econonist
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 20,189
- 29,663
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo kimekuwa chama kikuu Cha upinzani Tanzania kwa muda wa miaka kumi na nne Sasa. Ni muda wa chama Cha CHADEMA kujifunza kutoka kwa kilichokuwa Cha kikuu Cha upinzani Msumbiji chama Cha RENAMO.
RENAMO kulikuwa ndio chama kikuu Cha upinzani kule Msumbiji. Na kwenye Uchaguzi wa Urais mwaka 1999 almanusra washinde uchaguzi ule baada ya mgombea wa FRELIMO Chisanno na mgombea wa RENAMO Alfonso Ndlakama kuachana kwa kura laki Mbili 200,000. Uchaguzi huo ulilalamikiwa kwa uwizi baada ya Tume ya Uchaguzi kutangaza kura laki 600,000 zimeharibika.
Hivyo basi RENAMO kimekuwa chama kikuu Cha upinzani kuanzia mwaka 1994 mpaka mwaka 2024. Kwa Sasa sio chama kikuu Cha upinzani tena baada ya kuibuka Kwa chama Cha PODEMOS Chini ya Venacio Mondlane.
Swali ni kwanini chama Cha PODEMOS kimeipiku RENAMO?
Sababu ya kwanza, RENAMO kiliishiwa nguvu baada ya kifo Cha Kiongozi wao wa muda mrefu Alfonzo Ndlakama mwaka 2018. Baada ya kifo Cha Ndhlakama hapa kuwa na kiongozi aliyeandaliwa kuchukua mikoba yake na Wala hapakuwepo kiongozi mwenye uwezo na ushawishi Kama wa Ndlakama. Hivyo kutokana na kukosa kiongozi mwenye ushawishi, RENAMO ilianza kupungua makali ingawa sio kwa Sana.
Sababu ya pili, RENAMO ilianza maridhiano na chama tawala Cha Msumbiji FRELIMO mwaka 2019 na kupelekea wafuasi kuanza kupiga kelele kwamba kimekuwa soft Sana kwa serikali, ilipelekea uungwaji mkono kupungua ingawa sio kwa Sana. Pia wafuasi wake wakabatiza hayo maridhiano FRENAMO. Ikimaanisha FRELIMO na RENAMO zimeungana.
Sababu ya Tatu, migogoro ya uongozi. Na hii ndio sababu kubwa iliyoizamisha RENAMO. Baada ya kifo Cha Alfonzo Ndlakama wa RENAMO mwaka 2018, Kijana mmoja alihamia RENAMO akitokea kwenye moja ya vyama vidogo vya upinzani vya Msumbiji. Kijana huyu anaitwa Venancio Mondlane. Venacio aliongeza chachu na mvuto kwa RENAMO na mwaka 2023 alikuwa na ushawishi kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa ambapo RENAMO ilinyakuwa karibia Asilimia hamsini ya viti. Shida ikaja kwamba kiongozi aliyemrithi Ndhlakama aliyeitwa Ussofu Made akaona kama nafasi yake inataka kubebwa na Venazio Mondlane hivyo mikwara ikaanza na mwishowe Venazio Mandlane akaamua kuhama chama Cha RENAMO na kuhamia chama Cha PODEMOS.
Mondlane alipohamia PODEMOS RENAMO wakachukulia poa wakijua wao namba mbili ya kwao. Ila Cha kushangaza Mondlane kaibuka wa pili kwa zaidi ya Asilimia thelathini za kura za urais na mgombea wa RENAMO Ussofu Made akapata Asilimia Tano tu za kura ya Urais.
Hivyo somo la RENAMO kwa CHADEMA ni kwamba ;
1. CHADEMA isibweteke na kuitwa chama kikuu Cha upinzani, wafuasi wake wanaweza kuhamia hata CHAUMMA na kujifanya chama kikuu Cha upinzani Kama kitazingua.
2. Pili, CHADEMA iachane na maridhiano yasiyokuwa na maana na CCM. Haya maridhiano sio afya kwa CHADEMA kisiasa. Achana na maridhiano pambana kwenye ulingo. RENAMO iliangushwa na maridhiano ya kila mara na FRELIMO.
Tatu, CHADEMA iandae kiongozi mwenye ushawishi atakaye mridhi Mwenyekiti wa Sasa Freeman Mbowe. Mbowe akistaafu au akakosa uwezo wa kuongoza CHADEMA inaweza kupata shida Kama haikuandaa mrithi. Kwa maana nyingine inatakiwa CHADEMA iwe na watu walioandaliwa kuwa wenyekiti wa chama Taifa. Ila tukilala na kubaki na misemo ya mwamba tuvushe matokeo yake yatakuwa ni machungu.
Nne, CHADEMA ije na strategies mpya za kuvutia wapiga kura wapya. Kwa Sasa wapiga kura wengi ni vijana. Hivyo CHADEMA inatakiwa kukaa Chini na kutafakari namna gani itawavutia Hawa vijana.
Tano, CHADEMA iweke wazi sera zake ambazo zitajulikana wazi kwa wananchi kuhusu elimu, uchumi, ulinzi, michezo, usawa wa kijinsia, ajira, kilimo nk.
From Econonist.