22 August 2020
Tunduma, Songwe
Tanzania
CHADEMA imeomba vyombo husika vifuatilie tetesi za kuwepo mipango ya kuvuruga mchakato wa kuelekea katika hatua za kurudisha fomu za wagombea. Hivyo wameomba uchunguzi na hatua za haraka za kiuchunguzi zifanyike ili kama kweli mipango hiyo ipo basi vyombo husika vilivyoahidi kusimamia uchaguzi huru na haki vizuie njama hizo ovu.
Tayari wagombea kadhaa wa udiwani wa CHADEMA waliohudumu muda mrefu kabla mabaraza ya madiwani hayajavunjwa kufuatia kumalizika kwa kazi zao 2015 -2020 wameitwa kuhojiwa uraia wao.
CHADEMA inashangaa vipi viongozi hao waliohudumu katika Baraza la Madiwani la Halmashauri waanze kuhojiwa kipindi hiki kuelekea mchakato wa kurudisha fomu unaotarajiwa kuhitimishwa tarehe 25 Agosti 2020 ili waweze kuomba kuchaguliwa na wananchi wa Tunduma.
Madiwani teule waliopendekezwa na CHADEMA, mbele ya waandishi wa habari waongea kuhusu kupokea simu zilizopigwa na watu waliojitambulisha ni maofisa wa Idara ya Uhamiaji kuitwa kwenda kuhojiwa uraia wao. Diwani wa kata ya Sogea Tunduma alihojiwa kwa masaa kadhaa ktk ofisi za Uhamiaji Tunduma na kutakiwa kupeleka viambatisho vya vyeti vya kuzaliwa kesho kutwa Jumatatu tarehe 24 Agosti huku madiwani wengine wa CHADEMA walioshindwa kufika ofisi za Uhamiaji wakiendelea kuombwa kufika ofisi za Uhamiaji.
Viongozi wa CHADEMA Tunduma wanasema hizo ni njama za kutengeneza mazingira madiwani wa CCM wapite bila kupingwa katika uchaguzi wa Oktoba 2020. Kwani mmoja wa wagombea wa udiwani wa CHADEMA aliyeitwa Uhamiaji ana kaka yake ambaye ni mgombea wa udiwani wa CCM lakini huyu wa CCM hajaitwa kuhojiwa uraia.
Source : DSS Tunduma