Kwa jinsi ninavyoiona hoja ya CHADEMA ya no reform no election haija kaa vizuri inalenga kukiua chama moja kwa moja.
Hoja ambayo ni practical na ingekuwa na mashiko ni kuelemisha wananchi wazuie wizi wa kura kwa namna yoyote ile. kuzuia uchaguzi ni kujindaganya ni bora CHADEMA washiriki lakini watafute mikakati ya kuzuia wizi wa kura na kuzuia kutangaza wasioshinda.
Hii ni pamoja na kupitia mchakato mzima kuona nini kifanyike ili kuzuia maonevu. wafanye utafiti ili kupata suluhisho. washirikishe viongozi wa dini, wasome, nk kupata mawazo mbadala. option b ya mkakati wa no reform no election.
Soma Pia: Pre GE2025 - Tundu Lissu: Kauli ya No Reform No Election hatujasema tunasusia Uchaguzi. Tutaongea na Rais Samia lugha atakayoielewa
Kukosa option B ndiyo failure yenyewe.ELIMU NA UHAMASISHAJI KWA WANANCHI iweni kipaumbule chetu.
1. Ndugu
tripof, NO REFORMS, NO ELECTION sio hoja ndogo au moja tu kama unavyoelewa wewe. Hiyo ni movement iliyobeba hoja nyingi muhimu ndani yake mojowapo ya hoja hizo zilizo ndani ya hii movement ni hii hii unayopendekeza wewe hapa yaani "kuzuia wizi wa kura..."
2. Wizi wa kura hauzuiwi kwa kuingia ktk uchaguzi chini ya mfumo uliopo wa uchaguzi ambao sheria, kanuni na katiba iliyopo ina - facilitate wizi wa hizo kura. Imefanyika hivyo ktk chaguzi zote chini ya mfumo wa vyama vingi tangu mwaka 1995 hadi leo uhuni na uchafu wa demokrasia ya uchaguzi kwa namna hiyo unaendelea...!
4. Ndo kusema kwamba, pendekezo lako hili ni sawa na kuwaambia CHADEMA waende wakatwange maji kwenye kinu wakitaraji kuwa yatageuka kuwa mchele wa kupika na kuliwa. CCM hawako tayari na hawataki tena uchaguzi. The only option iliyopo ni kuwalazimisha au tuwatoe kabisa njiani maana hawa ni kizuizi cha demokrasia ya kweli na maendeleo ya taifa letu...!!
3. Ni mtu mjinga pekee ambaye hukimbilia kutibu matokeo ya tatizo badala ya chanzo au shina la tatizo hilo. Shina la tatizo la wizi wa kura au kuibiwa uchaguzi wote na maCCM hapa Tanzania msingi wake ni ubovu wa mfumo wa uchaguzi chini ya katiba inayozaa sheria na kanuni mbovu za kusimamia chaguzi zenu....
4. So, there's no other way ya kutibu tatizo hili once and for all isipokuwa kuufumua mfumo wote na kuutengeneza upya. We understand that this is not an easy job. It can take time and cost, but if we decide and make full commitment, it's going to be done...!
5. Na msingi wa hoja yako ya kuwa "NO REFORMS, NO ELECTION" itaiua CHADEMA ni nini hasa? Je, unamaanisha CHADEMA itafutwa na msajili wa vyama siasa/serikali? Kama ndizo fikra zako, kwanini aifute? Hebu sema, umejenga hoja ya "kufa CHADEMA" ukisimama ktk msingi gani hasa..?
6. Sikia bwana
tripof. Usipende niamini kuwa hoja yako hii umeijenga ktk fikra kwamba, kwa kuwa CCM wanaweza kufanya uchaguzi mkuu mwaka huu 2025 bila kujali grievances za CHADEMA na hivyo wakajishindisha kwa 100% na CHADEMA wakawa hawana Rais hata mmoja, mbunge hata mmoja, diwani hata mmoja, Mwenyekiti wa Kijiji/mtaa/kitongoji hata mmoja na kwa sababu hii akili yako inakuambia kuwa "ooh, CHADEMA itakufa". Hii ndiyo maana yako, au siyo...?
7. Kama hiyo👆👆ndiyo msingi wa hoja yako ya "CHADEMA itakufa", Sasa naweza kukuuliza swali moja tu la msingi. Kwamba, kwani toka uchaguzi wa vijiji/mitaa wa mwaka 2019, uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 na wa vijiji na mitaa wa mwaka 2024 CHADEMA ina wabunge wangapi? Ina madiwani wangapi? Ina hata Rais? Ina wenyeviti wa vijiji na mitaa wangapi....?
JIBU LA MASWALI HAYO YOTE UNAYAJUA VYEMA KUWA:
• CHADEMA haina Rais, haina wabunge, haina madiwani wala haina wenyeviti wa vijiji/mitaa kwa kuwa ktk chaguzi zote hizo CCM iliharibu na kupora chaguzi zote na hivyo wakajitangaza wenyewe kwa mabavu kuwa ni washindi kwa 100%..!!
• Sasa pamoja na hayo, CHADEMA imekufa? Je, sio kwamba ndo tu kimekuwa chama kikubwa zaidi na kuwa tishio zaidi kuliko hata ilipokuwa na Wabunge na madiwani? Sasa hoja yako ya "kufa" unaitoa wapi? Mimi nakuambia, haitakufa, labda ufe wewe na CCM yenu...!!
NDO KUSEMA KWA HIYO, KWAMBA: Hii hoja yako ni "nonsense" haina msingi na inalenga kuchelewesha mabadiliko ya kweli tu...
NAKUSHAURI, acha woga na uchawa. Jiunge kwenye mapambano kuipambania nchi yako kutoka kwenye makucha na midomo ya manyang'au CCM....!!
KWA heri, usiku mwema...