Uchaguzi 2020 CHADEMA imembebesha Lissu jumba bovu. Atashindwa lakini atatoa changamoto

Nimeandika uongo?
Tena umeandika ukenge mtupu .. chadema haina hela ? Ingeleta gari 20 za kampeni , ingetoa order ya kiwanda china kutengeneza vifaa vya uenezi kwa miezi 4 kama hawana hela? Juzi tu hapa wananchi wamechangia milion 350 za kuwalipia viongozi wa chadema unasemaje hawana ushawishi?..umeondoka Chadema lkn bado unamapenzi na chadema..rudi huko uliko hakuna wa kukushika mkono kamanda ... chadema ya Sasa imeimarika kuliko enzi hizo za padre slaa .. chadema ya Sasa ina vijana wapya na watu wazima wapya ..wamama wapya ..ndo chama klichotoa fursa kwa akina mama 68 kugombea majimbo, wkt hao unaowatumuza ccm wa wamtoa fursa kwa wqnawake 18 tu ... chadema tunaenda kuchukua nchi unaweza kubeza lkn hbr ndo hiyo ..rudi kundini mkuu na istoshe una mchango ndani ya chadema hata Kama sio mkubwa Sana ..rudi tuendeleze chama la wana
 
Thread of an embecile
 
Waambie CCM wakulipe kabisa fedha zao zote mwaka huu, maana kuanzia October hapo CCM ni chama cha upinzani
 
Umeeleza vema
 

Mkuu kwanza kwa wewe kuwa Platinum member ni heshima kuu hapa JF, Nakupongeza kwa kuwa wengi wetu tungependa tuwe na daraja lako.
Nina machache ambayo nitataka kukumbusha;
1) Alicho changia Mramba hapa hakina tofauti yeyote ikiwa umepata nafasi ya kuongea kwa uchambuzi na wafuatao, Prof. Safari, Rwakatare, Komu, Selasini, Waitara, Zitto Kabwe, Gekul, Prof. Mkubo, Prof. Baregu, Marando, Dr Slaa na wengine.

2) Lakini kwa kuwa The brain you have is your standard unaweza kusema utachotaka kusema.

3) Prof. Baregu aliniambia na naquote " you plan as if you will never die" na akaaniambia hichi kitu hakipo CHADEMA na hata unapolazimisha kwa kuwa faida yake itaonekana baadae , hakuna anae kuwa tayari kuku sikiliza.

4) Katika mazungumzo yangu na Prof. Safari japo kuna mengi aliyozungumza lakini nitaelezea moja tuu Kuna systemic deficiency katika mfumo wa kuendesha chama kiasi mawazo mbadala hayani nafasi ila ushabiki bila kuwakilisha hoja toshelevu ndio zenye nafasi CHADEMA.

5) Mh. Kommu anasema mfumo wa kundesha chama na matumizi ya pesa yana fanana sana na duka la mtaani. ' Mtu analipwa pesa haujui mantiki ya kulipwa na kwa nii analipwa kiwango hicho?" Huyu Bwana haipendi CCM kweli kweli, hataki hata kuisikia. Lakini anasema CCM wanao mfumo wa kuendesha chama ambao unweza kuuzungumza na wanachama wanatakiwa kuutii.

6) Na wote wanasema it is not a coincidence Mbowe -Chairman - non Graduate, Benson Kigaila- Deputy Secretary Gen. - non Graduate, Sec. Gen- Mnyika- Collage drp out, Mwalimu Deputy Sec Gen Non Graduate.

Ukitaka kuishi Chadema kwa amani na upendwe na viongozi uliowakuta lazima uwe "NYUMBU NA KASUKU" haya ni maneno ya viongozi waandamizi wasomi ambao bado wako CHADEMA waajiriwa.
MKUU SAFARI YA UPINZANI BADO NI NDEFU.
 
Kachukue buku Saba yako kwa polepole. Mmeishiwa hoja mmekimbilia viroja. Kweli CCM mna hali mbaya 😀
 
Anayefahamu majimbo ambayo CHADEMA hawajaweka wagombea ayataje hapa ili wengine tuyajue.

Kujusu kushindwa Lissu hilo ni dhahiri.
 
Hujui kitu wewe
 

..tatizo umesikiliza ma-graduate peke yao.

..ungesikiliza na hao college-drouputs, high school failures, na wengine walioko CDM.

..sikiliza pande zote ndiyo uje utoe hukumu.
 
Punguza chuki jombaa, endelea na maisha yako huko uliko maana ulipokuwa CDM hatujaona chochote na hata sasa huna legacy uliyoacha, so acha wenzio waendelee na kazi.
Kaulize
 
Umeandika sana ila hujui kitu. Viti maalum havihusiani na kura za Rais bali idadi ya wabunge wa kuchaguliwa
 
Hata matibabu ya Lissu uliambiwa hivyo hivyo kuwa zimechangwa ila waakubwa wakavunja akiba ya akaunti ya michango ya wabunge kwa matibabu hayo hayo. Wale walijilipia usiwe mjinga
 
..tatizo umesikiliza ma-graduate peke yao.

..ungesikiliza na hao college-drouputs, high school failures, na wengine walioko CDM.

..sikiliza pande zote ndiyo uje utoe hukumu.

Nitafanya hivyo bila kuchelwa kwa kuwa bado nina uhusiano bora kabisa na wengi tuu. Ila ukumbuke mwendo wa nyoka huongozwa na kichwa.
 

Ninahitaji kweli kuuliza Dr Slaa aliacha legacy gani wakati it speaks for itself? Sasa kwa nini niulize about you? Hakuna maana kingeonekana. Halafu mke mkiachana muache aendelee na maisha yake mapya....
 
Roho inakusokota na vile mkuu hakuoni bado unajitahidi sana lakini keep trying. Inategemea ataamka vipi.
 
Upo ccm lakini kutwa unahangaika na CHADEMA. Au na wewe ni afisa kipenyo?

Jengeni ccm yenu. Achana na chadema. Hawakuskilizi na hawatakusikiliza
 
Punguza chuki jombaa, endelea na maisha yako huko uliko maana ulipokuwa CDM hatujaona chochote na hata sasa huna legacy uliyoacha, so acha wenzio waendelee na kazi.
Hahaha bensi bwana. Ni mchumia tumbo tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…