CHADEMA ina mtaji mkubwa kisiasa kuliko CCM na ACT wazalendo, ruzuku na madaraka visiwaondoe kwenye reli

CDM kaza boti! mna mtaji mkubwa sana wa wanachama wenu!
Mkizidiwa wekeni bakuli mezani watu wanapiga donation maisha yanaendelea!
ILA mkataeni shetani na mambo yake yote na gilba zake zote ipo siku haki itatamalaki.
 
Chama cha maana kikichobakia Tanzania kinachotetea maslahi ya nchi ni CDM tu!!
 
Mimi pia najiuliza, hivi watanzania tungekua na tume huru ya uchaguzi na jeshi la polisi lisilopelekeshwa na akina pole pole, CCM ingekua madarakani kweli?

Sent from my TECNO W4 using JamiiForums mobile app
Hilo siwezi kujua kwa sababu pamoja na kwamba ccm inafanya figisufigisu kwenye chaguzi ila bado hadi leo ina wapiga kura wengi tu hasa akina mama na wazee,hivyo hata mimi natamani kuwe na uchaguzi uliyo huru kabisa halafu hali itakuwa vp maana sasa kumekuwa na imani ya kwamba kila chaguzi upinzani ndio unashinda ila ccm inatumia dola kujitangaza yeye kuwa ndio mshindi.
 
Acc ya chama imesoma ruzuku ya mwezi nov halafu kimya,ndio mkakati gani huo 🤣
 
Siasa ni mwanaharamu sana,yani juzi tu hapa A.C.T ilikuwa ndo kipenzi cha Chadema leo wamekuwa chui na paka!!
haya ngoja tuone nini kitafata.
 
Huwa najiuliza hivi Tanzania tungekuwa hatutumia Facebook na JF hivi hii chadema tungekuwa tunaiona kama tunavyoichukulia humu mitandaoni? Kwa maana huko mitaani chadema ingekuwa inazungumzwa kama ilivyo huku mitandaoni?
Kwani waliopo mtaani hawapo JF na Facebook ama mtaani wanaishi watu wasio ma smartphone!!

Hvi Lissu alipoenda porini Itilima huko na kukuta maelfu ya watu je huko nako walikuwa FB?

Kipindi cha Dr Slaa na Zitto bungeni kulikuwa na mitandao ya jamii? Je ilikuwaje CHADEMA ikapaa kiushawishi nchi nzima hadi kuwa chama kikuu.

Nasubiri majibu
 
Hata mimi nakubali JPM angeshinda of course sababu ya wajinga bado wapo wengi Tz hasa huko maporini. Ila kinachopingwa ni 80%+ haiingii akilini kabisa. Yaani majimbo na kata zote nchini zinaipenda CCM!!

JPM kma angeshinda basi ni 50-60% basi.... Kma tu US licha ya kelele kwa trump lakini Biden hajashinda kwa kishindo. So hiko ndio tume huru ingesaidia.... Hopefully na wabunge ingekua hivyo hivyo gap ya 60-40 ila sio majimbo yote.

Tuwe serious kidogo
 
Mimi ni mtu mmoja, sio taasisi. Usitumie neno "nyie" kuniongelea mimi mtu mmoja!
 
Ilitakiwa ukimaliza kuandika hapo useme umeingiza sh ngapi kwenye account ya chadema kwa ajili ya mafuta ya magari na kulipa watumishi
Ahahahahahahahajahah! Eti Chadema ina wabunge milioni 30 mtaani. Ahahahahahah! Wabunge walioshindwa kupiga kura, wakashindwa kulinda kura zao na wakashindwa kuingia mtaani kudai "ushindi" wao hadi Mgombea Lissu Ubelgiji akahama nchi kwa aibu! Ahahahahahah! Hongera sana kwenu WABUNGE MILIONI 30!!!!!
 
Mie nimeuliza tu swali mkuu,maana kilichopo mitandaoni si sawa na huko mitaani ndio maana hata yale maandamano ya Lissu kwa kuangalia hali ilivyokuwa mitandaoni ilishangaza kuona siku ya tukio watu mitaani wanaendelea na shughuli zao kama kawaida kama hakuna kilichotokea wakati mitandaoni hali ilikuwa tofauti.

Kwahiyo naona chadema ina nguvu kubwa sana mitandaoni kuliko huku mitaani,sisemi kuwa haina watu huku mitaani ila haipo kama ambavyo ilivyo mitandaoni.
 
Mkuu hta Mobutu DRC alikataliwa ila mbona wapinzani walipoitisha maandamano yalifeli? Vp Museveni 2016 Besigye alipoitisha maandamano?

Mbona Lissu alipotua kutoka ubelgiji watu waliandamana bila polisi kuingilia? Kma wangeruhusu alafu watu wasijitokeze hapo ungekuwa na hoja.

But baada ya vitisho then mnakuja kujisifia kuwa tupo mitandaoni sidhani kma ni sahihi.

Kenyatta hakuzuia maandamano ya Odinga na wote tuliona nguvu yake mpka akajiapisha Urais. Nyie mngeachia tu then tungeona kma yangefeli ili ssa tufanye analysis fair.
 
Tatizo mkuu sio tu watu hawajafanya hayo maandamano bali watu walikuwa bize na shughuli zao wala hakukuwa na dalili zozote kuonesha kuwa watu walikuwa teyari kwa maandamano ila polisi ndio kikwazo,na ukiangalia mitandaoni watu walikuwa wanaonesha kuwa wameshachoka hakuna tena wanalohofia liwalo na liwe. Hiyo ndio ilikuwa hali ya mitandaoni,sasa ajabu tena watu hao kuogopa mkwara wa polisi.

Huo ni mfano mmoja tu lakini kiujumla chadema ya mitandaoni ni tofauti na huku mtaani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…