Benson Mramba
JF-Expert Member
- Oct 29, 2013
- 648
- 1,485
Awali ya yote nawasalimu sana Ndugu zangu wa JF baada ya kupotea kidogo kwa muda.
Pili nampongeza Mh. Freeman Mbowe kwa kuamua kujiengua kwenye kinyang'anyiro cha Urais na kumpisha Tundu Lissu. Aidha nampongeza kwa kunivumilia na kupokea ukosoaji wangu. Sitazungumza tena habari za Mbowe kwasasa labda litokee jambo lenye maslahi kwa Taifa ambalo yeye atahusika.
Tatu nampongeza Tundu Lissu kwa kuteuliwa na CHADEMA kuwa Mgombea Urais. Hongera sana. Binafsi namuunga mkono Tundu Lissu kuwa miongoni mwa Wagombea wa upinzani kwenye uchaguzi. Atanogesha uchaguzi na pia atamsaidia Rais Magufuli kujitathimi. Naamini hata wanaCCM wengi wanamuunga mkono maana atawasaidia kupata fedha toka chamani na kwa wagombea wao msimu huu wa uchaguzi baada ya njaa ya muda mrefu. In short I endorse Mr. Lissu but I will not vote for him.
OK nirudi kwenye mada sasa, Kwanini nasema Lissu amebebeshwa Jumba Bovu? Kwa maoni yangu ni kwamba CHADEMA hii ambayo Lissu anapeperusha bendera yake kwenye uchaguzi huu ni jumba bovu kwa sababu kuu mbili:-
1. CHADEMA ya Lissu kwenye uchaguzi huu tofauti na ya miaka iliyopita ni CHADEMA dhaifu sana kitaalum, oganaizesheni na kuaminika kwake na viongozi wake kwa jamii yetu. Hivyo haiweze hata kwa nusu kukabiliana na CCM labada na ACT au NCCR-Mageuzi.
CHADEMA ya sasa kama ambavyo tumekuwa tukisema ni CHADEMA ambayo think tank yake ni John Mrema, Reggy Munis, Sugu, Lema, Mnyika na Msigwa watu ambao ni mahodari wa hotuba na fitina ila hawana mipango kabisa na ni mafisadi ndani ya Chama. CHADEMA hii ni tofauti na ile ya akina Lwakatare, Komu, Marando, Prof. Baregu, Prof. Safari, Prof. Kitila Mkumbo, Dr. Slaa n.k. Hii ni chadema dhaifu sana kitaaluma.
CHADEMA ya sasa ni CHADEMA ambayo viongozi wake wa chini na vijana wake ni dhaifu sana, waoga na wamekuja kutafuta fedha na fursa ndani ya Chama tofauti na CHADEMA ile yenye Redbridge imara na inayotisha, CHADEMA yenye viongozi wanaojitoa Mali na hali zao, CHADEMA iliyokuwa na viongozi wafiachama na wanachama wanaokipenda chama na kuwaamini viongozi wao.
CHADEMA ya sasa ina viongozi ambao ni wezi hawaaminiki hivyo haiwezi kuchangisha hata fedha za kampeni. CHADEMA ambayo hata ikitembeza kikapu kwenye mikutano hakuna wa kuchanga kwasababu wanaamini fedha zitaliwa tu. CHADEMA ambayo viongozi wamethubutu kula pesa za matibabu ya mwenzao aliyepigwa risasi 16. Badala ya kulia nae wakafanya matatizo yake ni fursa kwao.
CHADEMA ya sasa haina fedha na haiaminiki. Haina uwezo wala watu wa kutafuta fedha au wanaoweza kuaminika wakakopeshwa. Haiwezi kuhamasisha maandamano ya vijana kujitoa muhanga dhidi ya vitisho vya dola. Namsikia Lissu akisema habari ya kuingia barabarani. Nakuapia kwa viongozi hawa wa CHADEMA hakuna mtu mjinga wa kutoa uhai wake au kupata majeraha kwa ajili yao kwasababu sio wakweli.
2. CHADEMA ya sasa ina wagombea dhaifu sana wa Ubunge kuliko hata ile ya mwaka 2005. Wabunge wenye kamsuli kidogo wameshakaa miaka 10 madarakani na hawafiki 10. Wana wakati mgumu wa kuonyesha walichofanya kwa miaka hiyo 10 na kwa kawaida watu wanakuwa washakuchoka.
Wagombea wengi wa Ubunge wa sasa ni dhaifu kisiasa, kielimu na kirasilimali. Hawawezi kupambana na wagombea wa CCM hata kidogo. Wagombea wengi majimboni ni wale waliokuwa wanataka Vitimaalum wamelazimishwa kugombea majimboni ili angalau wachange change kura kwa ajili ya ruzuku siku zijazo. KUMBUKA RUZUKU INATEGEMEA IDADI YA KURA ZA WABUNGE SIO RAIS.
Sasa kama huna wagombea imara wa Ubunge utashindaje Urais? Isitoshe chama chenyewe hakina hata hela ya kampeni? CHADEMA hii ya sasa ni JUMBA BOVU limemwangukia Lissu. Kuna majimbo hayana wagombea na mengine yana wagombea wawakilishi tu ili karatasi ya kura isikose nembo ya CHADEMA sio Wagombea shindani. Muda ungekuwepo tungechambua mgombea mmoja baada ya mwingine wa CHADEMA kwenye kila jimbo.
Siku zijazo nitatoa sababu za Lissu kushindwa ambazo ni udhaifu wake binafsi ili siku matokeo yakitangazwa tukumbushane isiwe tumeshtukizwa. Naomba kuwasilisha