Elections 2015 CHADEMA ikipewa Nchi, Oktoba 2015, Hakuna Hatari Kugeuka Utawala wa Kidikteta? Nauliza Tuu!

Elections 2015 CHADEMA ikipewa Nchi, Oktoba 2015, Hakuna Hatari Kugeuka Utawala wa Kidikteta? Nauliza Tuu!

Ukiwa mwanachama wa FIFA huruhusiwi kupeleka shauri lolote linarohusu FA au mpira mahakamani.

Ina maana wewe Pasco una AKILI nyingi SANA kuliko FIFA walioweka kipengele hicho.

Sasa kuna shida gani CHADEMA kama chama kushughulikia mambo yake kwa kufuata katiba yao bila kupelekana kwenye mahakama za serikali

You're Hypocrisy of highest level!
 
Chadema ni chama kizuri na kina malengo mazuri kama kinavojinadi kila kukicha ila kwa suala la kupewa nchi bado sana,dhamana ya nchi sio suala rahisi kama tunavofikiria,chadema bado haina hazina ya viongozi kuendesha nchi jamani tuwe wa kweli, mfano mdogo tu,endapo chadema ikishika nchi baraza la mawaziri litakuaje?
 
CHADEMA siyo kituo cha kulelea mafisadi na wasaliti,wote hao wataendelea kukumbana na mkono wa sheria hizi hizi zilizopo.

CHADEMA watakachokifanya baada ya kuchaguliwa ni kuzisimamia sheria,ziendelelee kufanya kazi kwa makali yaleyale bila kujali makunyanzi ya mtu yeyote.
 
Chama lazima kiwe na nguvu kuliko mwanachama. Uimara wa CDM kwa sasa ndo mwisho wa matatizo ya Watanzania. Lakini nikukumbushe kwamba kwa uchaguzi ujao Chadema haitasimama pekeyake, inaunganisha nguvu na vyama vingine vya upinzani hili unalijua sina haja yakupoteza muda kuelezea. Hivyo oktoba 2015 upinzani utakuwa chama tawala na ccm itakuwa chama cha upinzani au ccm itakufa kabisa.
 
Pasco
Kwa hiyo kwa ushauri wako wezi wakiiba warudishe pesa taratibu

mwenye utovu wa nidhamu achekelewe ati
 
Last edited by a moderator:
Mbowe alinyofoa kipengele cha katiba ili awe mwenyekiti wa milele mbona hajafukuzwa?
kamlalamikie hakimu
kama unadhani hakimu hatakupendelea kwa sababu ya dini yako mwambie KITILYA NA MWIGAMBA wakalalamike hakimu/jaji atawaelewa kwa sababu ya dini zao
 
Chadema ni chama kizuri na kina malengo mazuri kama kinavojinadi kila kukicha ila kwa suala la kupewa nchi bado sana,dhamana ya nchi sio suala rahisi kama tunavofikiria,chadema bado haina hazina ya viongozi kuendesha nchi jamani tuwe wa kweli, mfano mdogo tu,endapo chadema ikishika nchi baraza la mawaziri litakuaje?

Wewe lazima utakuwa ni mzee maana naona umeshiba propaganda full. Uchaguzi utakaowapa cdm nchi ni hakika utakuwa na wabunge wengi sana, kutoka hao wabunge wanahitaji mawaziri chini ya 20 tu kuunda serekali. Sasa wewe unaona watapata nchi lakini watakuwa na wabunge hawahawa waliopo sasa huoni uzee wa mawazo yako?
 
Kaka msomi wa kitivo cha sheria cha Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam, natumai hapo chuoni ulisoma pia mambo ya mantiki.

Kwa mtaji huo, je, hilo swali lako lina mantiki kweli?

"Katiba ya Chadema ni "Unconstitutional" Jee ni Batili?"


Duuh!

Hahahahaha. Mhhhhhh. Lugha.
 
.....
x. CHADEMA itashughulikia matatizo ya viongozi nawanachama kwa kufuata taratibu zilizowekwa kwa mujibu wa Katiba ya Chama, wala hata siku moja haitashughulikia mambo kama hayo Mahakamani. Mwanachama atakayeshindwa kufuata taratibu na ngazi za Chama hatavumiliwa na atafukuzwa uanachama.

.....
Udhurungi/violet: hivi kiambata hicho ni 'ha' ama 'a'....? Ninavyojua kiambata 'ha' kikitagulia mzizi wa kitenzi/tendo umaanisha kanusho/kukataa. Sasa kwa jinsi kilivyotumika hapo hakipotoshi maana halisi ya kifungu hicho cha katiba ya CHADEMA?
 
Kwani uongo? Said Arfi kwa nini aliachia unaibu mwenyekiti Chadema?
aliachia kwa sababu ALICHEZA DILI ILI PINDA APITE BILA KUPINGWA.......au kama vipi dini yake mbaya

ZZK alitaka kujificha nyuma ya kichaka cha dini aiharibu cdm na sasa wanachama tumemchoka aende na aende na wa dini yake wooote waondoke kama wanaona kisa cha zitto ni dini

WALIFUKUZWA WATATU:HAO WENGINE NAO WALIPONZWA NA NINI???ni dini zao.

aondoke zake zzk, ziondoke na pumba zake
 
Wanabodi!.

Preamble: Chadema ni Chama cha Kimokrasia na Maendeleo jina tuu, ila uendeshaji wake ni wa kidikteta wa hali ya juu!. Katiba yake inavipengele vya kidikteta vinavyokwenda kinyume cha katiba ya nchi!,........................

Sijui hizi Thrd munazianzusha kwasbabu gani maana siamini kwamba kuna mtu anaweza kunituma kazi ya aina hii nikaikubali. Bila kujali uhasama wako unaoonyesha kwa CDM, hebu tuambie, nchi inaitwa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, je muungano upo?
 
Nilitaraji Pasco kuja na uzi kama huu, nilichokigundua kwako wewe ni mmoja ya watu ambao bila kujijua ni wale ambao mnapenda sheria zifanye kazi kutokana na vionjo vya watawala na sio sheria. Umesema kweli kwamba katiba ya cdm kuna kifungu kilichomolewa kinyemela na watu wachache mwaka 2006 bila muhtasari kama inavyopaswa, hilo ni kosa la cdm ama msajili wa vyama? Huko kwenye vyama kuna katiba, na iwapo hukubaliani na katiba ya chama husika hakuna anayekufunga miguu. Hamia chama kingine ama ukiona hakuna chenye katiba nzuri basi anzisha chakwako.

Naona hasira yako inafanana na wanaccm wengi kwa leo kuhusu hali iliyoikuta cdm kuhusu mwanachama wake mmoja. Lakini ki ukweli mpaka kufikia leo ni kama tayari hakuwa mwanachama zaidi ya kwamba alikuwa na kadi. Kama yeye huyo unayeona kaonewa na wakati yeye mwenyewe alikuwa hawakubali wenziwe kwamba yeye ni nyota sana, anaweza kwenda pengine kwani hakuna aliyeshika nyota yake. Achia chama kinachoweza kuchukua maamuzi hata kama hayatawafurahisha walio wengi lakini mpaka sasa kwa mujibu wa katiba iliyo kwa msajili ndio iliyotumika.

Nikushauri Pasco, nadhani wewe unaweza kukutana na huyo aliyefukuzwa, mimi namkubali sana kutokana na uwezo wake kwani sina shaka nao. Sisi wengi bado tunaona uwezo na mchango wake, lakini sioni ulazima wa mchango wake autoe akiwa ndani ya cdm wakati hana maelewano mazuri na wenzie, achia mbali ameonewa sijui katiba ya udikteta na nini. Sasa ndio wakati wa yeye kuonyesha ubora wake huko aendako kwani hakuna mchaga, sijui mkristo wa kumbana. Kuliko wewe kuja na post ya jazba ili yeye awe ndani ya cdm. Mwache kijana aende pengine kwani aliona nafasi yake inabanwa sasa aende akachague nafasi huko aendako ili kama hao cdm wanaaibika waaibike vizuri kwa kumkosa yeye. Vinginevyo ndugu yangu unajiaibisha na kujipunguzia heshima yako kwa kumlazimishia mtu mahali asipopata nafasi, au wewe una mpango wa kuua kipaji chake ndo maana unataka abaki cdm?
 
Back
Top Bottom