carbohydates
JF-Expert Member
- Oct 13, 2026
- 260
- 607
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimelaani kitendo cha Jeshi la Polisi kumnyima dhamana kiongozi wake, Mhe. John Pambalu, baada ya kukamilika kwa mahojiano yake. CHADEMA kimeeleza wasiwasi wake kuwa hatua hizo zinaashiria mpango wa kumfungulia kesi za ugaidi au uhaini ambazo hazina dhamana.
Kupitia taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi, Brenda Rupia, chama hicho kimetaka Jeshi la Polisi kuacha mara moja kutumika kama chombo cha kukandamiza upinzani na kuacha tabia ya kuwabambikizia viongozi kesi zisizo na dhamana ili kuathiri uhuru wao.
Aidha, CHADEMA kimelitaka jeshi hilo kutekeleza majukumu yake kwa haki, weledi na kwa kuzingatia Katiba ya nchi badala ya kufuata matakwa ya watawala, kikitilia mkazo kuwa hakuna mtu aliye juu ya sheria na haki za Watanzania wote zinapaswa kulindwa.
Chanzo: Chadema official
Soma Pia: Pambalu wa CHADEMA atuhumiwa kwa ugaidi