Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Wanabodi,
Preamble: Chadema ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo jina tuu, ila uendeshaji wake ni wa kidikteta wa hali ya juu!. Katiba yake inavipengele vya kidikteta vinavyokwenda kinyume cha katiba ya nchi!, hii thread ni ya swali tuu, Hivi Chadema ilivyo, bado haijakabidhiwa nchi, inatoa maamuzi ya kiimla na udikiteta wa ajabu!, Jee Chadema ikikabidhiwa nchi hapo October 2015!, hakuna hatari ya uwezekano wa kuigeuza nchi yetu kuwa ni nchi ya utawala wa kidikteta wa ajabu?!. Hili ni swali tuu nauliza mimi Paskali
Tanzania ni nchi ya kidemokrasia inayofuatia misingi ya sheria, taratibu na kanuni kwa mujibu wa katiba ya JMT ya mwaka 1977.
Katiba ndio sheria mama, kila kitu kuhusiana na shughuli yoyote ndani ya JMT ni kwa mujibu wa Katiba!. Sheria yoyote, kanuni yoyote na taratibu yoyote, inayokwenda kinyume cha katiba ni batili!.
Katiba yetu imeweka utaratibu wa kutafuta haki ndani ya JMT ni kupitia mhimili wa mahakama. Vyama vyote vya siasa nchini, viko kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa!.
Kwenye sheria ya vyama hivyo, vyama kabla ya kusajiliwa, vinapaswa kuwasilisha katiba ya chama hicho na kupitiwa na wanasheria, ikukutwa iko sawa kwa mujibu wa katiba ya nchi, ndipo chama hicho hupewa usajili wa muda, kisha usajili wa kudumu!.
Hivyo ndivyo Chadema ilivyofanya ule mwaka 1992. Uliwasilisha katiba safi ya kidemokrasia yenye ukomo wa vipindi vya uongozi, kuwa ni vipindi viwili tuu, na wanachama wa Chadema walikuwa wako huru kufuata sheria za nchi!.
Mwaka 2006, Chadema ilifanya mabadiliko ya katiba, katika mabadiliko hayo, kile kipengele cha ukomo wa madaraka, kilinyofolewa kinyemela bila kujadiliwa popote!, hivyo marekebisho yaliwasilishwa kwa msajili wa vyama, hayakuwa tena na kipengele hicho cha ukomo, na kiliyeyuka bila muhtaasari wa kikao chochote kilichokijadili kipengele hicho!, hivyo marekebisho yaliyowasilishwa kwa msajili, kipengele hicho hakikuwepo, as if kimejadiliwa na kufikia uamuzi kiondolewe!, wakati kiukweli, hakikujadiliwa popote na yeyote bali kilinyofolewa tuu kinyemela, na katiba iliyowasilishwa mwaka 2006 hakikuwepo tena!.
Lengo la watungaji wa katiba mama ya Chadema, lilikuwa zuri, kwa uongozi wa Chadema kuwa na ukomo wa vipindi viwili vya miaka mitano mitano ili kupokezana vijiti ili kuzuia uongozi wa kisultani!. Mwaka huo wa 2006, wakaingia wajanja fulani!, wakakinyofoa kipengele kile, sasa uongozi wa Chadema hauna ukomo!. Yaani ni uongozi wa maisha mpaka kiongozi atakapoamua mwenyewe kuwa sasa amechoka!.
Mabadiliko hayo ya katiba ya Chadema ya mwaka 2006, pia yalipenyeza kipengele kinachomzuia mwanachama wa Chadema, kupeleka kesi yoyote mahakamani kukishitaki chama!. Hi ni kipengele cha kidikteta kuminya haki, na kiko kinyume cha katiba ya JMT, ambayo inasisitiza chombo pekee cha kutoa haki ndani ya JMT ni mahakama!. Kwa kipengele hiki, Chadema imejijengea himaya yake ya kidikteta ndani ya JMT ambayo haiutambui mhimili wa mahakama when it comes kwenye haki za wanachama wake, lakini when ni kuhusu haki za chama, ni mbio mahakamani!.
Mwanachama ukipeleka jambo lolote mahakamani, ukishindwa, hapo ndipo mwisho wa uanachama wako wa Chadema!.
Sasa nawauliza wanasheria na watetezi wa haki za binaadamu, hivi mwana Chama wa Chadema akikosa haki ndani ya chama chake akaitafute wapi?!.
Kama Chadema hivi tuu ni chama na bado hakijapewa dola, kimepenyeza vifungu vya kidikteta na kinyume cha katiba kwa kutoutambua mhimili wa mahakama, jee kikipewa nchi hiyo October, si ni kina uwezekano kabisa wa kuisimamisha kabisa katiba yenyewe na kutangaza utawala wa kiimla na kidikiteta jumla?!.
Hili la Katiba ya Chadema, nimewahi kulizungua hapa na nilishutumiwa sana na kunyooshewa vidole kuwa mimi ni CCM!.
Leo nimelikumbuka na kulizungumzia hapa, kufuatia mwanachama fulani wa Chadema, kupoteza uanachama wake, simply kwa kosa la kutafuta haki yake kwenye vyombo halali vya kutoa haki!.
Kwa udikiteta huu, na unaokwenda kinyume cha katiba ya nchi, enyi members wa jf wenye uelewa na sheria na katiba, ndio mnataka kutueleza nini kuhusiana na Chadema katika kufuata sheria taratibu na kanuni?!.
Nalirudia swali la msingi, Katiba ya Chadema ni "Unconstitutional" Jee ni Batili?. Na Chadema Ikipewa Nchi, Hakuna Hatari Kugeuka Dikteta?!.
Paskali
NB. Paskali ni mwanachama wa chama cha siasa!, ila pia ni an independent political commentator, asiyeegemea upande wowote, ambaye anazungumzia jambo lolote, kuhusu chama chochote. Sio mfuasi, mshabiki, wa kambi yoyote, au kiongozi yoyote, bali kama Mtanzania mwingine yoyote, kuna watu anaowakubali kijamii, kiuchumi na kisiasa, na siku ya kupiga kura, atapiga kura kuchagua kiongozi anayekupenda and not necessarily ni mgombea wa chama chake!.
Update 1.
Hii sio mara ya kwanza kulizungumzia hili la Katiba ya Chadema kunyofolewa kipengele hicho cha ukomo wa madaraka!. Nilipouliza mwanzo nilijibiwa hivi.
Suala hili lilifafanuliwa vyema na JJ Mnyika kama hivi.
Yaani Chadema imewasilisha marekebisho ya katiba yenye kifungu ambacho kimenyofolewa kinyemela, hakikujadiliwa popote, yaani katiba ya 2004 imeweka ukomo wa vipindi viwili vya uongozi, katiba ya 2006 ikavinyofoa kinyemela na sasa uongozi wa Chadema ni for life!. Excuse ya kuhalalisha uharamia huu, ni kuiita katiba ya 2006 ni katiba mpya!. Katika constitutional making process zote za kutunga katiba mpya, katiba ya zamani hujadiliwa kipengele kwa kipengele, na ndipo katiba mpya hutungwa. Hakuna mahali popote kipengele hiki cha ukomo wa kipindi cha uongozi, kilijadiliwa!, kwa lugha rahisi, kipengele hiki kili 'just vanish into thin air!.
Na kipengele kinachokiuka katiba ya JMT ni hiki.
x. CHADEMA itashughulikia matatizo ya viongozi nawanachama kwa kufuata taratibu zilizowekwa kwa mujibu wa Katiba ya Chama, wala hata siku moja haitashughulikia mambo kama hayo Mahakamani. Mwanachama atakayeshindwa kufuata taratibu na ngazi za Chama hatavumiliwa na atafukuzwa uanachama.

Mkuu MwanaHaki, kwanza asante kwa post hii, uzi huu unaelekea post 100, hii ndio posti ya kwanza kuijibu kwa sababu ndio post pekee iliyojikita kwenye subject matter!, na kufuatia post hii, nimeipeleka kule juu ili wenye kuhitaji kuujua ukweli, waujue ukweli, tuwaache hawa wajinga wajinga waendelee kupiga porojo!.Paskali
Unaidadisi Katiba ya CHADEMA? Basi, ilete tuijadili. Fanya scanning, tuoneshe Katiba ya awali na hiyo ya sasa ambayo unadai kwamba vipengele vimenyofolewa.
Wawakilishi wa wanachama waliokuwapo kwenye Mkutano Mkuu ndio walioipitisha. Unataka kutuambia kwamba wao ni watawala wa kiimla?
UMETUMWA?
Tunawajua watu wa aina yako. Baadae ukishindwa kujibu hoja unakaa kimya.
Haya, changamoto kwako. Tuletee hizo katiba unazodai zimechakachuliwa, tuuone ukweli. Wala usituletee soft copy. SCAN THE BLOODY THING. Weka hapa. Tutasoma wenyewe!
La sivyo, KAA KIMYA!
Hii sio mara ya kwanza kulizungumzia hili la Katiba ya Chadema kunyofolewa kipengele hicho cha ukomo wa madaraka!. Nilipouliza mwanzo nilijibiwa hivi.
Soma kwa makini hapo kwenye bold!, kisha tazama hapa kama ulivyoshauri, tena ni scanned copy na sio soft copy!WanaJF,
Pamoja na kuwa sitaki kuingilia mjadala katika hatua hii, naomba kuthibitisha kuwa:
I) Katibu Mkuu wa Chadema, kwa mujibu wa Katiba na Kanuni ya Chadema, ndiyo mhimili mkuu na mwenye jukumu la kutunza na kuhakikisha Katiba ya Chama inatunzwa.
2) Nataka kuwahakikishia wanachadema wote, kuwa nilikuwepo nimekuwa ndani ya Chadema kuanzia 1998 ambapo nilikuwa Makamu Mwenyekiti Bara, na baadaye 2003 Kaimu Katibu Mkuu, na hatimaye Katibu Mkuu. Hivyo nimeshiriki kikamilifu kuandaa Katiba ya 2004 na pia Katiba ya 2006 baada ya Rebranding ya Chama. Nataka niwahakikishie wanachadema, hakuna toleo lolote la Katiba ndani ya Chadema imeweka " muda wa Uongozi kuwa vipindi viwili tu", kuanzia Katiba aliyoiasisi Mzee Mtei na kupitishwa na Mkutano Mkuu, wala si ya 2004 au ya 2006. Kama kuna mtu anasema ilikuwepo na imeondolewa kinyemela, basi aonyeshe kifungu hicho kwenye Katiba yeyote ile, au miniti za kikao chochote kile.
Suala hili lilifafanuliwa vyema na JJ Mnyika kama hivi.
Pasco nimesoma mjadala ulioanzisha na majibu ya Dr Slaa. Nimekubaliana na katibu mkuu kuna marekebisho kwenye majibu yake ya awali, katiba ya mwaka 2004 iliondolewe katika orodha ya katiba alizozitaja. Suala la kwamba kuna kipengele kiliondolewa kinyemela halina ukweli, na kilichofanyika 2006 ni kuandika katiba upya kama ambavyo nimeeleza kwenye majibu hayo.. Mjadala mwema. JJ
Majibu ya Mnyika anasema 2006 walitunga katiba mpya!, taarifa iliyopo ofisi ya Msajili sio katiba mpya bali ni marekebisho ya Katiba!.Pasco, Pamoja na marekebisho niliyoeleza kuhusu majibu ya Dr Slaa kwamba katiba ya 2004 iondolewe kwenye orodha kama nilivyochangia hapo awali. Katiba ya mwaka 2004 haiwezi kuwa ushahidi wa hayo madai yasiyokuwa ya kweli. Katiba ya mwaka 2004 mimi ninayo hapa nilipo, kwenye kifungu cha 6.3.2 kina kipengele cha 'muda usiozidi vipindi viwili katika cheo kimoja kwa ngazi moja'. Hata hivyo, huu sio ushahidi wa kwamba kipengele hiki kimeondolewa 'kinyemela'. Hii ni kwa sababu tatu; Mosi, 2006 hatukuwa tunafanya marekebisho ya katiba kwa maana ya kuondoa au kuacha kifungu cha katiba ya mwaka 2004. Tuliandika katiba upya, ndio maana tarehe 13 Agosti 2006 pale PTA tukafanya uzinduzi wa katiba mpya ya CHADEMA. Kwenye mchakato wa kukusanya maoni ya katiba mpya na hatimaye maandalizi ya rasimu ya katiba mpya, hili suala halikuingia kabisa. Halikupitishwa kwenye mapendekezo ya sekretariati, kamati kuu, baraza kuu na hata mkutano mkuu kwa kadiri ya kumbukumbu zangu. Hivyo huwezi kuzungumzia 'kuondoa kinyemela' kipengele ambacho hakikuingia.. JJ