwa na Tundu Lissu mwanasiasa mwenye mdomo mrefu sana kuliko wanasiasa wengine ndiyo maana akaingizwa kwenye jaribio la risasi miaka iliyopita, hii redio yenye sauti kubwa sana inashutumu uongozi wa Mh Mbowe mara kadhaa hii inaleta picha kuwa Lissu ni mtu asiye na heshima wala adabu kwa Mwenyekiti wa Chama

Angekuwa na heshima angemshauri Mh Mbowe katika vikao vyao vya Chama ili wakija hadharani watuoneshe matukio mawili tu ya Mbowe kustaafu na Lissu kupewa Uenyekiti badala yake hili jambo linafanyika kihuni mwisho Mh Mbowe aonekane hana mchango wowote na kuvunjiwa heshima yake moja kwa moja

Mh Mbowe atambue kuwa kitendo hiki kwake ni cha kumshushia heshima na kuharibu mchango wake wote ndani ya Chadema hivyo basi maumivu yake yatalaani Chama hiki na hakitafanikiwa tena huu ndio utakuwa mwanzo wa Chadema kufa
🤔🤔🤔
 
Basi wenyeviti wa ccm wangeachwa kwa mchango wao, waendelee kubaki madarakani ?

yes amefanya kazi kubwa but muda hautambui hilo, muda unataka mabadiliko. Vizazi vinabadilika, watu wanabadilika, mahitaji yanabadilika.

Kiongozi yoyote ana option mbili, aendane na changes or aachwe nyuma
🙋‍♂️✍️🎯💐🤝🙏
 
Mbowe mwenyewe anachosha ameamua kuwasikiliza machawa wake. Sisi kumkosea heshima kataka mwenyewe. Wala usihofu jua kuwa akirudia kuwa mwenyekiti kwa muhula huu basi atakuwa level moja na Lipimba, Cheo na vile vyama 14. Kwa pamoja watakuwa wanatoa matamko.
 
Chama cha Chadema hakina heshima kwa viongozi wake, kinataka kumwondoa Mh Mbowe kihuni bila kujali mchango wake mkubwa ndani ya Chama hiki, Mbowe alitakiwa kustaafishwa kwa heshima kubwa

Mh Mbowe amejenga Chama kwa gharama kubwa ya fedha na Wanachama kwa zaidi ya miaka 30 historia hii ni kubwa sana
Mbowe wakati akianza uenyekiti Chama kilikua na hali mbaya sana hasa idadi ndogo ya wanachama pamoja na fedha za kujikimu

Hivyo basi Mh Mbowe alitakiwa kustaafishwa kwa heshima kubwa sana katika mchango wake huu mkubwa na sio kihuni kama vile kinavyofanya kwa sasa

Tatizo hili limeanzishwa na Tundu Lissu mwanasiasa mwenye mdomo mrefu sana kuliko wanasiasa wengine ndiyo maana akaingizwa kwenye jaribio la risasi miaka iliyopita, hii redio yenye sauti kubwa sana inashutumu uongozi wa Mh Mbowe mara kadhaa hii inaleta picha kuwa Lissu ni mtu asiye na heshima wala adabu kwa Mwenyekiti wa Chama

Angekuwa na heshima angemshauri Mh Mbowe katika vikao vyao vya Chama ili wakija hadharani watuoneshe matukio mawili tu ya Mbowe kustaafu na Lissu kupewa Uenyekiti badala yake hili jambo linafanyika kihuni mwisho Mh Mbowe aonekane hana mchango wowote na kuvunjiwa heshima yake moja kwa moja

Mh Mbowe atambue kuwa kitendo hiki kwake ni cha kumshushia heshima na kuharibu mchango wake wote ndani ya Chadema hivyo basi maumivu yake yatalaani Chama hiki na hakitafanikiwa tena huu ndio utakuwa mwanzo wa Chadema kufa
Lissu Muda gani alikuwa nje.

Muda wote chama kina kwenda na MBOWE ndiye akiongoza jahazi.
Mbowe ana mvuto wa aina yake.
Lissu ni mihemko na jazba. Chama kinahitaji kiongozi wa mipango na hekima sio jazba na muhemko.
 
Hakuna uhuni, hata wasanii wanajua kuna mda wa kukaa kwenye jukwaa na mda wa kuondoka. Ni mda wa Mbowe kuondoka. Wimbo ni mzuri ila umetushosha tunataka wimbo mwingine.
 
Hii sio namna nzuri ya kuaga viongozi
Kwani katiba ya Chadema inaelekezaje,kuhusu namna nzuri ya kuaga viongozi.?.
Zaidi ya chaguzi mbalimbali sioni kama katiba imekihukwa.
Kama una maelezo ya ziada ya namna gani katiba ya Chadema imevunjwa yadadavue hapa.
 
Mbona unamlilia mbowe? Unakumbuka nape na lile sakata lake kwa yule muhuni aliyemtolea bastola? Nape alilalama kuwa amekipigania chama mpaka akaumia halafu wahuni iweje wasitambue mchango wake. Alijibiwa na makada wenzake kuwa ilikuwa ni wajibu wake na alilipwa kwa kazi hiyo. Hata mbowe alifanya hivyo kwa faida ya chama, we unalia nini wakati kesho atatangaza kuhusu kugombea au kutokugombea? Hata akigombea unajuaje kama atashindwa, ile kauli yake ya kujiamini kuwa ataingia mzigoni hukuisikia? Suburi ashindwe ndio uje na hoja hii
 
Lissu anatosha. Mbowe alishatangaza atastaafu mwaka 2023, sijui Nini kilibadilika.
 
Lissu Muda gani alikuwa nje.

Muda wote chama kina kwenda na MBOWE ndiye akiongoza jahazi.
Mbowe ana mvuto wa aina yake.
Lissu ni mihemko na jazba. Chama kinahitaji kiongozi wa mipango na hekima sio jazba na muhemko.

Mihemko unayo wewe.
 
Basi wenyeviti wa ccm wangeachwa kwa mchango wao, waendelee kubaki madarakani ?

yes amefanya kazi kubwa but muda hautambui hilo, muda unataka mabadiliko. Vizazi vinabadilika, watu wanabadilika, mahitaji yanabadilika.

Kiongozi yoyote ana option mbili, aendane na changes or aachwe nyuma
Mbona ccm hakunaga uchaguzi??
 
Kwani katiba ya Chadema inaelekezaje,kuhusu namna nzuri ya kuaga viongozi.?.
Zaidi ya chaguzi mbalimbali sioni kama katiba imekihukwa.
Kama una maelezo ya ziada ya namna gani katiba ya Chadema imevunjwa yadadavue hapa.
Badala ya kustaafishwa kwa heshima anafukuzwa kama mbwa
 
Hivi mbowe anastaafishwa kwa njia ipi? Labda wazee wa chadema kama wapo wangemwomba asigombee
 
Kule kukaa katika nafasi hiyo kwa muda mrefu ni heshima kubwa! Na kama angetaka kuondoka kwa heshima angeachia Uongozi kwa hiari.
 
Back
Top Bottom