Uchaguzi 2020 CHADEMA haina pesa za kampeni, tuongeze nguvu za kuwachangia

Uchaguzi 2020 CHADEMA haina pesa za kampeni, tuongeze nguvu za kuwachangia

Countrywide

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2015
Posts
20,694
Reaction score
32,527
Habari wadau wa JF, leo nipo kuwakumbusha wanachadema wenzetu juu ya mwenendo wa chama kipindi hiki cha kampeni.

Mwanzo kabisa nilikuwa napinga kabisa watu kukichangia chama kwa maana hatujui hizo pesa zitatumikaje na pengine zinaweza kuishia mikononi mwa wajanja wachache kama ilivyo kwa miaka mingine.

Ila mimi ni binadamu na nina moyo wa huruma sana, siwezi kuweka msimamo kwa jambo ambalo najua linaenda au linamuumiza binadamu mwenzangu. Naweka angalizo, wanaotakiwa kuchangiwa ni wale ambao hawakuwahi kuwa wabunge na wala sio viongozi wakubwa chamani. Hali ya kifedha kwa CHADEMA kwa sasa ni mbaya mno, haijawahi kutokea.

Chama kinatakiwa kufanya kampeni za kwenda mbali zaidi ili kuwafikia wananchi wengi, lakini hadi sasa imeshindikana kutokana na uhaba wa pesa unaokikumba chama chetu. Hivi navyoongea kuna majimbo mengi sana (74) wagombea wa ubunge hawajaanza kampeni, hawa hawahusiani na wale waliokata rufaa ya kutoteuliwa.

Na tatizo la kutoanza kampeni ni uhaba wa pesa kwa maana hawana vitendea kazi kama magari na watu wa kuzunguka kuwasaidia kufanya hizo kampeni. Ninajua watu wanataka mabadiliko, lakini pia wanahitaji kuwanua hao wanaotaka kuwaletea mabadiliko na ndio maana nzima ya kampeni inapokuja.

Hivyo ni lazima kwa mgombea wa upinzani kufanya kampeni, ila kwa hali iliyopo ninaona dalili nyingi sana za majimbo mengi ya chama chetu chadema kwenda chama tawala. Tusije baadae kuanza kulalamika tumeibiwa kura wakati hadi sasa sehemu kubwa ya wagombea wetu hadi leo hawajaanza kampeni.

Hivyo kwa dhati ya moyo wangu, ninawaomba tuwachangie hawa watu ambao hawana kabisa rasilimali pesa.

Tuache kusema ruzuku imetumikaje kwa kwa kuwa wengi tunajua kilichotokea na pesa ilivyoliwa kijanja na baadhi ya viongozi wetu.
Chini ni picha ya mgombea wetu lissu alipokuwa zanzibar kwenye kampeni. Uchache huu wa watu pia ni sababu ya kukosekana pesa ambazo zingeweza kutumika kwa ajili ya matangazo ya kampeni na kufanya watu kuja wengi kwenye kampeni.

Hivyo tusaidie ili mambo yasiwe magumu zaidi ya yalivyo sasa. Leo hii lissu alibidi awe kwenye kampeni mkoa fulani, lakini yupo kwake Tegeta amelala

IMG_20200908_162606.jpg
 
Picha za saa 4 asubuhi mkutano saa9 😀 😀 😀 😀
 
Mimi binafsi sitachanga, ila kwa wale wenye moyo wa kuchanga nduo ninawaomba wazidishe mchango
We changa wenzio wazile Kwa kisingizio cha kampeni ,watz hawawezi kukabidhi nchi Kwa wahuni..!
 
Naomba kuuliza, kwani vyama vya siasa huwa havipewi pesa ya kampeni na serikali?
 
Havipewi, na hata kama vingepewa kuna wajanja wachache kwenye chama chetu ni mabingwa wa kuzitafuna.
Tuongoze michango, mwa sababu zikiwa nyingi sana hawawezi kutafuna zote
Naomba kuuliza, kwani vyama vya siasa huwa havipewi pesa ya kampeni na serikali?
 
Duh kuchangia hao mchwa! Kitu chochote kinachohusoana na hela usikiweke karibu nao! Wapo tayari hata kuama chama hawaaminiki hao!
 
Havipewi, na hata kama vingepewa kuna wajanja wachache kwenye chama chetu ni mabingwa wa kuzitafuna.
Tuongoze michango, mwa sababu zikiwa nyingi sana hawawezi kutafuna zote
Kumbe! basi mimi siku zote nkajua kuna ruzuku vyama vinapewa kupigia kampeni. Dah, ndio maana kuna mshkaji nkasikia anataka kukopeshwa!
 
WAAMBIE TUNAWADAI MAPATO NA MATUMIZI YA ZILE SADAKA WANAZO TOZA KWENYE ZILE NDOO NYEUPE.
WASITUTANIE KABISAA.
 
Na katika hili la kuomba michango, cdm itafanya tathmini ni jinsi gani inapendwa na wananchi.

waweke bakuli kwa meza.
 
Ila tuwaonee huruma, maji yashafika shingoni. Leo hii tunapozungumza hapa lissu yupo tegeta amelala. Walati ilibidi aende kwenye kampeni
WAAMBIE TUNAWADAI MAPATO NA MATUMIZI YA ZILE SADAKA WANAZO TOZA KWENYE ZILE NDOO NYEUPE.
WASITUTANIE KABISAA.
 
Bado watu wamegoma kuchangia, hivyo kwa wale wemye nacho wawasaidie tu
na katika hili la kuomba michango, cdm itafanya tathmini ni jinsi gani inapendwa na wananchi.

waweke bakuli kwa meza.
 
Ukweli kabisa mkuu, binafsi ukiondoa mapenzi makubwa niliyonayo Kwa JPM ni mpenzi pia wa Chadema Kwa mtu mmojammoja, kuna Watanzania wazuri kule wanafaa kuwa viongozi wetu na wanauwezo pia Ila sio Kwa upande wa Rais, kwenye swala la uraisi tuacheni mchezomchezo, JPM anatosha

Naweza kumchangia mgombea ubunge
 
Acha upuuzi, tuchange pesa ziende kuliwa na Mbowe na familia yake. Ile michango ya mil kila mbunge kwa ajili ya uchaguzi iko wapi?
 
Back
Top Bottom