CHADEMA, hiki ndio kipindi cha kuandaa makongamano mengi ya Katiba Mpya

CHADEMA, hiki ndio kipindi cha kuandaa makongamano mengi ya Katiba Mpya

Poa 2

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2019
Posts
1,317
Reaction score
1,320
Ni wazi kabisa kwamba Serikali (CCM) imedhamiria kufubaza harakati za kudai katiba mpya Tena kwa nguvu zote, na hii ndio maana ya kumbambika mbowe kesi ya Ugaidi.

Lengo lao kubwa ni kuwatisha Ili mpunguze Kasi, Kesi ya mbowe itapigwa danadana Sana mpaka pale ninyi mtakapo ishurutisha serikali kwa mbinu zozote zile.

Mapambano yenu kwa Sasa yalenge kuandaa makongamano mengi ya katiba mpya, msipofanya hivyo maana yake mtakuwa mmenasa kwenye mtego wa maadui.

Kesi ya mbowe ni ukurupukaji mkubwa wa serikali na vyombo vyake, na imewakwama kabisa haitafuniki,haitemeki, Wala haimezeki, kuendeleza makongamano ndio njia pekee itakayoongeza joto kali zaidi kwa serikali.

Makamanda huu sio mda wa kurudi nyuma Kama kuumizwa mmeumizwa Sana, kudhulumiwa mmedhulumiwa sana, Kama kuteswa mmeteswa Sana mkilegeza kidogo TU chadema itakuwa Kama nccr, Cuf au TLP siku chache zijazo.
Wanachama, wafuasi, na wananchi kwa kiasi tuameanza kuchoka matamko na malalamiko yenu yaleyale ya siku zote, tunatamani kuona mbinu mpya na hatua zaidi ya makelele yasiyo na matokeo chanya

Na Pia kuendelea kutumia demokrasia ya kistaarabu kushindana na ccm heti kwamba kesho wakupeni nchi ni kusubiri dodo chini mkorosho, ccm wamevuka kiwango Cha uovu Sasa ni magaidi na mashetani wekundu kabisa ambao wako tayari kwa chochote mnachelewa nyinyi TU kuikomboa hii nchi.

Wananchi tuko tayari na dunia iko tayari mnasubiriwa nyinyi muunganishe nyaya ukombozi upatikane

😚😂😂( Ni jamaa kutoka ighanuda) 😂😂😂😂
 
Tuko radhi kuachia wafungwa wote ili tuweke wachadema magerezani. Nimeongea kwa niaba ya selikari
 
Mwambieni pambalu aanze jamaa muoga kama nini kakamatwa siku mojatu mwanza kahojiwayaani hataki hata kuja kwenye kesi kisutu
 
Tatizo hata makongamano yakiitishwa mwitikio unakuwa mdogo sana.
 
MWAQMBIENI PAMBALU AANZE JAMAA MUOGA KAMA NINI KAKAMATWA SIKU MOJATU MWANZA KAHOJIWAYAANI HATAKI HATA KUJA KWENYE KESI KISUTU
Sawa makamanda watamwambia
 
Kama Wana kibari waandae kama hawana wasithubutu , wazungu hawatawasaidia wakati wanapewa kisago
 
Anza wewe kuandaa hapo ulipo, tafuta ukumbi, weka mabango and tafuta gari la matangazo utangaze mji mzima. Then uje utupe mrejesho nini kimetokea
 
Jambo linalohitajika kwenye jamii huwa halijifichi kama kweli wananchi hitaji lao namba moja katiba mpya basi ungelisikia kila KONA lakini kwa sasa ni tofauti kabisa limebakia kwa baadhi ya wafuasi wa vyama ambao kufanya hivyo ni ajira kwao.

Kama Serikali ingewapuuza Wala wasingefanya chochote hizi kelele zimesikika kutokana na kamatakamata jambo kuu Serikali ingeongeza ufanisi Katika kutekeleza majumu yake.

Wanaojadili katiba ni wale wale hoja ni zilezike hamu Yao Rais asiwe na madaraka MAKUBWA! hawajiulizi Nani aliyempa madaraka hayo na ni kwanini? Hawajiulizi Nani alitunga katiba iliyopo kwa manufaa GANI?

Nchi zilizoendelea katiba zao zimewasaidiake kufikia maendeleo? Wachina,Warusi,Wamarekani,Waarabu na waingereza.

Tatizo Katika nchi yetu siyo katiba Wala CCM. tatizo ni sisi wote wananchi uwajibikaji upo chini ya kiwango Leo ukitoa bilioni moja ijenge daraja utakachokishuhudia ndiyo hali halisi ya mtanzania Kuna MAHALI tulikosea Katika kuanza matokeo yake tumezaliza vizazi vya kila kitu ni deal na deal inapigwa katikati ya Sheria Kali mifumo hii inatatizwa na kizazi hiki kipya njia ya kutoka hapa ni kutumia udikteta kwani watanzania kwa KUPANGA maneno na kuyatengeza yakavutia kwa wafadhili ni mahili mno.
 
Jambo linalohitajika kwenye jamii huwa halijifichi kama kweli wananchi hitaji lao namba moja katiba mpya basi ungelisikia kila KONA lakini kwa sasa ni tofauti kabisa limebakia kwa baadhi ya wafuasi wa vyama ambao kufanya hivyo ni ajira kwao...
Ni lini uliwauliza watanzania juu ya katiba mpya na wakakujibu sio hitaji lao? Na kwa Nini mnawazuia chadema kufanya makongamano yao Ili tuone wananchi wataitikia au kukataa, lini wanasiasa wamekuwa si wananchi/raia
 
Back
Top Bottom