jingalao
JF-Expert Member
- Oct 12, 2011
- 36,197
- 29,717
Hii si sawa na lazima isemwe.
Mhe.Rais samia ameendelea kuwa mwenye nia njema sana ya kuondosha malalmiko ya jamii hususani katika muktadha wa kisiasa.
Baada ya tuhuma za uongo na zilizosukwa na kupambwa na vyama vya upinzani nchini Tanzania na hususani wafuasi wa chadema dhidi ya hayati Magufuli .Rais Samia aliamua kuchukua mrengo laini na wa kimaridhiano ili kuhakikisha kama nchi tunaenenda na siasa za kistahimilivu na maridhiano.
Hakika hakuna na haikuwahi kutokea hapa nchini na pengine Afrika kuona Kiongozi aliopo madarakani anajikita na sera hii ya kipekee na hasa ikizingatiwa alikuwa amechukua madaraka kutoka kwa mtangulizi wake ambaye alisemwa vibaya iwe kwa hoja za ukweli au za kusingiziwa .
Rais samia hakuishia kusema tu bali kwa vitendo aliruhusu uhuru mkubwa sana kwa vyama na jamii ya wanasiasa kufanya siasa za kistaarabu naamini aliamini atakata kiu ya wapinzani.
Bila shaka lengo lake lilikuwa ni kuona nchi ya utulivu na ustahimulivu wa kisiasa,maoni mbadala na ushirikishaji wa kiwango kikubwa.
Wapo wengi walioshuku juu ya sera hii kwani walijua hulka ya wapinzani nchini lakini pia malengo ovu ya nchi za nje wanaopambana kuihujumu Tanzania na kuiacha iwe sehemu isiyotawalika ili kunyonya rasilimali.
Hata hivyo Dr Samia Suluhu Hassan hakuacha kuitetea na kuisimamia sera yake ya 4R akiamini ni sera muhimu na itakayobadilisha hali ya kisiasa.
lipo somo muhimu ambalo mhe.Rais anaendelea kujifunza na watanzania wazalendo wanamakinika nalo ..ya kwamba hata ufanye nini au lolote linaloombwa na wapinzani bado wakinzani watatafuta mbinu za kuchonganisha ili tu lengo ovu litimie.
Sikutarajia kuona Chadema wakija na mbinu zile zile kutaka kuweka rehani maslahi ya amani ya nchi hii.
Inashangaza kuona watu wale wale wakija na mbinu ile ile ya kutaka kuzua taharuki katika nyakati ambazo yupo kiongozi asiyependa taharuki.
Inatufunza na ninajifunza kuwa ...kumbe issue sio Changamoto zinazotajwa kama sababu za taharuki bali yupo au zipo au wapo watu nyuma ya pazia wasiotaka kuona nchi inatulia na kujikita kwenye afua za maendeleo.
Hivyo bila shaka sasa naaendelea naona ni muhimu kama nchi tukatambua na kuelimishana kuwa wapo ,yupo anayetuchezesha kama wanasesere akiwa na lengo moja tu...kuchota mali zetu na kutuacha utumwani.Huyu ndiye kubwa la maadui na hajaanza leo na wala hatamaliza leo.
CCM kama chama kilichotutoa utumwani kwa kiasi flani bado ndio nguzo pekee ya kuhakikisha tunatoka utumwani kikamilifu.
Tunayoshuhudia leo na yanayopitiwa na viongozi wetu ni yale yale ya miaka kabla ya 61...
Hivyo basi hatuna budi ya kuunga mkono jitihada za chama na serikali.
CCM iendelee kushika hatamu na ikibidi muundo wa chama na serikali urejee kikamilifu kwani ndio njia iliyo sahihi.
Ikitokea siku nikiwa mtawala wa nchi hii sitaangalia sura ya mwenyeji au mlami bali maazimio,mazindiko na makubaliano ya siku ya uhuru ni lazima kwa njia yoyote yatekelezwe yaani kazi iliyokwama lazima iendelezwe.
KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!!