Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Sijawahi kuona umuhimu wa nafasi za wanyeviti wa wa serikali za mitaa katika mabadiliko au maendeleo ya nchi, kikubwa ninachokifahamu kama sehemu ya majukumu yao ni kugongea mihuri watu tu. Maamuzi yote muhimu huwa yanafanywa ngazi ya Halmashauri ya wilaya na kata.
Katika huu uchaguzi unaotarajiwa wa serikali za mitaa CHADEMA ni kama wapo mguu mmoja ndani mguu mmoja nje, wafanye uamuzi kamili na watoe msimamo wao kuhusu uchaguzi, kwa uhalisia hakuna umuhimu wa wao kushiriki, sioni faida yoyote itokanayo na wao kushriki huu uchaguzi, uchaguzi muhimu zaidi ni wa mwakani wa madiwani, ubunge na urais.