Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Zipo karibu taasisi 20 ambazo zimejiunganisha katika kupinga tuzo ya Dowans. Sijaelewa kwanini Chadema isiwe mojawapo. Nadhani litakuwa jambo jema kisheria na kisiasa kwa Chadema kuwa sehemu ya wanaopinga tuzo hiyo na kutoa msaada wowote wa kisheria. CCM na Kamati yake Kuu waliamua kukaa nchini na kuwaacha Watanzania wengine kufanya hivyo. Naamini ni vizuri kwa Chadema kujiunganisha katika kesi hiyo.
Vinginevyo endapo taasisi hizo zitashinda Chadema kama chama cha siasa hakiwezi kudai kuwa kilipinga waziwazi. Ni lazima kioneshe it can talk the talk as well as walk the walk.
Siyo katika kesi hii tu bali pia katika kesi nyingine za Kikatiba na zile zinazohusu haki za wananchi na kiraia. Najua yawezekana wanaogopa kuona kuwa kwa kufanya hivyo watakuwa wanaingiza siasa katika 'suala la kisheria'. Huu ni mtizamo wa makosa, siasa na sheria zimeingiliana sana kiasi cha kutoweza kuwa na moja pasipo kugusa jingine. Siasa na Sheria zina uhusiano wa kutegemeana - symbiotic relationship.