CHADEMA imeelani vikali kukataliwa kwa dhamana ya John Pambalu

carbohydates

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2026
Posts
260
Reaction score
607
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimelaani kitendo cha Jeshi la Polisi kumnyima dhamana kiongozi wake, Mhe. John Pambalu, baada ya kukamilika kwa mahojiano yake. CHADEMA kimeeleza wasiwasi wake kuwa hatua hizo zinaashiria mpango wa kumfungulia kesi za ugaidi au uhaini ambazo hazina dhamana.

Kupitia taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi, Brenda Rupia, chama hicho kimetaka Jeshi la Polisi kuacha mara moja kutumika kama chombo cha kukandamiza upinzani na kuacha tabia ya kuwabambikizia viongozi kesi zisizo na dhamana ili kuathiri uhuru wao.

Aidha, CHADEMA kimelitaka jeshi hilo kutekeleza majukumu yake kwa haki, weledi na kwa kuzingatia Katiba ya nchi badala ya kufuata matakwa ya watawala, kikitilia mkazo kuwa hakuna mtu aliye juu ya sheria na haki za Watanzania wote zinapaswa kulindwa.
Chanzo: Chadema official

Soma Pia: Pambalu wa CHADEMA atuhumiwa kwa ugaidi

​
 
Angalau amejulikana yuko wapi! Hilo ni la baraka tele. Mengine wanajihangaisha bure
 
Wasiwasi wa nini?

Mahakama zipo zitumike. Kelele hazitosaidia zaidi ya kuleta taharuki
 
Chama Cha magaidi naomba serkali ikifute

USSR
 
CCM kwishaaa...kwishaaa kabisaaaa....!

Salama yenu iliyobaki ni hii ya kujisalimisha kwa vyombo vya Ulinzi na Usalama viwaokoe.

Polisi wenyewe washamba wa fikra.Hawana ushahidi nje ya kujenga hofu kwa wengi eti waogope.

Hakuna Kesi Ya Uhaini/Ugaidi hapo na mnazidisha hasira
za Raia wengi tu.

Ni Zama Mpya za CCM kuondolewa kwa pressings za kila aina na hata Magaidi/Mahaini OG, yanakwenda kuingilia hapo hapo maana mnayapenda sana na yanawasikia.

Washamba kabisa wa Current Political Situation nyie.

Mnabomolewa na Heche kwa Hoja za Kiwango cha Juu mno ambazo mlipaswa kuzijibu na hamuwezi mnaishia kupiga porojo.

Yaani CHADEMA sasa wanapiga Fataki level ya Vitongoji,Vijiji na Kata sasa na mwitikio wawatu ni wa kutisha na wanachangiwa Pesa on the spot ili waelekee kituo kinachofuata ..mnaona Ni kawaida tu?!!!Kweli.??

Kwaherini...Mmejiamini mtapora Uchaguzi....haipo.!.Kwa kuua watu mtaweza ila kuna Wengine wataingilia kuokoa hilo.
 
Ni serikali ya kijinga pekee ndiyo inaweza kupambana na wananchi wake
 
Wasiwasi wa nini?

Mahakama zipo zitumike. Kelele hazitosaidia zaidi ya kuleta taharuki

Huna unalojua wewe Chawa uchwara.Muulize Samia au Makonda.

Ni mpango Mkakati wa CCM kupunguza tishio la eti CCM
kuja kupoteza Ubunge wa Jimbo Nyamagana tena.
Pambalu ndiye Mbunge wa Nyamagana kipindi chote kumrithi Wenje.
Aliporwa na CCM-2020..

Pita vijiwe na viunga vya Nyamagana kisha anzisha mjadala Juu yake.

2025-CCM Mliokolewa na No Reforms No Election..
Mlikuwa mmeshajaa kwenye mfumo na huyo Nzilamingi..Muulizeni hata yeye .

Kilikuwa Ni Zaidi ya Kichapo cha Mbwa Koko.
 
Chama Cha magaidi naomba serkali ikifute

USSR

Ukiwa na roho ya shetani, kila wakati unaota uovu. Kwa sababu CHADEMA na viongozi wake wanaitafuta haki, hakika, kwa hekima ya Muumba, utafutika wewe kabla ya CHADEMA na wapigania haki.
 
Kulaani vikali maana yake nini?
Umuhimu wake nini?
Manufaa yake nini?
Wenzenu wanasema mpo predictable. Mnaongea ongea baadaye mnasahau!
Kule Congo DRC hadi Rais mstaafu amechukua hatua.
 
Kulaani vikali maana yake nini?
Umuhimu wake nini?
Manufaa yake nini?
Wenzenu wanasema mpo predictable. Mnaongea ongea baadaye mnasahau!
Kule Congo DRC hadi Rais mstaafu amechukua hatua.
******* hawana kitu hakuna mwenye pumbu za chuma anayeweza kuliamsha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…