CHADEMA hawana uwezo wa kuchukua nchi. Wakikamiwa wanapoa Kama uji wa dundi

UPUUZI MTUPU!

Salama Wakuu!

Kwa jinsi mambo nilivyoyakuta na yalivyosasa kuhusiana na Siasa za nchi hii, nadiriki kusema kuwa CHADEMA bado Sana katika kuchukua nchi.

Nimeanza kufuatilia Siasa mwaka 2005, mpaka sasa ni miaka 16. Sio miaka mingi ila pia sio michache Sana. Inatosha Kueleza Jambo.

Nikiwatazama CHADEMA, kisha nikiwaangalia Watanzania, alafu nikamalizia na CCM wenyewe. Ni wazi kuwa, CHADEMA bado Sana kuchukua nchi hii.

Hawana uwezo Kwa sababu, hawana uwezo wa kukaza, hawana uwezo wa mapambano makali ya Muda mrefu.
CHADEMA ni Kama watoto, ambao Sisi wanafasihi tunasemaga Ngoma ya watoto haikeshi.

Kama ni kwenye riadha CHADEMA wanaziweza mbio fupi za Mita Mia, hapo wanaouwezo wa kukimbia Kwa Kasi kubwa wakashinda. Lakini mbio ndefu hakika CHADEMA wamethibitisha kuwa hawaziwezi. CCM wao wamejithibitishia kuwa wao ni mabingwa wa mbio ndefu.

CHADEMA kwenye Uwanja WA vita wapo kwenye kundi ambalo wanapenda ukanda wenye mashambulizi yaliyopoa, hawahimili ukanda wenye mashambulizi makali yasiyokoma.

CHADEMA wamepoa Kama uji wa dundi.
Mengi wanayoyapigania wameshindwa kuyapata, wanaishia kulalamika tuu.

Siku zote kwenye maisha, ukishakuwa upande wa mlalamikaji basi jua umekwisha.

CCM wao ni watu wakuchukua hatua. Hawalalamiki.

CHADEMA mkiendelea hivi kuwa Kama uji wa dundi, mtakatika vipande vipande.

Nawasilisha
 
Haya mambo shida wanayaanzia juu kitu cha kufanya wawajaze sumu kwa Raia huku chini kwa muda wa Miaka miwili Then ndo waende kwenye media lakini haya masuala ya kukimbilia camera fasta hawawezi fika
Hii siri usiiseme kwa nguvu.
Punguza Sauti
 
Sisi watanzania waoga kama nini, tukiambiwa tuidai haki yetu utasikia ooowao wamekaa huko sisi tunapigwa virungu huku, hakuna haki bila ya kutoka jasho tusidanganyane tutabakia kushangaa kwa wenzetu tu sisi kamwe hatuna uthabiti wa kutoka moyoni.
 
Nimecheka kishenzi huu uhuni ulioandika hapa. Ccm kipindi cha JK walituimbisha umeme wa Gas sijui uchumi wa gas kama watoto wadogo. Huku wakisema umeme wa maji tatizo ni mabadiliko ya tabia nchi. Bomba la gas likifika Dar. Kipindi cha Magufuli wakasema umeme wa maji ndio wenyewe maana ni wa bei rahisi, sasa tuko kwenye bwawa la SG, Je yale mabadiliko ya tabia nchi yaliisha kipindi cha JK mpaka tumerudi kwenye umeme wa maji? Tupe msimamo wa ccm kwenye Hilo.
Huwa nafuatilia maandiko yako, nashangaa sana. Hujui advantage za Hep vs gas?
 
cdm na watanzania pia ni tatzo,
em post picha ya huo uji😂
 
Sisi watanzania waoga kama nini, tukiambiwa tuidai haki yetu utasikia ooowao wamekaa huko sisi tunapigwa virungu huku, hakuna haki bila ya kutoka jasho tusidanganyane tutabakia kushangaa kwa wenzetu tu sisi kamwe hatuna uthabiti wa kutoka moyoni.

Watanzania hatujaona tatizo. Shida hamtafanikiwa kwa kuwa ninyi mmekuwa sehemu ya tatizo. Kwanza mna kelele sana. Pili jina Demokrasia Lakini mtu akitoa maoni yake yasipofanana na yenu Basi matusi na kuongozana kuattack. Mpo so shallow. Mnajiona wengi sana humu Lakini Ni watu wa ovyo sana. Amani yetu Ni muhimu kuliko Siasa za kijinga na za kila wakati. Nchi maskini Ni muda wa kazi. Kazi. Kazi. Siasa Ni za watu walioshibaaaa.
 
Nimecheka kishenzi huu uhuni ulioandika hapa. Ccm kipindi cha JK walituimbisha umeme wa Gas sijui uchumi wa gas kama watoto wadogo. Huku wakisema umeme wa maji tatizo ni mabadiliko ya tabia nchi. Bomba la gas likifika Dar. Kipindi cha Magufuli wakasema umeme wa maji ndio wenyewe maana ni wa bei rahisi, sasa tuko kwenye bwawa la SG, Je yale mabadiliko ya tabia nchi yaliisha kipindi cha JK mpaka tumerudi kwenye umeme wa maji? Tupe msimamo wa ccm kwenye Hilo.
Ujinga wa CCM unahalalisha CDM nao kufanya ujinga?
 
Watanzania hatujaona tatizo. Shida hamtafanikiwa kwa kuwa ninyi mmekuwa sehemu ya tatizo. Kwanza mna kelele sana. Pili jina Demokrasia Lakini mtu akitoa maoni yake yasipofanana na yenu Basi matusi na kuongozana kuattack. Mpo so shallow. Mnajiona wengi sana humu Lakini Ni watu wa ovyo sana. Amani yetu Ni muhimu kuliko Siasa za kijinga na za kila wakati. Nchi maskini Ni muda wa kazi. Kazi. Kazi. Siasa Ni za watu walioshibaaaa.
Ni mawazo yako na nayaheshimu.
 
Huwa nafuatilia maandiko yako, nashangaa sana. Hujui advantage za Hep vs gas?

Kabla ya kutaka umeme wa gas, tulikuwa tunatumia umeme wa maji, bado Tanzania haikuwa na umeme wa bei rahisi kulinganisha na nchi nyingine za Afrika mashariki. Tuchukulie HEP ni nafuu kuliko gas, je ilikuwaje ccm yote kabla ya 2015 kutuaminisha kuwa gas ni muarobaini wa nishati yetu? Ulikuwa wapi wakati huo kuonyesha kuwa umeme wa maji ndio sahihi?
 
Kwani mipango ya kiuchumi huwa haibadiliki? Mipango ya kiuchumi huwa inabadilika ndugu. Mnaweza kupanga kuwa na gas electricity na baadae mkaona mmebugi kisha mnaenda kwenye maji. Acha kukariri.
 
Ingekuwa ni kubadilika kwa mipango ya uchumi hapo sawa, ila sio mabadiliko kwa utashi wa rais aliye madarakani. Kwenye gas tumekopa 3t, kisha ndani ya muda mfupi tunakopa 6.5t kuanzisha mradi wa umeme wa maji. Nani atalipa 10t kwa ajili ya huduma hiyo hiyo? Hiyo sio akili bali ni matope. Halafu mnaongopea watu kuwa umeme utakuwa bei rahisi, utakuwa bei rahisi huku ukiwa na deni la 10t?
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Upo upande upi mkuu, ccm ama sio ccm??
Kama ni ccm basi bandiko liko sawa. Ila kama haupo upande huo basi bandiko halijakamiika hilo, ni njia zipi sasa watumie hao chadema unazoona wewe ni sahihi kupambana na dola.??

Maana kwa mazingira ya hapa kwetu inahitaji moyo wa chuma kua mpinzani halisi aisee, kupotezwa na kuswekwa rumande ni dakika 0.
 
Ingekuwa ni kubadilika kwa mipango ya uchumi hapo sawa, ila sio mabadiliko kwa utashi wa rais aliye madarakani. Kwenye gas tumekopa 3t, kisha ndani ya muda mfupi tunakopa 6.5t kuanzisha mradi wa umeme wa maji. Nani atalipa 10t kwa ajili ya huduma hiyo hiyo? Hiyo sio akili bali ni matope. Halafu mnaongopea watu kuwa umeme utakuwa bei rahisi, utakuwa bei rahisi huku ukiwa na deni la 10t?
Una hakika na ulichoandika? Kwamba tril 10 zilikopwa? Au unaropoka ukidhania mimi ni mpuuzi?
 
Sio Kuchukua tu, Uwezo wa Kuongoza tu Hawana.... ! Jaribu tu Kuwaza Mnyika ndo PM !! Waishie huko huko kwenye Saccos Yao...!
Sasa huyo PM wenu si mwalimu tu wa michezo Ana jipya gani Bora Mnyika😁😁😁😁😁
 
Unauliza au unapigia jibu mstari?
Screenshot_20210817-161110.png
 
Back
Top Bottom