CHADEMA Ijiuanganishe kwenye kesi ya kupinga tuzo ya Dowans

CHADEMA Ijiuanganishe kwenye kesi ya kupinga tuzo ya Dowans

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
33,771
Reaction score
41,027
Zipo karibu taasisi 20 ambazo zimejiunganisha katika kupinga tuzo ya Dowans. Sijaelewa kwanini Chadema isiwe mojawapo. Nadhani litakuwa jambo jema kisheria na kisiasa kwa Chadema kuwa sehemu ya wanaopinga tuzo hiyo na kutoa msaada wowote wa kisheria. CCM na Kamati yake Kuu waliamua kukaa nchini na kuwaacha Watanzania wengine kufanya hivyo. Naamini ni vizuri kwa Chadema kujiunganisha katika kesi hiyo.

Vinginevyo endapo taasisi hizo zitashinda Chadema kama chama cha siasa hakiwezi kudai kuwa kilipinga waziwazi. Ni lazima kioneshe it can talk the talk as well as walk the walk.

Siyo katika kesi hii tu bali pia katika kesi nyingine za Kikatiba na zile zinazohusu haki za wananchi na kiraia. Najua yawezekana wanaogopa kuona kuwa kwa kufanya hivyo watakuwa wanaingiza siasa katika 'suala la kisheria'. Huu ni mtizamo wa makosa, siasa na sheria zimeingiliana sana kiasi cha kutoweza kuwa na moja pasipo kugusa jingine. Siasa na Sheria zina uhusiano wa kutegemeana - symbiotic relationship.
 
I fully support you, btw kwa nini umesema chadema na sio upinzani in general?
 
Sio kesi zote, hili la dowans nakubali, mengine they need be careful. Kuna taasisi za qanaccm kibao wasije wakaingizwa mjini. Kesi kama ina maslahi ya kimwamko kama dowans support 100pct, ila zingine avoid them
 
I fully support you, btw kwa nini umesema chadema na sio upinzani in general?

kwa sababu Chadema ndio chama kikuu cha upinzani nchini; na vyama vingine navyo vikitaka vinaweza kujiunga. Lakini kubwa ni kuwa hakuna chombo kinachounganisha upinzani wote Tanzania.
 
kwa sababu Chadema ndio chama kikuu cha upinzani nchini; na vyama vingine navyo vikitaka vinaweza kujiunga. Lakini kubwa ni kuwa hakuna chombo kinachounganisha upinzani wote Tanzania.

well eplained, easily understood!
 
kwa sababu Chadema ndio chama kikuu cha upinzani nchini; na vyama vingine navyo vikitaka vinaweza kujiunga. Lakini kubwa ni kuwa hakuna chombo kinachounganisha upinzani wote Tanzania.

Kwa hiyo vyama visivyo vikuu hili la Dowans haliwahusu? au hawana nafasi kwa sababu ni vyama vidogo?
 
Waberoya

Kama ilivyo ainishwa juu hatuna chombo kinacho unganisha vyama vya siasa hapa nchni, vyama vikuu vya upinzani kwasasa ni CDM ikifuatiwa na CUF lakini CFU tayari imeunda serikali na CCM kwahiyo ni CCM kwa simple logic ya hesabu sasa wewe unataka chama gani tena, vile vingine vilikwisha tangaza adharani kuwa wao ni Kikwete na Kikwete ni CCM kumbuka wakati wa uchaguzi wale jamaa wa ajabu ajabu mimi hata majina siyakumbuki, walitangaza bila kuficha kuwa wao ni CCM "B" chama kingine ni NCCR hao nadhani hawajui kama kuna kitu kinaitwa Dowans labda kama wewe umewai kusikia wakiongea chocho juu ya Richmond na Dowans ebu tusaidie, ehee maana husilaumu bila mizania, labda chukua nafasi utupatie wewe kwa maoni yako unashauri chama gani pia kijiunge ili tusiongelee hewa taja chama ambacho unadhani pia kijiunge!!!
 
Kwa hiyo vyama visivyo vikuu hili la Dowans haliwahusu? au hawana nafasi kwa sababu ni vyama vidogo?

Of course lina wahusu ndio maana kina Kafulila wanapeleka hoja Bungeni ambayo binafsi ninaamini Chadema watapaswa waiunge mkono.
 
funny_589.jpg
 
I dont know if you know what u r talking about.kwa hiyo chadema wapeleke hoja mahakamani ama wapeleke wakili ama gani?
 
I dont know if you know what u r talking about.kwa hiyo chadema wapeleke hoja mahakamani ama wapeleke wakili ama gani?

hujui maana ya kujiunga kwenye kesi ambayo una maslahi nayo hata kama walioileta mwanzoni ni watu wengine?
 
Mwanakijiji, Nkuunga mkono 100% Inabidi tuangalie jinsi yakushirikiana na taasisi nyingine ambazo zinatetea maslahi ya umma
 
Waberoya

Kama ilivyo ainishwa juu hatuna chombo kinacho unganisha vyama vya siasa hapa nchni, vyama vikuu vya upinzani kwasasa ni CDM ikifuatiwa na CUF lakini CFU tayari imeunda serikali na CCM kwahiyo ni CCM kwa simple logic ya hesabu sasa wewe unataka chama gani tena, vile vingine vilikwisha tangaza adharani kuwa wao ni Kikwete na Kikwete ni CCM kumbuka wakati wa uchaguzi wale jamaa wa ajabu ajabu mimi hata majina siyakumbuki, walitangaza bila kuficha kuwa wao ni CCM "B" chama kingine ni NCCR hao nadhani hawajui kama kuna kitu kinaitwa Dowans labda kama wewe umewai kusikia wakiongea chocho juu ya Richmond na Dowans ebu tusaidie, ehee maana husilaumu bila mizania, labda chukua nafasi utupatie wewe kwa maoni yako unashauri chama gani pia kijiunge ili tusiongelee hewa taja chama ambacho unadhani pia kijiunge!!!

Coalition governments or grands governments education is very important it seems neither chadema nor you know what is real coalition governments its advantages and disadvantages.
 
Nakubaliana na Mzee Mwanakijiji kwani CDM isipowaunga mkono vyama vya kijamii katika hili, watakuja hadi UVCCM/UWT/Wazee wa CCM na kuidakia kuwa ulikuwa ni ushindi wao kama ambavyo tumeona kwa bodi ya mikopo, Richmond na EPA wakati fulani hata CCM wanasema hii hoja yao kuwshughulikia mafisadi ni yao.

Lakini wananchi hawakuwamini kwa sababu idadi kubwa ya wahusika ni viongozi wa juu wa CCM.
 
Sasa hapo chadema mna usafi gani wa kusimamia DOWANS wakati mwenyekiti wenu mwenyewe katapeli fedha za wananchi huko NSSF. Kagoma kulipa, ni fisadi pia. Chama kinachoongozwa na fisadi nacho ni cha kifisadi. Chadema haina tofauti na CCM kwani ufisadi ni ufisadi hakuna fisadi nyangumi, papa wala dagaa, wote mafisadi tu.
 
Back
Top Bottom