Elections 2015 CHADEMA ikipewa Nchi, Oktoba 2015, Hakuna Hatari Kugeuka Utawala wa Kidikteta? Nauliza Tuu!

Elections 2015 CHADEMA ikipewa Nchi, Oktoba 2015, Hakuna Hatari Kugeuka Utawala wa Kidikteta? Nauliza Tuu!

Wiki hii walianza na Halid Kagenzi,leo Zitto
 
Last edited by a moderator:
CHADEMA ni chama kinachoongozwa na utashi wa wateule wachache ambao ukithubutu kuwapinga kimtazamo, utaishia pabaya. Yalianzia kwa Chache Wangwe, leo yamemkuta Zitto.

Kwa mtaji huu,hili genge la wateule wachache wajionao bila wao CHADEMA hakipo; nafasi ya CHADEMA kukabidhiwa Ikulu inazidi kuwa finyu. Hiki hakikuwa kipindi muafaka cha kufukuzana kwa super sonic speed pasipo kusubiri angalau nakala ya hukumu itoke, halafu kiitishwe kikao ndipo maamuzi yatoke.

Kwa maamuzi yaliyotolewa na utaratibu uliofuatwa, moja kwa moja ishara tosha ni anguko la UKAWA. Poleni UKAWA kwa kuwaamini CHADEMA ambao hawana busara katika kufikia maamuzi.
 
Ubabe,ubinafsi,chuki,kutopenda mtazamo tofauti kunaua Demokrasia ndani ya Chadema.Nashauri wabadili jina la chama.
 
Alianza ishu ya ukomo wa uongozi, nikaguna baada ya kuhisi ukakasi wa kipengele cha kutokuwa na ukomo wa uongozi. Nilijifariji nikidhani labda viongozi na wanachama walipitiwa kwenye hicho kipengele. Leo hii limekuja suala la mahakama, kwa kiasi fulani nilishindwa kumwelewa Lissu aliposema eti mwanachama hapaswi kwenda mahakamani, nikaguna ila kama kawaida yangu nikatafuta katiba ya Chadema, kiukweli nadiriki kusema neno DEMOKRASIA halipaswi kutumiwa na Chadema hata kidogo. Hata jina la chama tu lingebadilishwa. Huwezi kuhubiri demokrasia wakati unazuia watu kwenda mahakamani. Hii si sawa hata kidogo. Kuna baadhi ya watu wanasema eti hata TFF hupaswi kwenda mahakamani. Wanakosea, TFF au mpira wa miguu wana mahakama zao na wanasheria waliosomea sheria za mpira wa miguu. Kinachokatazwa ni kwenda kwenye hizi makahakama ambazo si za michezo, ila kwenda mahakama ya mpira wa miguu inaruhusiwa. Sasa Chadema wamekuwa wao ndio mahakama, wao ndio majaji, wao ndio vyombo vya dola. Katiba wameiweka kiasi kwamba mwanachama hana haki yoyote ile pindi linapokuja suala laa kutafuta suluhu. Sidhani kama demokrasia ipo namna hii. Wengi leo wanashangailia labda kwa sababu hawampendi Zitto, ni sawa, ni haki yao. Lakini ifike mahali tuangalie haya mapungufu ya katiba kwa mapana zaidi.

Mkuu nafikiri kuna kitu unakikosa juu ya hasa katazo la taasisi kuweka iwe katika katiba ya taasisi husika au hata kama ni Agreement. Ninachokifahamu sababu hasa ya kuiondoa mahakama kushughulikia mambo ya chama au taasisi at some stage ni ili kuipa taasisi au chama na ofcourse mtuhumiwa fursa ya suala lake kushughulikiwa na chama

Na kama mtuhumiwa baada ya maamuzi ya chama kutoka hajaridhika nayo, still fursa ipo ya kwenda mahakamani.

Lakini haiwe haiwezekana each and every thing concerned with the political party or any other instiute to be dealt with at first instance by the court. Nafikiri hii siyo sawa.
 
Ukikosana na mwajiri wako,hata kama una haki, huwezi kukimbilia mahakamani. Utafuata some sort of procedures, ikiwa ni pamoja remedy zilizopo kwenye kampuni husika, ikikosekana utaenda usuluhishi, ikishindikana ndipo hapo utaenda mahakamani. Hizi ni hatua tuu ili kuongeza ufanisi katika taasisi na si kila mtu mtu ajisikiapo kukimbilia mahakamani.

Assume wanachama laki moja wamekwenda kufungua kesi mahakamani, na kila mtu na kesi yake na dai lake. How can you attend this? mwaka mzima si mtakuwa mnadili na kesi mahakamani kila uchao?
 
Dah!mtoa mada unaweza kuwaina watanzania ni wajinga kwa kudhani waweza kuwalaghai kwa hoja zako za kichoko lakuni kaa ukijua watanzania wanaelewa wanachokifanya na wanafuatilia mambo zaidi yako.kama katiba ya CHADEMA imekiuka katiba ya nchi kwa maana haina kipengele cha ukomo wa madaraka na msajili akaikubali sasa alie kiuka katiba ya nchi hapo nani ni msajili alie wekwa na ccm au chadema.acha kuandika upuzi kama umekalia kitu chenye ncha kali..
 
Acheni kuchanganya mambo, Zitto alikataa kujadiliwa na chama na kukimbilia mahakamani, na katiba ya chama inamwambia mwanachama akikipeleka chama mahakamani? Atakuwa amejifuta uwanachama yeye mwenyewe shida iko wapi hapo?someni katiba ya chama, Albert sheria hajui,
 
Kwani unafikiri hajui kua chadema hakimzuii mtu kwenda nahakanani lakini ukienda shinda kesi.ukishindwa umejitoa nwonyeqe chanani..alafu mwambie huyo snitch kua wanaowawajibisha wanachama na wabachama kupitia katiba halali..
 
Chadema hakuna ubabe hakuna chuki wala ubinafsi..huwezi kuwaelewa chadema mana hata we mwenyewe hujielewi
 
You're killing me Pasco!

Kama unalala na kuamka ukidhani CHADEMA watakabidhiwa nchi hapo October 2015, utakuwa ni kati ya watu wenye daydream.

Kwa CHADEMA hii, haitatokea.
Unafikiri Nchi itapewa tena hao maharamia ya kisomali kama Katibu wenu?
 
Pasco

Unaidadisi Katiba ya CHADEMA? Basi, ilete tuijadili. Fanya scanning, tuoneshe Katiba ya awali na hiyo ya sasa ambayo unadai kwamba vipengele vimenyofolewa.

Wawakilishi wa wanachama waliokuwapo kwenye Mkutano Mkuu ndio walioipitisha. Unataka kutuambia kwamba wao ni watawala wa kiimla?

UMETUMWA?

Tunawajua watu wa aina yako. Baadae ukishindwa kujibu hoja unakaa kimya.

Haya, changamoto kwako. Tuletee hizo katiba unazodai zimechakachuliwa, tuuone ukweli. Wala usituletee soft copy. SCAN THE BLOODY THING. Weka hapa. Tutasoma wenyewe!

La sivyo, KAA KIMYA!
 
Last edited by a moderator:
Pasco

Pole kwa yaliyomsibu rafiki yako Zitto

Sisi wanachama wa Chadema tumeridhika 100% na Mabadiliko ya Katiba ya 2006.

Pia kwa sasa hatuoni mbadala wa Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa.Tunawaomba walau waongoze chama hiki kwa miaka 10 ijayo zaidi.

Pia nchi hii ni ya mfumo wa vyama vingi asiyeridhika na Chadema aanzishe chama chake kama Zitto alivyoanzisha ACT
 
Last edited by a moderator:
You're killing me Pasco!

Kama unalala na kuamka ukidhani CHADEMA watakabidhiwa nchi hapo October 2015, utakuwa ni kati ya watu wenye daydream.

Kwa CHADEMA hii, haitatokea.

Kwa hiyo nchi hii unataka wapewe majangili kama hilo Jangili la kisomali unalolijua?
 
Chadema hakuna ubabe hakuna chuki wala ubinafsi..huwezi kuwaelewa chadema mana hata we mwenyewe hujielewi
 
Chadema ni chama cha ajabu sana sijawahi kuona wala kusikia chadema wakifanya jambo kwa mujibu wa sheria ila ni ubabe na ugandamizaji kwa wanaowaongoza.
 
Hawa ni madikteta wa kutupwa kwan mabaya ya viongoz wao n halali,ya wanachama haramu.
 
Back
Top Bottom