Elections 2015 CHADEMA ikipewa Nchi, Oktoba 2015, Hakuna Hatari Kugeuka Utawala wa Kidikteta? Nauliza Tuu!

Elections 2015 CHADEMA ikipewa Nchi, Oktoba 2015, Hakuna Hatari Kugeuka Utawala wa Kidikteta? Nauliza Tuu!



Pasco.


NB. Kwa msisitizo: Pasco wa jf, sio mwanachama wa chama chochote cha siasa!, hajawahi kujiunga na chama chochote cha siasa, wala hana mpango wowote wa kujiunga na chama chochote, kwa lengo la lolote, bali ni political commentator, ambaye anazungumzia jambo lolote, kuhusu chama chochote. Sio mfuasi, mshabiki, wa kambi yoyote, au kiongozi yoyote, bali kama Mtanzania mwingine yoyote, kuna watu anaowakubali kijamii, kiuchumi na kisiasa, na siku ya kupiga kura, atapiga kura kuchagua kiongozi.

Mwanangu Paskali, poleni sana kwa kifo cha mpambanaji mwenzenu na hasa ambaye angekuwa ngome yenu kuu kwa Mzee wetu Lowasa ambaye wewe ni kambi yake ange wawezesha kuufikia ukuu wa nchi mliotamani sana mzee wetu Edo aupate, sinashaka nyuma ya kifo hiki kuna wachawi ambao wanaendelea kuwa loga. Kifo hiki cha kapteni wetu Komba kwa kweli ni pigo kuu kwa kambi yenu. Tangu Kapten aseme kama Edo anafaa zaidi aliandamwa na mikosi na hatimaye waxhawi walifanikiwa.
Pili mwanangu Je bado kambi yenu ina nguvu na hizo ndoto zitafikiwa? Naona kambi inayoungwa na mfalme na wengineo wanazidi kuwaporomosha, sasa inaonekana hakuna jiwe litakao salia juu ya lingine.
Au kwa maelezo niliyonukulu hapo juu na wewe umemtema? naomba nifahamishe hata kama siyo juu ya mada yako. Na kwa mada yako naona kama unampango wa kujiunga na CDM, binti mwanana ambaye wenye gere wamekuambia hafai lakini rohoni unapenda sana.
 
PASCO NI MFUASI WA LOWASSA ZITTO NI MFUASI WA LOWASSA ZITTO kaachwa na CCM aadhibike kwa kuwa ni mfuasi wa lowassa
Haha...wanajifanya kutamani kuwa wacheza chess kwa akili za kasuku za kurudia kila sauti.Ndio maana wanarudia matusi.Ndivyo inavyokuwa kambi ya wapiga dili kichaa.Anytime wanaweza thurika kwa ukubwa wa dili wanazoziingia.
 
Pasco umetoka povu sana nchi yetu inhitaji viongozi wenye element za udiketa tusingwe wahi kusikia milion kumi za kununua mboga wala nyoka mwenye makengez wat cdm did whether is unconstitutional or nt let them do tanzania inahitaji viongozi kama haw wanareact mapema then it's over tuko nyuma sana hizi porojo za watu kama pasco ndo zinaidumaza hii nchi
 
Pasco
Kwa jinsi unavyojikanyaga, inaonekana umechomwa moyoni kwa uamuzi huu wa mahakama; na hitimisho lake kutoka CDM. Pole sana.
 
Pasco

Unaidadisi Katiba ya CHADEMA? Basi, ilete tuijadili. Fanya scanning, tuoneshe Katiba ya awali na hiyo ya sasa ambayo unadai kwamba vipengele vimenyofolewa.

Wawakilishi wa wanachama waliokuwapo kwenye Mkutano Mkuu ndio walioipitisha. Unataka kutuambia kwamba wao ni watawala wa kiimla?

UMETUMWA?

Tunawajua watu wa aina yako. Baadae ukishindwa kujibu hoja unakaa kimya.

Haya, changamoto kwako. Tuletee hizo katiba unazodai zimechakachuliwa, tuuone ukweli. Wala usituletee soft copy. SCAN THE BLOODY THING. Weka hapa. Tutasoma wenyewe!

La sivyo, KAA KIMYA!
Mkuu MwanaHaki, kwanza asante kwa post hii, uzi huu unaelekea post 100, hii ndio posti ya kwanza kuijibu kwa sababu ndio post pekee iliyojikita kwenye subject matter!, na kufuatia post hii, nimeipeleka kule juu ili wenye kuhitaji kuujua ukweli, waujue ukweli, tuwaache hawa wajinga wajinga waendelee kupiga porojo!.

Asante.

Pasco
 
Pasco
ccm ipo madarakani na sasa ni zaidi ya miaka 30 je huu si udikteta????
 
Last edited by a moderator:
ITAUWA WATU WENGI SANA.
just imagine uwe na waziri kama sugu halafu ujifanye kumchimbachimba,kama hajatuma watu wakakunyonga ama kukupiga shaba.
lema awe waziri umletee vyoko,utaokotwa mtaloni minus your head.

Ulimboka, Mvungi, Prof. Mwaikusa, Kubenea, Abisolom, Mwangosi, Kombe, Muuza magazeti Morogoro, Mauwaji ya Arusha, Oparesheni Tokomeza watu badala ya Majangili ambao wengine ni viongozi ndani ya ccm na mengine mengi. Je Lema na Rais wa Mbeya (Sugu) ni mawaziri? Kenge we!
 
Mkuu MwanaHaki, kwanza asante kwa post hii, uzi huu unaelekea post 100, hii ndio posti ya kwanza kuijibu kwa sababu ndio post pekee iliyojikita kwenye subject matter!, na kufuatia post hii, nimeipeleka kule juu ili wenye kuhitaji kuujua ukweli, waujue ukweli, tuwaache hawa wajinga wajinga waendelee kupiga porojo!.

Asante.

Pasco

Sijasoma Katiba ya CHADEMA, ila nitaisoma. Tuwekee version zote mbili, ile ya awali, na hiyo mpya. Nataka kujua iwapo kweli usemayo yametokea, ili iwe changamoto kwetu sote!
 
You're killing me Pasco!

Kama unalala na kuamka ukidhani CHADEMA watakabidhiwa nchi hapo October 2015, utakuwa ni kati ya watu wenye daydream.

Kwa CHADEMA hii, haitatokea.

Sasa huu ndiyo udictator ............ Kwa hiyo CCM ikishindwa haitakabidhi nchi siyo? It will happen, whether this year, next year or 2020, it will happen!! The history never lied before!!
 
Wanabodi!.

Preamble: Chadema ni Chama cha Kimokrasia na Maendeleo jina tuu, ila uendeshaji wake ni wa kidikteta wa hali ya juu!. Katiba yake inavipengele vya kidikteta vinavyokwenda kinyume cha katiba ya nchi!, hii thread ni ya swali tuu, Hivi Chadema ilivyo, bado haijakabidhiwa nchi, inatoa maamuzi ya kiimla Jee Chadema Ikikabidhiwa Nchi hapo October 2015!, Hakuna Hatari ya Uwezekano wa Kuigeuza nchi yetu kuwa ni nchi ya Utawala wa Kidikteta?!. Pasco

Tanzania ni nchi ya kidemokrasia inayofuatia misingi ya sheria, taratibu na kanuni kwa mujibu wa katiba ya JMT ya mwaka 1977.

Katiba ndio sheria mama, kila kitu kuhusiana na shughuli yoyote ndani ya JMT ni kwa mujibu wa Katiba!. Sheria yoyote, kanuni yoyote na taratibu yoyote, inayokwenda kinyume cha katiba ni batili!.

Katiba yetu imeweka utaratibu wa kutafuta haki ndani ya JMT ni kupitia mhimili wa mahakama. Vyama vyote vya siasa nchini, viko kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa!.

Kwenye sheria ya vyama hivyo, vyama kabla ya kusajiliwa, vinapaswa kuwasilisha katiba ya chama hicho na kupitiwa na wanasheria, ikukutwa iko sawa kwa mujibu wa katiba ya nchi, ndipo chama hicho hupewa usajili wa muda, kisha usajili wa kudumu!.

Hivyo ndivyo Chadema ilivyofanya ule mwaka 1992. Uliwasilisha katiba safi ya kidemokrasia yenye ukomo wa vipindi vya uongozi, kuwa ni vipindi viwili tuu, na wanachama wa Chadema walikuwa wako huru kufuata sheria za nchi!.

Mwaka 2006, Chadema ilifanya mabadiliko ya katiba, katika mabadiliko hayo, kile kipengele cha ukomo wa madaraka, kilinyofolewa kinyemela bila kujadiliwa popote!, hivyo marekebisho yaliwasilishwa kwa msajili wa vyama, hayakuwa tena na kipengele hicho cha ukomo, na kiliyeyuka bila muhtaasari wa kikao chochote kilichokijadili kipengele hicho!, hivyo marekebisho yaliyowasilishwa kwa msajili, kipengele hicho hakikuwepo, as if kimejadiliwa na kufikia uamuzi kiondolewe!, wakati kiukweli, hakikujadiliwa popote na yeyote bali kilinyofolewa tuu kinyemela, na katiba iliyowasilishwa mwaka 2006 hakikuwepo tena!.

Lengo la watungaji wa katiba mama ya Chadema, lilikuwa zuri, kwa uongozi wa Chadema kuwa na ukomo wa vipindi viwili vya miaka mitano mitano ili kupokezana vijiti ili kuzuia uongozi wa kisultani!. Mwaka huo wa 2006, wakaingia wajanja fulani!, wakakinyofoa kipengele kile, sasa uongozi wa Chadema hauna ukomo!. Yaani ni uongozi wa maisha mpaka kiongozi atakapoamua mwenyewe kuwa sasa amechoka!.

Mabadiliko hayo ya katiba ya Chadema ya mwaka 2006, pia yalipenyeza kipengele kinachomzuia mwanachama wa Chadema, kupeleka kesi yoyote mahakamani kukishitaki chama!. Hi ni kipengele cha kidikteta kuminya haki, na kiko kinyume cha katiba ya JMT, ambayo inasisitiza chombo pekee cha kutoa haki ndani ya JMT ni mahakama!. Kwa kipengele hiki, Chadema imejijengea himaya u ya kidikteta ndani ya JMT ambayo haiutambui mhimili wa mahakama!. Na mwanachama ukipeleka jambo lolote , ukishindwa, hapo ndipo mwisho wa uanachama wako wa Chadema!.

Sasa nawauliza wanasheria na watetezi wa haki za binaadamu, hivi mwana Chama wa Chadema akikosa haki ndani ya chama chake akaitafute wapi?!.

Kama Chadema hivi tuu ni chama na bado hakijapewa dola, kimepenyeza vifungu vya kidikteta na kinyume cha katiba kwa kutoutambua mhimili wa mahakama, jee kikipewa nchi hiyo October, si ni kina uwezekano kabisa wa kuisimamisha kabisa katiba yenyewe na kutangaza utawala wa kiimla na kidikiteta jumla?!.

Hili la Katiba ya Chadema, nimewahi kulizungua hapa na nilishutumiwa sana na kunyooshewa vidole kuwa mimi ni CCM!.

Leo nimelikumbuka na kulizungumzia hapa, kufuatia mwanachama fulani wa Chadema, kupoteza uanachama wake, simply kwa kosa la kutafuta haki yake kwenye vyombo halali vya kutoa haki!.

Kwa udikiteta huu, na unaokwenda kinyume cha katiba ya nchi, enyi members wa jf wenye uelewa na sheria na katiba, ndio mnataka kutueleza ni i kuhusiana na Chadema katika kufuata sheria taratibu na kanuni?!.

Nalirudia swali la msingi, Katiba ya Chadema ni "Unconstitutional" Jee ni Batili?. Na Chadema Ikipewa Nchi, Hakuna Hatari Kugeuka Dikteta?!.

Pasco.

NB. Kwa msisitizo: Pasco wa jf, sio mwanachama wa chama chochote cha siasa!, hajawahi kujiunga na chama chochote cha siasa, wala hana mpango wowote wa kujiunga na chama chochote, kwa lengo la lolote, bali ni political commentator, ambaye anazungumzia jambo lolote, kuhusu chama chochote. Sio mfuasi, mshabiki, wa kambi yoyote, au kiongozi yoyote, bali kama Mtanzania mwingine yoyote, kuna watu anaowakubali kijamii, kiuchumi na kisiasa, na siku ya kupiga kura, atapiga kura kuchagua kiongozi.

Update 1.

Mkuu MwanaHaki, kwanza asante kwa post hii, uzi huu unaelekea post 100, hii ndio posti ya kwanza kuijibu kwa sababu ndio post pekee iliyojikita kwenye subject matter!, na kufuatia post hii, nimeipeleka kule juu ili wenye kuhitaji kuujua ukweli, waujue ukweli, tuwaache hawa wajinga wajinga waendelee kupiga porojo!.

Hii sio mara ya kwanza kulizungumzia hili la Katiba ya Chadema kunyofolewa kipengele hicho cha ukomo wa madaraka!. Nilipouliza mwanzo nilijibiwa hivi.


Soma kwa makini hapo kwenye bold!, kisha tazama hapa kama ulivyoshauri, tena ni scanned copy na sio soft copy!
attachment.php

Suala hili lilifafanuliwa vyema na JJ Mnyika kama hivi.

Majibu ya Mnyika anasema 2006 walitunga katiba mpya!, taarifa iliyopo ofisi ya Msajili sio katiba mpya bali ni marekebisho ya Katiba!.

Yaani Chadema imewasilisha marekebisho ya katiba yenye kifungu ambacho kimenyofolewa kinyemela, hakikujadiliwa popote, yaani katiba ya 2004 imeweka ukomo wa vipindi viwili vya uongozi, katiba ya 2006 ikavinyofoa kinyemela na sasa uongozi wa Chadema ni for life!. Excuse ya kuhalalisha uharamia huu, ni kuiita katiba ya 2006 ni katiba mpya!. Katika constitutional making process zote za kutunga katiba mpya, katiba ya zamani hujadiliwa kipengele kwa kipengele, na ndipo katiba mpya hutungwa. Hakuna mahali popote kipengele hiki cha ukomo wa kipindi cha uongozi, kilijadiliwa!, kwa lugha rahisi, kipengele hiki kili 'just vanish into thin air!.

Na kipengele kinachokiuka katiba ya JMT ni hiki.

x. CHADEMA itashughulikia matatizo ya viongozi nawanachama kwa kufuata taratibu zilizowekwa kwa mujibu wa Katiba ya Chama, wala hata siku moja haitashughulikia mambo kama hayo Mahakamani. Mwanachama atakayeshindwa kufuata taratibu na ngazi za Chama hatavumiliwa na atafukuzwa uanachama.

Pasco

We Pasco utakuwa ni mburula mshika pembe!!!! Chama hakijakataa kuutambua uwepo wa mahakama na ndio sababu mzito kabwela akaacha kwanza aitafute haki mahakamani, baada ya mahakama kumpatia haki aliyostahili ndio na ufafanuzi juu ya katiba ya chama inavyoelekeza au kuagiza ulipotolewa na mwanasheria mkuu wa chama sasa huo udikteta uko wapi? Au unakumbusha Makonde alivyomzuia mzee Waryoba kutoa yake ya moyoni? Aibu kwenu msiokuwa na haya
 
Pamoja na wengi kucoment hakuna aliyejibu kwa hoja
ktk kile kilichoandikwa na Pasco mpaka sasa.
Ni dalili kilichowasilishwa kipo sahihi.
Badala ya kujibu hoja anashambuliwa aliyeleta hoja.
 
Last edited by a moderator:
wafuasi wa chadema wengi wao hawajitegemei kiakili,jambo ata liwe LA ukweli,ila kama linamuhusu Mbowe au Slaa wao mahaba mbele,Mbowe kadanga taifa kuwa anamkanda wa Bomu LA arusha kimya mpaka Leo,Mnyika nae ameacha kutumia akili,anawaza ataishi VP kwa anaojipendekeza
 
Udikteta una advantages zake pia. Kama umesoma histry vizuri ukiangalia mafanikio yaliyoletwa na Mussolin akiwa na Fascists, Hitler na Nazis wake. Only if ukipata patriotic leaders (dictator).
 
Msingi wa hoja yako Pasco kwamba Chadema ni chama cha kidikteta ni dhaifu kwasababu sababu zote unazotoa hujazitetea vizuri kuthibitisha ukweli wake.

Kwamba Chadema walibadilisha katiba pasipo maamuzi ya vikao halali vya chama, tukuulize wewe na msajili wa vyama mabadiliko hayo au katiba hiyo mpya ya Chadema ilikubaliwa vipi na ofisi ya msajili wa vyama. Mjadala wako juu ya hii hoja ungeonekana uko balanced kama ungejadili "role" ya ofisi ya msajili katika "uchakachuaji" huo wa katiba ya Chadema. Vinginevyo hoja yako inaonekana ina msukumo mkubwa wa hisia kuliko "facts".

Kwamba Chadema wanavunja katiba ya nchi kwa kukataza wanachama wake wasikishitaki chama, wewe mwenyewe kwenye hili andiko lako unaonekana unaelewa kwamba si kweli; maana umegusia kwamba wanachama wa Chadema wanaruhusiwa kukishtaki mahakamani chama. Habari ya mwanachama kufukuzwa kwa kukishtaki chama ina ukweli pale tu mwanachama anapokuwa ameshindwa katika hiyo kesi yake dhidi ya chama. Binafsi hapo sioni kama mtu unahitaji elimu ya sheria kuona kwamba katiba ya nchi haijavunjwa.

Hitimisho: kwenye kujadili hizi hoja Pasco "emotions" zako zimeonekana wazi zikizidiwa na "logic". Hasa leo; sijui matokeo ya mahakama hukuyapenda? Otherwise I still respect your ability to discuss issues. You are among the minority who often present "substance" here at JF. The gaffe didn't hurt too much, IN MY OPINION.
 
Msingi wa hoja yako Pasco kwamba Chadema ni chama cha kidikteta ni dhaifu kwasababu sababu zote unazotoa hujazitetea vizuri kuthibitisha ukweli wake.

Kwamba Chadema walibadilisha katiba pasipo maamuzi ya vikao halali vya chama, tukuulize wewe na msajili wa vyama mabadiliko hayo au katiba hiyo mpya ya Chadema ilikubaliwa vipi na ofisi ya msajili wa vyama. Mjadala wako juu ya hii hoja ungeonekana uko balanced kama ungejadili "role" ya ofisi ya msajili katika "uchakachuaji" huo wa katiba ya Chadema. Vinginevyo hoja yako inaonekana ina msukumo mkubwa wa hisia kuliko "facts".
Mkuu ycam, kwanza asante kwa objectivity yako katika bandiko lako hili. Chama kikishapata usajili wa kudumu, kiko huru kubadilisha katiba yake wakati wowote kitakapotaka, Chadema hakikumweleza Msajili kuwa kinabadilisha katiba kuunda katiba mpya, bali kilitoa taarifa ya kufanya mabadiliko ya katiba yake. Kwa vile katiba ndio roho ya chama, kila kipengele kilichomo kwenye katiba husika, kiliwekwa kwa sababu. Logic ya kuwepo kwa kipengele kile ni kuzua usultani na uongozi wa kifalme ndani ya Chadema na kwa maoni yangu this is the essence ya jina la Chadema kuwa ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo.

Katika mabadiliko hayo ya 2006, kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Chadema, kwangu alikanusha kuwepo kwa kipengele hicho cha ukomo wa madaraka, rejea hapa
WanaJF,

Pamoja na kuwa sitaki kuingilia mjadala katika hatua hii, naomba kuthibitisha kuwa:
I) Katibu Mkuu wa Chadema, kwa mujibu wa Katiba na Kanuni ya Chadema, ndiyo mhimili mkuu na mwenye jukumu la kutunza na kuhakikisha Katiba ya Chama inatunzwa.

2) Nataka kuwahakikishia wanachadema wote, kuwa nilikuwepo nimekuwa ndani ya Chadema kuanzia 1998 ambapo nilikuwa Makamu Mwenyekiti Bara, na baadaye 2003 Kaimu Katibu Mkuu, na hatimaye Katibu Mkuu. Hivyo nimeshiriki kikamilifu kuandaa Katiba ya 2004 na pia Katiba ya 2006 baada ya Rebranding ya Chama. Nataka niwahakikishie wanachadema, hakuna toleo lolote la Katiba ndani ya Chadema imeweka " muda wa Uongozi kuwa vipindi viwili tu", kuanzia Katiba aliyoiasisi Mzee Mtei na kupitishwa na Mkutano Mkuu, wala si ya 2004 au ya 2006. Kama kuna mtu anasema ilikuwepo na imeondolewa kinyemela, basi aonyeshe kifungu hicho kwenye Katiba yeyote ile, au miniti za kikao chochote kile.

3. Mimi Dr Slaa, ndiye niliyewasilisha Miniti za Mkutano Mkuu wa 2006 kwa Msajili ikiambatana na Katiba iliyopitishwa na Mkutano Mkuu. . Hivyo, ninathibitisha kuwa hakuna kipengele chochote kilichoingizwa kinyemela.
Soma hapo kwenye bold. Kisha msome JJ. Mnyika hapa.
Pasco, Pamoja na marekebisho niliyoeleza kuhusu majibu ya Dr Slaa kwamba katiba ya 2004 iondolewe kwenye orodha kama nilivyochangia hapo awali. Katiba ya mwaka 2004 haiwezi kuwa ushahidi wa hayo madai yasiyokuwa ya kweli. Katiba ya mwaka 2004 mimi ninayo hapa nilipo, kwenye kifungu cha 6.3.2 kina kipengele cha 'muda usiozidi vipindi viwili katika cheo kimoja kwa ngazi moja'. Hata hivyo, huu sio ushahidi wa kwamba kipengele hiki kimeondolewa 'kinyemela'. Hii ni kwa sababu tatu; Mosi, 2006 hatukuwa tunafanya marekebisho ya katiba kwa maana ya kuondoa au kuacha kifungu cha katiba ya mwaka 2004. Tuliandika katiba upya, ndio maana tarehe 13 Agosti 2006 pale PTA tukafanya uzinduzi wa katiba mpya ya CHADEMA. Kwenye mchakato wa kukusanya maoni ya katiba mpya na hatimaye maandalizi ya rasimu ya katiba mpya, hili suala halikuingia kabisa. Halikupitishwa kwenye mapendekezo ya sekretariati, kamati kuu, baraza kuu na hata mkutano mkuu kwa kadiri ya kumbukumbu zangu. Hivyo huwezi kuzungumzia 'kuondoa kinyemela' kipengele ambacho hakikuingia. JJ
Nadhani unaweza ku compare na ku contrast.

Kwamba Chadema wanavunja katiba ya nchi kwa kukataza wanachama wake wasikishitaki chama, wewe mwenyewe kwenye hili andiko lako unaonekana unaelewa kwamba si kweli; maana umegusia kwamba wanachama wa Chadema wanaruhusiwa kukishtaki mahakamani chama. Habari ya mwanachama kufukuzwa kwa kukishtaki chama ina ukweli pale tu mwanachama anapokuwa ameshindwa katika hiyo kesi yake dhidi ya chama. Binafsi hapo sioni kama mtu unahitaji elimu ya sheria kuona kwamba katiba ya nchi haijavunjwa.

Hitimisho: kwenye kujadili hizi hoja Pasco "emotions" zako zimeonekana wazi zikizidiwa na "logic". Hasa leo; sijui matokeo ya mahakama hukuyapenda? Otherwise I still respect your ability to discuss issues. You are among the minority who often present "substance" here at JF. The gaffe didn't hurt too much, IN MY OPINION.[/QUOTE]
Demokrasia ndio msingi mkuu wa Chadema, ikiwa na maana pana zaidi ya kuheshimu haki na uhuru wa kutafuta haki popote kwa mujibu wa katiba!. Zuio hili ni la nini haswa?!.

Pasco.
 
Back
Top Bottom