Pre GE2025 CHADEMA hoja yenu iwe ni kuzuia wizi wa kura na siyo kuzuia uchaguzi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Chadema kama itakua si ndiyo furaha yenu, poleni pilau msherehekee wajinga wanao kiua chama.
Hizi akili zenu zitaliingiza taifa kwenye mauaji huko mbele , sio vizaz vyote watakuwa wapumbav kama , kipo kizaz kitahitaj usawa , Rais lazima ajiuzuru apishe uchaguz pia lzm , jeshi liboreshwe , liondolewe itikadi za kisiasa ambazo ccmu. wamepandikiza pia tume iundiwe mfumo wa kupara watu wa tume

TUKIPUUZIA LEO,KESHO TUTACHINJANA KAMA KUKU , SIO VIZAZ VYOTE WATAKUWA WAJINGA KAMA MIMI NA WEW , YAANO MGOMBEA MMOJA KAPEWA FURSA YA KUSET UP UCHAGUZ MZIMA NA UNAHISI HATOTUMIA HIYO FURSA KUJIWEKEA MAZINGIRA MAZURI

TUENDELEE KUHISI HAYA NI MAMBO YA SIMBA NA YANGA , MPK MUONE DAMU NDO AKILI ZITAWAKAA , HATA RWANDA WATUTSI WALIZOEA KUUA VIONGOZ WA KIHUTU MPK WALIPORUDIA MWAKA 1994 NDIPO LEO KAGAME ANAJARIBU KULETA USAWA HATA WA MAIGIZO MAANA AMEONA NA AMEJIFUNZA

CCMU ENDELEENI KUSUBIRI MATATIZO NDO MCHUKUE HATAU
 
Umenielewa ninachomaanisha au umekurukpuka!!?
Chadema haiwezi tumia nguvu ya imma coz mbinu hiyo ilishafeli mara nyingi sana!!

Sasa basi kauli yao hiyo Ina support toka wapi!!?najiuliza tu!!
hv ww unahitaj nguvu ya umma kufanya marekebisho kwa maslai ya nchi ?

ukiitwa chimpzee utakasirika ?
 
Nilikuwa namjibu huyo anaesema Chadema wazuie wizi wa kura

Hadi unazuia kuibiwa kura umeingia ulingoni je ukienguliwa kabla hata ya upigaji kura utazuia nini?
Uhalisia vyote haviwezekani kwa uchaguzi ujao.
Wote waliojaribu kuzuia wizi wa kura wametekwa na kuuawa, fuatilia uchaguzi wa serikali za mitaa uliosimamiwa na Mtukufu Mchengerwa
Tutazuia uchaguzi na sio kwamba tutasusia uchaguzi.


Kamwe, hakuna uwezekano wa kuzuia kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu Mwaka huu wa 2025.
Aidha, ni kweli kabisa kwamba Hoja za Watu wa CHADEMA ni za kweli, pia ni za msingi. Hoja zao zina mashiko kuhusiana na Kukosekana kwa Mamlaka zinazoaminika kwa ajili ya kusimamia Uchaguzi ulio huru, wa HAKI na ulio wa Wazi.

Jambo muhimu zaidi la kuzingatiwa ni kwamba: KAMWE CCM HAITAWEZA KUKUBALI KWA HIYARI KUBADILISHA MIFUMO YA UCHAGUZI. NA KAMWE CCM HAITAWEZA KUKUBALI KWA HIYARI KUBADILISHA KATIBA YA NCHI.

KAMWE HAUPO KABISA UWEZEKANO WA KUBADILISHA KATIBA YA NCHI KWA NJIA ZA KIDEMOKRASIA. HAUPO UWEZEKANO!

Kwa bahati mbaya sana, huu ndio Ukweli mchungu Sana kupita kiasi!
 

Attachments

  • 5811771-84b12f6d5ff81d807821a183416ac2ed.mp4
    648.4 KB
Umejikatia tamaa ukiwa wapi mkuu?
 
Yani hapo ulipo wasubiri kufa tu nothing else kazaa wewe ni wakiume ujue
 

..wasubiri kwanza washindwe kuzuia uchaguzi.

..watakaposhindwa kuzuia uchaguzi, jitokeze uungane nao kuzuia wizi wa kura.
 
TUME Huru ya Uchaguzi ndio kazinyake na sio CHADEMA iwepo TUME huru na hesabu ziwekwe wazi na mshindi ajulikane kwa uwazi. Polisi sio kazi yao kuwepo vituoni kibeba maboksi za kura na risasi za moto!.
 
Uko nchi gani? Hujaona kuwa majina ya wapinzani mengi hata kufika kwenye ballot paper hayafiki? Wanaanza kuambiwa hawajui kuandika majina yao au kujaza fomu. Au hawajali kabisa upigaji kura bali wanatangaza wagombea wa CCM. Utazuia wizi wa kura lakini mgombea wako hatatangazwa.
 
Ebu eleza ni kwa namna gani wanaweza kuzuia wizi wa kura wakati mawakala wao wanafukuzwa au hawaruhusiwi kuingia vyumba vya kuhesabia kura au hata kufukuzwa wakati wa majumuisho ya kura?
 
1. Ndugu tripof, NO REFORMS, NO ELECTION sio hoja ndogo au moja tu kama unavyoelewa wewe. Hiyo ni movement iliyobeba hoja nyingi muhimu ndani yake mojowapo ya hoja hizo zilizo ndani ya hii movement ni hii hii unayopendekeza wewe hapa yaani "kuzuia wizi wa kura..."

2. Wizi wa kura hauzuiwi kwa kuingia ktk uchaguzi chini ya mfumo uliopo wa uchaguzi ambao sheria, kanuni na katiba iliyopo ina - facilitate wizi wa hizo kura. Imefanyika hivyo ktk chaguzi zote chini ya mfumo wa vyama vingi tangu mwaka 1995 hadi leo uhuni na uchafu wa demokrasia ya uchaguzi kwa namna hiyo unaendelea...!

4. Ndo kusema kwamba, pendekezo lako hili ni sawa na kuwaambia CHADEMA waende wakatwange maji kwenye kinu wakitaraji kuwa yatageuka kuwa mchele wa kupika na kuliwa. CCM hawako tayari na hawataki tena uchaguzi. The only option iliyopo ni kuwalazimisha au tuwatoe kabisa njiani maana hawa ni kizuizi cha demokrasia ya kweli na maendeleo ya taifa letu...!!

3. Ni mtu mjinga pekee ambaye hukimbilia kutibu matokeo ya tatizo badala ya chanzo au shina la tatizo hilo. Shina la tatizo la wizi wa kura au kuibiwa uchaguzi wote na maCCM hapa Tanzania msingi wake ni ubovu wa mfumo wa uchaguzi chini ya katiba inayozaa sheria na kanuni mbovu za kusimamia chaguzi zenu....

4. So, there's no other way ya kutibu tatizo hili once and for all isipokuwa kuufumua mfumo wote na kuutengeneza upya. We understand that this is not an easy job. It can take time and cost, but if we decide and make full commitment, it's going to be done...!

5. Na msingi wa hoja yako ya kuwa "NO REFORMS, NO ELECTION" itaiua CHADEMA ni nini hasa? Je, unamaanisha CHADEMA itafutwa na msajili wa vyama siasa/serikali? Kama ndizo fikra zako, kwanini aifute? Hebu sema, umejenga hoja ya "kufa CHADEMA" ukisimama ktk msingi gani hasa..?

6. Sikia bwana tripof. Usipende niamini kuwa hoja yako hii umeijenga ktk fikra kwamba, kwa kuwa CCM wanaweza kufanya uchaguzi mkuu mwaka huu 2025 bila kujali grievances za CHADEMA na hivyo wakajishindisha kwa 100% na CHADEMA wakawa hawana Rais hata mmoja, mbunge hata mmoja, diwani hata mmoja, Mwenyekiti wa Kijiji/mtaa/kitongoji hata mmoja na kwa sababu hii akili yako inakuambia kuwa "ooh, CHADEMA itakufa". Hii ndiyo maana yako, au siyo...?

7. Kama hiyo👆👆ndiyo msingi wa hoja yako ya "CHADEMA itakufa", Sasa naweza kukuuliza swali moja tu la msingi. Kwamba, kwani toka uchaguzi wa vijiji/mitaa wa mwaka 2019, uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 na wa vijiji na mitaa wa mwaka 2024 CHADEMA ina wabunge wangapi? Ina madiwani wangapi? Ina hata Rais? Ina wenyeviti wa vijiji na mitaa wangapi....?

JIBU LA MASWALI HAYO YOTE UNAYAJUA VYEMA KUWA:

• CHADEMA haina Rais, haina wabunge, haina madiwani wala haina wenyeviti wa vijiji/mitaa kwa kuwa ktk chaguzi zote hizo CCM iliharibu na kupora chaguzi zote na hivyo wakajitangaza wenyewe kwa mabavu kuwa ni washindi kwa 100%..!!

• Sasa pamoja na hayo, CHADEMA imekufa? Je, sio kwamba ndo tu kimekuwa chama kikubwa zaidi na kuwa tishio zaidi kuliko hata ilipokuwa na Wabunge na madiwani? Sasa hoja yako ya "kufa" unaitoa wapi? Mimi nakuambia, haitakufa, labda ufe wewe na CCM yenu...!!

NDO KUSEMA KWA HIYO, KWAMBA: Hii hoja yako ni "nonsense" haina msingi na inalenga kuchelewesha mabadiliko ya kweli tu...

NAKUSHAURI, acha woga na uchawa. Jiunge kwenye mapambano kuipambania nchi yako kutoka kwenye makucha na midomo ya manyang'au CCM....!!

KWA heri, usiku mwema...
 
Mheshimiwa Rais Samia..hebu rudisha moyo, ita Wapinzani Ikulu, ongea nao na fanyeni Marekebisho madogo ya Katiba kwa ajili ya Kupata Tume huru ya Uchaguzi isimamie uchaguzi wa haki wa 2025..

Usiwasikilize sana hao Wapambe, wengi wao wanaangalia Matumbo na familia zao, Refer yaliyomkuta Nyerere na Mkapa

Mama Tanzania ni MKUBWA kuliko CCM, CDM na ACT
 
Sasa kama dola ndio inachagua kiongozi kwanini tunaingiza watu kwenye vilema na vifo bila sababu.

Ngoja kwanza nichangie 5,000 ili viongozi hawa wasichoke.
Mungu aendelee kuwalinda na kuwabariki
 
Kina Mbowe, Dr. Slaa, Lowasa walishafanya sana hayo, Kujaribu kucheza na timu ambayo kuanzia refa mpaka Linesmen ni wa Tajiri, Guess what! Mpaka leo CCM inatamba!
 
Tafuta shughuli ya kueleweka ya kukuingizia kipato wewe

Kukodolea mimacho siasa tu utakufa kilofa wewe
 
Kina Mbowe, Dr. Slaa, Lowasa walishafanya sana hayo, Kujaribu kucheza na timu ambayo kuanzia refa mpaka Linesmen ni wa Tajiri, Guess what! Mpaka leo CCM inatamba!
Hayati Mwalimu Nyerere alishasema upinzani wa kweli utatoka ndani ya CCM siyo hao wachumia tumbo!
 
Ukizuia chafuzi hamna chafuzi njoo na ngojera ingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…