MTANZANIA620
Member
- Jun 20, 2023
- 65
- 81
Huu ni ushauri wa bure kabisa kwa uongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuelekea uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba, 2025 kwamba kwa viashiria vyote vya kitafiti na kiuchambuzi wa sayansi ya siasa na masuala ya kiuchaguzi siioni nafasi yao katika kushinda Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ikiwa walimudu kusimamisha wagombea asilimia 33 tu kote nchini kabla ya kudai kuondolewa ni tafsiri ya kukosekana uongozi imara kuanzia ngazi za chini hadi kanda.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Kwa kazi za maendeleo zilizofanyika na mwenendo huu tunaouona nashawishika kusema Rais aliopo Dkt Samia Suluhu Hassan atashinda tena kwa kishindo.
Sasa kwa kuwa tunahitaji wapinzani wazuri bungeni ni rai yangu chama hiki kielekeze nguvu kwenye udiwani na ubunge angalau waambulie wawakilishi wachache kule kuliko kupoteza muda na Urais halafu wakapigwa pakubwa sana.
Au wanajukwaa mnaonaje???