Wakudadavuwa
JF-Expert Member
- Feb 17, 2016
- 17,506
- 16,003
Ndugu zangu,
Wakati umefika sasa baadhi ya viongozi wamemweleza Mbowe aache kuhadaa makamanda "kukubaliana na njaa, kuendesha chama kwa hela zao" ilihali yeye anatumia rasilimali za chama kuaafiri, kujilipa posho nk.
Kiongozi mmoja ambaye ni mwandamizi alisema "huwezi kuwaambia wenzako wajikite kwenye shughuli za chama kwa kutumia gharama zao, watoto wao watakula nini, watasomaje, hakuna kazi ya bure; viongozi wa dini wanakula madhabahuni, majaji na wanasheria wanakula kortini na sisi wanasiasa lazima siasa zitutunze"
Baadhi ya viongozi wamebeza kauli ya Mbowe kuwa "CHADEMA haichukui ruzuku", wameonyesha wasiwasi, wameenda mbali kwa kusema "ni nani kati yetu anajua kwa hakika mambo ya fedha ya Chadema miaka yote?"
Kumekuwepo pia na tuhuma za upendeleo wa wazi wazi ambao baadhi ya viongozi hao wamelalamikia. "Tunarudi tulikotoka,tulianza kutengeneza taasisi lakini sasa ni dhahiri tunaiona sura ya ubinafsi"
Muda unasema sasa!