1000 digits,
Acha kulisha watu udenda mchafu kiongozi. Kwani mbowe anagawa uongozi kama kule chama kingine ambako huwa hawagombei? Mbowe hana cheo cha kugawa viongozi wote wanachaguliwa sasa amempaje Lisu ukaimu. Kila mtu kachikua form alipoona anatosha. Na uchaguzi tar 18 Lisu sio naibu mwenyekiti bali kwa sasa ni mgombea.
Hivi unafikiri Mkapa angeamua kuweka wapambe au watu wake wangeweka wapambe au angetumia nguvu yake kama kiongozi wa chama na serikali kubadili katiba na kuondoa ukomo wa uenyekiti ndani ya Chama na ukomo wa kugombea Urais kupitia Chama chake pangetokea mazingira rafiki ya watu wengine kugombea ndani ya Chama chake ?Mpaka leo Mkapa angekua Rais wa Tanzania. Kama unakumbuka kipindi cha mwisho cha Uongozi wa Mkapa walijitokeza watu wakaanza kusema kuwa Mkapa katiba ibadilishwe ili waondoe ukomo Mkapa aendelee.
Kutokana Elimu kubwa Na akili kubwa ya Mkapa hakuwasikiliza wala hakupoteza muda kuwazungumzia wale walevi.
Kwa hulka aliyoonyesha Mbowe na akili na busara zake chache angekua ndio yeye Rais wa nchi angeanda magenge ya waandamanaji wadai kuwa awe Rais wa maisha na yeye angekubali na kujisifu kuwa nimetafakari nakaona nisikilize maombi ya watanzania.
Watu wanaoweka mbele Maslahi ya nchi na Demokrasia pana kwa vitendo wanakuwa tayari kujitoa sadaka kwa ajili ya wengi. Kujitoa sadaka kwa mwenye madaraka ni kuwa tayari kuachia ngazi hata kama bado unaweza kuongoza alimradi ukubali kuwa kina wengine wenye uwezo pia.
Mbowe angetoa hotuba nzuri ya kuwaasa watanzania kuhusu umuhimu wa Demokrasia ndani ya Vyama na Taifa kwa ujumla kwa kila ngazi na baada ya hapo angetangaza kuwa Sasa anakaa pembeni na kubwa mlezi wa Chama na kufungua Mlango wa Wanachama wenye uwezo kuchukua Form za kugombea nafasi yake ya Uenyekiti.
Na kwa sababu yupo kwenye Chama kwa muda Mrefu angeweza kabisa kutumia nguvu yake kuwakata wale wote ambao anajua kabisa hawana sifa na uwezo na kubakiza hata majina mawili au matatu tu ili wapigiwe kura na kupatikana Mwenyekiti Mpya.
CCM wangeogopa sana mana Demokrasia ndiyo mahitaji ya kizazi hiki na haikwepeki hata kwa mabomu ya nyuklia. Hata Chadema ilipata umaarugu kuliko Vyama vingine kutokana na kuachiana Uongozi kabla hata ya kuingia Ikulu.
Hali iliyowavutia vijana wenye ndoto za kuwa viongozi kujiunga na chama hicho kwa wingi.
Ndio maana vijana wengi wenye uwezo wa kujenga hoja na ushawishi walikua wanajiunga na Chadema mana kule CCM waliona hakuna Demokrasia zaidi ya kujuana na kurithishana Uongozi. Huyu ni mtoto wa kada Fulani basi apite bila kupingwa. Huyu ni kada Fulani apite bila kupingwa. Huyu ni mbunge wa jimbo Fulani basi asipingwe lile ni jimbo lake. Vijana wengi wakaona fursa ya kuonyesha vipaji vyao kisiasa vipo katika chama chenye Demokrasia ambacho kilikua ni Chadema wakati huo.
Sasa Chadema kimebeba mfumo wote wa CCM wa kubebana na kufanya figisu za kuvuruga Demokrasia.
Cha ajabu anayeongoza Figisu ni Mbowe na genge lake. Sasa kila jimbo,Kata,kijiji na mitaa kila mtu amejimilikishia Uongozi na kuwahadaa wananchi kuwa hapa kwenye hili jimbo Mimi ndio kiboko ya CCM hivyo kila anayejaribu kuchukua form anaitwa msaliti anatumiwa na CCM.
Nani mwenye akili zake atakayebakia ndani ya Chadema wakati akienda CCM anaonekana lulu na ndani ya Chadema anaitwa Msaliti,kisa anataka kuongoza chama au anapinga watu kujimilikishia Chama na uongozi wake.
Awamu ya Tano Mbowe akitumia mbinu zile zile za awamu ya NNE hakika atakiua chama kabisa mana kitakosa watu makini.
Mbowe anasifia awamu ya nne kuwa ilikua na Demokrasia lakini anashindwa kutuambia kuwa ni kwa nini aliamua kufuta kifungu cha ukomo wa Uenyekiti wa Taifa kama alikua anaona kuna Demokrasia? Je ,alimhofia nani wakati nchi ilikua ina mazingira mazuri ya kisiasa?
Ni wazi Mbowe alijiona ndiye kiboko wa kila mtu tangu JK wakati Dr.Slaa ndiye aliyekuwa kiboko wa Watawala tangu akiwa CCM mpaka alipohamia chadema ,ndani na nje ya bunge. Dr.Slaa alikua kiboko kweli lakini aliondoka na chama nusura kiingie Ikulu. Sasa huyu Mbowe anayejiita kiboko huku Chama kikipukutika kwenye mazingira ya matamko tu tena ya Polepole! Kweli !! Yaani Polepole anaitisha chadema na wanaufyata kama kuku wa kisasa,halafu anatokea mtu mmoja aliyeshindwa kujenga spirit ya mapambano anajiita kiboko wa CCM. Kiboko kinachoigopa mikwala ya CCM Tena CCM iliyoparaganyika.
Watu na akili zao badala ya kushtuka na kumweleza Mbowe ukweli wanampamba huku Chama kikikosa dira.
Hivi CCM wangekua wanamuogopa Mbowe wangeshindwa kuandaa igizo la maandamano nchi nzima huku wakijifanya ni wanachadema na kupinga mbowe kujiongezea muda? Au ni kitu gani wanashindwa kumfanya ?
Kama Mbowe ndiye Tishio kwa CCM Kwa nini Tageti ni akina Mdude Chadema, Lisu, Saanane, Mawazo n.k ?
Kwa nini Mbowe hawi mkweli na kusema kuwa Chadema imejengwa kwa mawazo na nguvu ya wanachama wengi na sio yeye peke yake?
Mbowe anatofauti gani na yule wa Chama kikubwa anayesema yeye ndiye ameleta maendeleo ya nchi na wenzake wote waliotangulia hawakufanya kitu zaidi ya wizi tu?